Polisi aliyefyatua bomu lililoua mwandishi akamatwa, kushitakiwa kwa mauaji

Jamii Africa

OLISI ambaye alifyatua bomu kwa karibu na kusababisha kifo cha Mwandishi wa habari wa Channel Ten,  Daudi Mwangosi, anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote, Fikra Pevu imefahamishwa.

Taarifa za kutoka Iringa zimeeleza kwamba kushitakiwa kwa askari huyo, kunafuatia kukamilika kwa uchunguzi wa awali ambao unathibitisha pasi shaka kwamba bomu alilofyatua ndilo lililosababisha kifo cha mwandishi huyo wa habari.

Imethibitishwa kwamba kilichousambaza mwili wa mwandishi huyo ni bomu maalumu linalorushwa kwa kutumia bunduki kwa nia ya kusambaza watu waliokusanyika kwa nia ya kutenda uhalifu na lilirushwa kwa karibu mno kinyume cha masharti na kanuni za matumizi yake.

Bomu hilo hutakiwa kurushwa kutoka umbali wa mita kati ya60 na 80, wakati askari huyo alilirusha kwa karibu mno na akimlenga mwandishi Mwangosi.

Katika tukio hilo, bomu hilo liliusambaratisha mwili wa Mwangosi na kumjeruhi ofisa mmoja wa polisi ambaye anaelezwa kutaka kumsaidia mwandishi huyo ambaye alikua akipigwa na polisi wenzake.

Marehemu Mwangosi aliuawa Jumapili iliyopita katika kijijini cha Nyololo, wilayani Mufindi, mkoani Iringa katika tukio ambalo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walikuwa wakifungua tawi la chama chao, huku Polisi wakitumia nguvu kubwa kuzuia uzinduzi wa tawi hilo.

28 Comments
  • Kwa kweli inauma sana mahali tulipofikia na
    Pa hatari sana kwa usalama wa nchi na watanzania .mauaji haya watawala watayalipia siku sio nyingi Mungu hatavumilia haya tena yuko tayari kuijilia nchi hii.

  • police wameonyesha uzembe wa hali ya juu kumuuwa mwandishi wa habari, hili linawaumiza vichwa hakukua na ulazima wakumkamata yule mwandishi yy alifika kuchukua matukio. lakini kutikana na police kutumia nguvu kupitakiasi kwa wananchi waliona mwandishi ameisha warekodi hivyo wataonekana wakaamua kumlipua.

  • Wamekosea kudanganya. mbona shegela wa ccm alisema chadema ndo walimrushia bomb? Inanipa mashaka upeo wa akili ya nchimbi, mwema, tendwa, nape, na hawa mapolisi kwa ujumla.

  • Ee Mungu, tusaidie Watanzania tusijewaka hasira juu ya Askari hawa wanaoua ndugu zetu kila kukicha na kutualika kuamini kuwa CHADEMA NI WAUAJI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!. Wakati huo, hawa jamaa wanadunda mitaani kwetu tunawaangalia tu! Pamoja na yote hayo, watanzania watadumu kuwa watazamaji hata lini?

    • ipo siku polis watajua mbivu na mbichi kwan wataua wengi lakini watakaobaki hawatakubali upumbavu wao uendelee. tunaelekea huko na mazingira wanayatengeneza wenyewe

  • Ni jambo la kusikitisha mtu yoyote kupoteza maisha mikononi mwa polisi lakini pia ni kwa bahati mbaya ile tear gas can kumtoka askari, si kusudio lake kumuua yule mwandishi. ukitazama picha yote unagundua katika tukio lile kuna askari watatu wamejeruhiwa na ule mlipuko iweje kuwapiga wao kwa wao. Kibaya ni kitendo kile cha kumburuza marehemu mwangosi kabla ya kuuwawa. Yaliyofuata ilikuwa ni ajali mbaya ya mlipuko wa bomu la machozi inasikitisha sana. nafikiri na yule askari anajuta kwa kitendo kile. mkanganyiko umekuwa ni mkubwa mno hakuna aliyetegemea matokeo hayo mabaya, Si polisi wala cdm.

  • Ni wakati sasa viongozi wakuu wa nchi kulikemea tabia hii mbaya ya polisi kujichukulia sheria mikononi. Kama mwandishi alikuwa na kosa mbona tayari alikuwa mikononi mwao kwanini wasimpeleke mahakamani? Vinginevyo wananchi wana haki ya kuamini kuwa yale ni maagizo toka kwao!

  • Sio muda wa kufumbia macho haya matukio mabaya tena (Arusha, Morogoro na Iringa ss) yanayotendwa napolisi. What I know polisi hawawezi kwenda kusambaratisha maandamano yoyote yale bila ruhusa au kibali kutoka kwa wakubwa wao.Hivyo matukio haya yote yanapaswa kuchukuliwa hatua na haki itendeke, we are too tired now kwa stori za hawa viongozi wasioona wakati wanatazama!!!!!

  • tumechoka kudanganywa!!!!! hizo ni propaganda 2. ishu nzima ilisukwa na POLICCM, hakuna kitakacho fanyika zaidi ya kutulaghai. hebu tafakari polisi kutolewa nje ya mkoa tena kwa siri!!!! Huo ulikuwa mpango wa kuinufaisha CCM lkn MUNGU kawaumbua. POLICCM endelea kutimiza wajibu wenu wa kukipendelea chama tawala. ueni, umizeni, teseni, pigeni, wengine pelekeni mistuni mkawang’oe meno kwa praiz lakini mjue yule mtanzania atakaye salia ataendelea kudai haki zake.

    • tusipokuwa makini watanzania hakuna hatua yoyote itakayochukuliwa na magamba dhidi ya muuaji….na pengine kama kweli alitumwa kuua basi akifikwa na maji ya shingo huenda akasema ukweli huyo police au wakamuua na yy ili kupoteza ushahidi…. let us be vey keen…!

  • Adam Nindi –Songea

    Hospitali ya Songea ambayo nitegemeo kwa wakaazi wa Mkoa wa Ruvuma ina kabiliwa na Changamoto ya Kukosa ma shine ya Exray kwa kipindi cha mwezi mmoja hivi sasa.

    Hayo yamebainika baada ya watu 17 kupata ajali na kushindwa kupata huduma ya upimaji katika hospitari ya mkoa wa Ruvuma kutokana na mashine ya Exray kuwa mbovu na kusababisha majeruhi kupelekwa hospitali ya Peramiho songea vijijini kilometa 24 kutoka songea mjini ili kwenda kupata huduma Exray

    Kaimu Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Songea Mathew Chanangula amesma katika ajali hiyo iliyo tokea katika eneo la Mlima Mkwaya songea vijijini kati ya watu 17 walio pata ajali hiyo mototo mwenye umri wa miaka 2 Daima Rashidi alifariki dunia baada ya kupoteza damu nyingi

    Kaimu Mganga Mfawidhi Mathew Chanangula akieleza wagonjwa walio kimbizwa katika Hospitali ya Peramiho na sabababu zilizo mfanya kuidhinisha kwenda kutibiwa huko amesema ni kutokana wengi kuvunjika mikono miguu na Majeraha makubwa ambayo yalihitaji vipimo vya Exray

    Wagonjwa walio nusurika katika ajali iliyo tokea barabara Mkenda Songea Maeneo ya Mlima Mkwaya wamesema ajali hiyo ilitokana na mwendo wa Kasi na Gari aina ya Center Ilikosa Breki na Dereva baada ya kuona hana Breki alilazimika kuigonga Rand rover iliyo kuwa mbele yake na kuongeza ajali nyingine.

    Wananchi wengi walio ongea na mwandishi huyu wamesema barabara ya Songea Mkenda kuelekea mpakani msumbiji magari mengi yanayo tumika ni Marori. Hata hivyo Roli hizo ni mbovu hakuna gari lenye uhakika linalo elekea mpakani

  • lakini mwanzoni mwa mkasa huu polisi walisema eti wafuasi wa chadema ndio waliorusha kitu kinachosemekana kuwa bomu baada ya ushahidi wa picha za waandishi wa habari, polisi wameonekana kwamba walikuwa wanaudanganya umma wa watanzania wakiongozwa na RPC wa iringa ashukuriwe mungu kwamba waandishi wa habari JASIRI waliendelea kuchukua matukio ya kinyama waliyofanya hawa askari dhidi ya marehemu DAUD MWANGOSI, wakiongozwa na RPC Kamhanda, inashangaza kuona mpaka sasa huyu RPC hajaachia ngazi sijui nani anamlinda na kwa faida gani, POLISI wanatakiwa watambue kwamba sisi ndfio waajiri wao wakuu wanaishi kwa kutegemea KODI zetu inatia kichefuchefu kuona kwamba Jeshi la polisi linaendeleza tabia CHAFU ya kuua RAIA wasio na hatia je hivi wao wanadhani hoa wanao watumia vibaya watakapo kaa pembeni hali itakuwaje kwa upande wao? HII NI NCHI YETU SOTE WASIJIGEUZE MIUNGU WATU WAKATI KODI ZETU NDIO ZINAENDESHA MAISHA YAO.

  • Mwanadamu amemtawala mwanadamu mwezake kwa Hasara
    Hakuna Serikali itakayofanya vizuri katika dunia yetu

  • Polisi wawe waangalifu kwa raia kwani huyu alikuwa kazini ila kwa dhambi ya kuwanyanyasa raia bila kujua adhabu ya mungu inakuja amejikuta akienda kizimbani peke yake…

    Najiuliza asingekuwa Mwangosi akawa ni raia kama wa Morogoro unadhani angekamatwa na mtu yoyote au kuandikwa na vyombo vya habari mara nyingi hivi?

  • chochote kinacho zaliwa lazima kife no matter its a human being or political party as long as kimepitia hatua ya kuzaliwa lazima kitakufa je tunakaa upande upi na decisions zetu zipo fair baada ya walio zaliwa tutakapokufa kumaintain au tupo tayati kuwa charged nao its a matte
    r of generations to determine it

  • Miezi yazidi kukatika tu! Kesi iko wapi? Au upelelezi haujakamika?!? Kweli watz tu maboya! Tunataka afe nani ndo tuchukue hatua? Mitandao Kama hii ndo ilikuwa ndo pakuchangia mawazo juu hatua gani tuwachukulie hawa wajiitao mapolisi pamoja na serikali iliyopo madarakani kwa ujumla wake. Badala yake…..!!!!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *