Mambo 13 yatakayokusaidia kukamilisha furaha katika maisha

Jamii Africa
BURUNDI: Serikali imesema ni lazima Wapenzi wahalalishe mahusiano yao(Kuoana) kabla ya kuisha kwa mwaka huu. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Terence Ntahiraja amesema hiyo ni moja ya njia ya kukuza maadili nchini humo. . Ameongeza kuwa miaka ya karibuni kumekuwa na ongezeko la mimba za mashuleni hivyo lazima jitihada zichukuliwe kukabili changamoto hiyo.

Kila mtu anapenda kuwa na furaha, lakini kuna wakati huzuni hutawala na mtu kushindwa kufanya atakayo. Furaha haipatikani isipokuwa umechukua hatua kuitafuta.  Ukitaka furaha katika maisha yako fanya mambo yafuatayo:

  1. Jitolee kufanya kazi za kijamii
  • Jumuika na marafiki zako majukumu ya kijamii kama kufanya usafi mitaani, kuwatembelea yatima. Pia wasaidie wenye uhitaji. Itakusaidia  kuboresha afya ya akili na mwili kwa ujumla.
  1. Tabasamu wakati wote
  • Hata kama una jambo linalokupa shida, jitahidi kuonyesha uso wa tabasamu na kuyachukulia matatizo yako kama changamoto ambazo zinapita.

  1. Tafuta marafiki wapya
  • Itakufanya usijisikie vizuri kukaa na watu ambao wanakujali na kuheshimu hisia zako. Uwe muwazi kwa mahusiano mapya, ikiwa ni mtu umekutana naye ofisini, kanisani, sokoni au kwenye mazoezi. 
  • Hakikisha  unajenga na kuimarisha mahusiano mazuri marafiki wapya ili uzidi kupata fursa. Tafiti zinaonyesha kadiri mtu anavyojumuika na watu wengine ndivyo unakuwa na furaha.
  1. Kubali Baraka ulizopata
  • Andika kwenye daftari mambo mazuri uliyoyapata katika maisha yako. Unapofanya bidii kuangalia upande wa mazuri, inasaidia kuwa na mawazo chanya na kuwa mwenye furaha daima. Epuka kufikiri mambo mabaya kwa muda mrefu.
  1. Fanya mazoezi
  • Fanya mazoezi mepesi kwa dakika 15 hadi 30 kwa siku itakusaidia kuiweka hali ya mwili wako sawa. Jenga tabia ya kufanya mazoezi kila siku, itakuondolea msongo wa mawazo na upweke.

  1. Samehe na sahau
  • Unaweka vinyongo moyoni? . Wasamehe waliokukosoa na sahau mabaya yote uliyotendewa na tafuta kuwa na amani ya moyo. Hapo utapata furaha.
  1. Jitamkie mambo mazuri
  • Tenga muda angalau saa moja kwa wiki, tamka kwa kinywa chako mambo mazuri unayoyataka katika maisha yako. Kuna nguvu katika kukiri, jiepushe kutamka mambo mabaya.
  • Kiri ushindi na itausaidia ubongo wako kufanya yale unayoyataka kwa sababu ubongo umeumbwa kukulinda  na kukutea dhidi ya chochote kibaya kinachokuja katika maisha yako.
  1. Sikiliza muziki
  • Muziki una nguvu ya kusawazisha hisia zako na kukufanya ujisikie vizuri. Chagua muziki wenye maudhui mazuri atakufariji na kukufanya ujione ni wathamini.

  1. Lala usingizi wa kutosha
  • Mtu mzima anashauriwa kulala masaa 7 mpaka 8 kwa usiku mmoja ili kukuweka sawa.  Utakuwa na furaha kama unalala kwa masaa ya kutosha.
  1. Kumbuka Kusudi lako
  • Ukiwa na kusudi la kuishi duniani, utajuiliza ‘kwanini’ unafanya unachokifanya na itakupa nguvu ya kufurahia kutimiza wajibu.  Furaha ni zaidi ya kupata raha bali ni kuridhika na hali uliyonayo.
  1. Pitia Malengo yako
  • Andika malengo yako kwenye daftari.  Tumia muda wa kutosha kupitia lengo moja moja ili kuliwekea mikakati ya kulitekeleza kwa wakati. Mfano una lengo la kufanya mazoezi kila siku, unaweza kupanga kufanya mazoezi hayo dakika 30 kila siku jioni.
  • Ukijenga tabia ya kupitia malengo ya kila wakati itakupa nguvu ya kutafuta njia mbadara kufikia mafanikio yako na kupata furaha maishani.
  1. Watafute watu wenye mawazo chanya
  • Jitahidi kukaa na watu wenye mawazo ya maendeleo ambao watakutia moyo, kukufariji na kupenda kile unachokifanya. Watu ambao wanajari hisia zako na kukuona una thamani na wako tayari kukusaidia pale unapokwama. Jiepushe na watu ambao wanakuambia huwezi kufanikiwa kwa lolote.

  1. Ongea na Wataalamu wa Saikolojia
  •  Ikiwa bado haupati furaha baada ya kufuata hatua zote hapo juu, muone mtaalamu wa Saikolojia akusaidie. Mwambie mtaalamu jinsi unavyojisikia kama ni msongo wa mawazo utaambiwa tiba yake.

 

 

 

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *