Mapacha watano wafariki dunia, wameishi kwa masaa kumi tu!

Albano Midelo

WATOTO wote watano waliozaliwa juzi katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma wamefariki usiku wa kuamkia jana.

Watoto hao wote watano walizaliwa salama na Sophia Mgaya (28) mkazi wa Ruhuwiko mjini hapa  kwa kufanyiwa upasuaji  katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma.

Mganga mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa Songea(HOMSO) Dkt. Benedict Ngaiza, alisema kuwa watoto hao wameishi kwa masaa kumi tu na kufariki dunia kutokana na  kuzaliwa na uzito mdogo wa chini ya kilo moja.

Dkt. Ngaiza alibainisha kuwa watoto wote wanaozaliwa wakiwa na uzito mdogo wanakuwa na maisha mafupi, hata hivyo alisema hali ya mama wa watoto hao inaendelea vizuri ingawa bado amelezwa katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma akiendelea kupata matibabu..

Tukio ambalo halijawahi kutokea katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma  limetokea Mei 24 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi  huku mtoto wa kwanza akiwa na uzito wa gramu 730, wa pili 810, watatu 670, wanne 820 na watano gramu 430.

Kulingana na mganga huyo kati ya watoto hao waliozaliwa, watatu ni wa kiume na wawili ni wa kike  na kwamba huu ulikuwa ni mzao wa pili kwa mwanamke huyo.

Alieleza kuwa katika mzao wa kwanza wa mama huyo alifanikiwa kujifungua mtoto mmoja na huu wa pili  amebahatika kujifungua watoto hao watano ambao wote wamefariki dunia.

2 Comments
  • Mpango wa Mungu wetu hauna mjadala,alipangalo yeye Mwanadamu hawezi kulipinga,tunatakiwa kushukuru kwa kila jambo.

     

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *