Kuna tofauti gani katika aina zote za dawa za meno?

Jamii Africa

Ukijaribu kwenda kwenye maduka makubwa utashangazwa na idadi ya dawa za meno utakazokutana nazo. Zipo aina nyingi na ni msululu wa dawa umepangwa kwenye makabati baadhi zikifanya kazi ya kung’arisha meno, zingine kwenye fizi na zingine zina ladha nzuri tu.

Pamoja na kuwepo kwa msululu wa dawa hizo lakini mwisho wa siku, hizo zote ni dawa za meno tu na hakuna cha ziada. Hata hivyo swali, Je, kuna utofauti gani katika dawa zote hizo?

 

Jibu lake linaweza kukushangaza sana…

Kiuhalisia dawa zote za meno ziko sawa ila wazalishaji huongeza vitu kidogo tu kwa ajili ya kuvutia wateja kwenye soko. Hakuna utofauti mkubwa sana katika aina mbalimbali za dawa hivyo huhitaji kutumia nguvu kubwa kufikiri ni aina gani ya dawa inakufaa.

Kwenye matangazo mengi ya dawa, utaona wakisema Madaktari 9 kati ya 10 wanashauri utumie aina fulani ya dawa lakini hakuna ukweli wowote katika hilo bali uhalisia ni kwamba idadi hiyo ya madaktari hushauri watu kusafisha vinywa kwa kutumia dawa za meno. Ndiyo maana yake halisi.

Madaktari wa meno huwa hawashauri kutumia aina fulani ya dawa ya meno (ila pale tu dawa hiyo inapokuwa na umuhimu kwa kundi fulani la watu) ila wanataka utumie aina yoyote ya dawa kusafisha meno.

Kwa wazalishaji wa dawa hizo ili dawa yako iweze kukubaliwa na serikali ni lazima ifanye kazi mbili muhimu ambazo ni:-
1) Kuboresha harufu ya kinywa na
2) Isimdhuru mtumiaji.

 

Madini yaliyopo kwenye dawa nyingi za meno:

Dawa zing’arishazo meno
Dawa ya meno yenye madai ya kung’arisha meno zaidi tofauti na dawa nyingine huwa na kiwango kikubwa cha msasa ndani yake (kichubuo) au nyongeza ya madini ambayo hukwangua sehemu ya mbele ya meno.

Hata hivyo, ni vyema kutambua kuwa matumizi makubwa ya dawa hizo huweza kuharibu kabisa tabaka gumu la meno (Enamel layer) na kusababisha athari kubwa.

Dawa kwa tabaka gumu la meno (Enamel repair toothpaste)
Hizi ni dawa ambazo huwa na madini ya ‘Calcium’ ambayo huusika kwenye kutengeneza tabaka gumu la meno (Enamel layer). Zenyewe hufanya kazi ya kuondoa uchafu ukaao katikati ya meno kwa haraka zaidi.

Kumbuka kwamba tabaka gumu la meno (Enamel) haliwezi kurudishwa kirahisi hivyo dawa hizi huwa na athari kidogo kwenye tabaka hili ndani ya muda mrefu.

Dawa kwa ajili ya meno dhaifu
Meno dhaifu ni tatizo baya sana hasa kwa watu ambao ni wapenzi wa vitu vya baridi. Dawa zitumikazo kutibu meno dhaifu huwa na madini ya ‘Potasium’ kama kiungo kikuu ndani yake ambayo hutumika kutuliza neva zilizopo kwenye meno.

Hivyo kama ni mtumiaji mzuri wa dawa hizi hutaweza kusikia ganzi kwenye meno pamoja na fizi zako pale unapotumia vitu vya baridi au vitamu sana.

Dawa zinazozuia meno kutoboka
Pia hujulikana kama dawa za ‘Floride’, Dawa hizi huwa na kiwango kikubwa cha Floride tofauti za dawa zingine za kawaida. Pia kuna dawa za ulinzi wa meno ambazo huwa na kiwango kikubwa cha Floride kwa ajili ya tabaka la jino.

Hii inaweza kufanyika kupitia kuongeza madini ya ‘Floride sodium’ kwenye dawa ya meno, ambapo husaidia kuboresha afya ya tabaka gumu la meno.

Dawa nyingi za meno zina madini ya floride sodium, hivyo upataji wa madini haya ndani ya mtumiaji ni wa lazima bila kujali unatumia aina gani ya dawa.

Hata hivyo japokuwa ni vizuri kushauriana na daktari wa meno kuhusu dawa gani utumie. Lakini usafishaji wa meno yako kwa namna nzuri ni jambo muhimu bila kujali unatumia aina gani ya dawa ya meno.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *