Mlimani moto, polisi wajiandaa kudhibiti mgomo wa wanafunzi

Jamii Africa

HALI inazidi kuwa tete katika maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, baada ya wanafunzi wa chuo hicho kuamua kugoma na kuandamana wakitaka ongezeko la posho.

Habari kutoka UDSM inaeleza kwamba tokea jana hali ilikua tete ndani ya maeneo yote ya chuo hicho ikiwa ni pamoja na hosteli wanazoishi wanafunzi ambako baadhi walikua wakiwachapa viboko wenzao wanaopinga mgomo huo.

Habari zinasema tayari polisi wameshajiandaa kukabiliana na wanafunzi hao na wameshazunguka eneo lote la UDSM.

FikraPevu limeshuhudia baadhi ya wanafunzi wakiwa na fimbo ndefu Alhamisi usiku na taarifa zinasema walisema watamchapa mwanafunzi yeyote atakayeingia darasani.

“Tangu jana kulikuwa na mwendelezo wa vikao vya mgomo na maandamano ya vitivyo takribani vyote main campus, Udsm. Pia inategemewa kujumuisha wana Ardhi University wakigomea kuongezewa fedha za kujikimu (allowance) kutoka Tshs. 5,000 mpaka Tshs. 10,000 kwa siku na madai mengine.

“Tangu jioni ya jana wanafunzi wasiojiusisha na mgomo wamepigwa na haruhusiwi mtu kutoroka kwenda nje ya chuo ili kulazimika kugoma,” anaeleza mtoa habari aliyeweka taarifa katika mtandao wa www.jamiiforums.com.

Mtoa taarifa huyo ameendelea kwa kusema:

“Pia wamekataa ombi la UVCCM kuigomea Bodi ya mikopo,wamedai kuwa bodi inapokea maelekezo kutoka Serikalini, tatizo ni serikali na wanataka kuandamana kwenda ikulu! Pia wametoa madai mazito kuwa viongozi wao wa serikali ya wanafunzi wanalipwa mpaka shilingi 9,000 mpaka 10,000 kwa siku ili kuwashawishi kutopaza sauti na ili wazime migomo.

“Kwa yote haya wanafunzi hawayataki na wanaandamana,hapa mwaka wa pili na wa tatu ndo wanaonekana kuhamasisha. Jamani hali si shwari UDSM katika siku ya leo!”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *