TAASISI ya utafiti wa samaki na uvuvi (TAFIRI) inadaiwa kukalia matokeo ya utafiti wa aina mpya ya samaki wanaofaa kupandwa katika ziwa Ikimba lililopo wilaya ya Bukoba mkoani Kagera.
Hayo yamebainika wiki hii kwenye baraza la madiwani baada ya mwenyekiti wa kamati ya uchumi, ujenzi na mazingira Aristides Modest kutaka upandaji wa aina mpya ya samaki katika ziwa hilo ili kukuza uchumi wa wananchi wa wilaya hiyo.
Alisema kamati yake imeona rasilimali hiyo haijatumika ipasavyo na hivyo kupendekeza upandaji wa aina mpya ya samaki katika ziwa hilo ambao hautaathiri viumbe wengine katika ziwa hilo.
Pia alipendekeza wilaya kuandaa utaratibu utakaoweze wananchi wanaozunguka ziwa hilo kundesha shughuli za kilimo cha umwagiliaji na kubuni miradi mingine ya kuiongezea halmashauri mapato.
Naye kaimu ofisa kilimo, ushirika na uvuvi Mashauri Bebirasi alisema tayari taasisi ya utafiti wa samaki na uvuvi (TAFIRI) iliyopo jijini Mwanza ilishafanya utafiti wa kufahamu aina ya samaki wanaotakiwa kupandwa ziwa Ikimba.
Pia alilieleza baraza hilo kuwa ofisi yake itaanza kufuatilia matokeo ya utafiti huo ili kubaini aina ya samaki wanaopendekezwa kupandawa katika ziwa hilo linalodaiwa kuwa na tope na aina chache ya samaki.
Hata hivyo diwani wa kata ya Kishanje Thadeus Mutarubukwa alitahadharisha upandaji wa samaki wapya kuwa utahatarisha samaki waliopo kama ilivyo kwa sangara ambao wanadaiwa kupunguza aina nyingine za samaki ndani ya ziwa Victoria.
hawa watu hawako serious na kazi zao. mfano mzuri nchi za jirani kenya uganda etc na nchi nyingine ambazo zinaendelea kiuchumi kama nigeria na southafrica wamepiga hatua kubwa katika fish farming to be specific. kati ya majukumu ya TAFIRI ni kutoa assistance kwa jamii in terms of fish farming educative materials and seminars ambazo si tu zitatoa changamoto ila pia zitatoa utalam ambao in the long run utainua sector fisheries na kuongeza kipato kwa jamii na nchi kwa njia ya mapato. inakuaje tangu taasisi ya TAFIRI ianzishwe hamna iformation yoyote kwenye tovuti yake in terms of documents, research files and fish markets hapa nchini. sasa tutapat wapi habari kuhusu ufugaji wa samaki nchini..!! katika hizi taasisi watu wafanye kazi kukuza uchumi sio mapambo na kukaa ofisini kula viyoyozi, leo ukitaka kushiriki katika tafiti za tafiri unatakiwa kulipa $2500 kwa wanafunzi na watafiti wa kimataifa na kitaifa, this is outrageous…! tutafika kweli wazee