Kesi ya Manji dhidi ya Mengi kuendelea

Jamii Africa

Yusufu ManjiMahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Juni 7, mwaka huu itatoa uamuzi wa kuyapokea au kutoyapokea kama kielelezo cha ushahidi magazeti yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Mfanyabiashara Yusuf Manji ambaye ni mlalamikaji katika kesi ya kashfa ya madai ya Sh moja, aliyomfungulia Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi.

Katika kesi hiyo Manji anataka Mengi na kituo chake cha ITV kumlipa Sh moja kwa kumkashifu kwa kumuita fisadi papa na mmoja kati ya watu wanaofilisi rasilimali za nchi.

Kesi hiyo ilikuja jana kwa ajili ya mlalamiaji kuendelea kutoa ushahidi wake ambapo alidai kutokana na kashfa hiyo ya kuitwa fisadi papa kwenye magazeti na kuchapwa kwenye nakala zaidi ya 2000 na kushushiwa hadhi yake mbele ya jamii.

Wakili wa Mengi Michael Ngalo alidai mbona makampuni mengi yanayochapisha magazeti hayo ni mengi lakini hajayashitaki.

Baada ya mabishano ya kisheria kati ya mawakili hao wa upande wa mashitaka na utetezi, Hakimu Mustapha Siyani kuwaambia kuwa atatoa uamuzi dhidi ya hoja hizo Juni 7, mwaka huu na kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Juni 10, mwaka huu.

Hakimu Siyani ameanza kusikiliza shauri hilo leo baada ya aliyekua akisikiliza awali Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Aloyce Katemana kujitoa bila kutoa sababu za kujitoa kwake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *