Sababu 3  kwanini zaidi ya 50% ya ajali za barabarani hutokea karibu na makazi ya watu

Jamii Africa

Mwendo kasi inatajwa kuwa sababu kubwa inayosababisha ajali za barabarani, huku madereva wakilaumiwa kwa kuendesha magari wakiwa wamelewa. Lakini kwanini ajali nyingi hutokea maeneo wanayoishi watu?

Kulingana na uchunguzi uliofanywa na Jalida la Huffngton Post nchini Afrika Kusini umebaini kuwa zaidi ya asilimia 50 ya ajali za barabarani hutokea karibu na maeneo wanayoishi watu hasa wakati wa usiku ambapo madereva hurejea nyumbani. Hizi hapa sababu nne zinazosababisha ajali hizo katika makazi ya watu:

1.         Ulevi
Inaelezwa kuwa kuna matumizi makubwa ya pombe maeneo ambayo watu wanaishi hasa mwishoni mwa juma. Maeneo ambayo watu wanakunywa pombe zikiwemo baa na klabu za usiku yako karibu na makazi ya watu ambapo walevi wanafikiri wakimaliza kunywa ni rahisi kuendesha gari na kurudi nyumbani kupumzika.

Dereva au mtembea kwa miguu akinywa pombe kupita kiasi umakini unapungua na ni rahisi kufanya maamuzi magumu ambayo yanaweza kugharimu uhai wake na wa yule anayetembea kwa miguu.

Inashauriwa ikiwa umeenda kunywa pombe, usiendeshe gari ni vema ukakodisha mtu wa kukuendesha au kuwa na mtu ambaye hatumii vileo.

 

2.         Umakini wa madereva hupungua
Imefahamika kuwa umakini wa madereva hupungua ikiwa wanaendesha magari kwenye maeneo wanayoyafahamu. Katika maeneo hayo kuna shughuli mbalimbali za watembea kwa miguu na hatari zingine ikiwemo makutano ya barabara na taa za kuongoza magari.
 

Pia madereva hupumbazwa na matumizi ya simu ikiwemo kutuma ujumbe mfupi na maongezi. Usalama wa dereva na gari lako unatimia ikiwa amewasili nyumbani lakini ukiwa barabarani unatakiwa kuwa makini na kujiepusha na vitendo vyote vinavyoweza kukusababishia ajali.

 

3.         Mwendo Kasi
Sababu nyingine inayochangia ajali za barabarani ni mwendo kasi. Licha ya askari wa barabarani kusimamia sheria na kutumia tochi ili kuwabaini madereva wanaoendesha kwa mwendo kasi bado lakini hawawezi kuwafikia wote hasa katika makazi ya watu ambako hawawezi kufika. 

Jambo la muhimu kwa dereva ni kujitambua yuko katika mazingira gani, kama ni kwenye makazi ya watu endesha polepole mwendo usiozidi kilomita 40 kwa saa (40km/h) ili kuwalinda watembea kwa miguu kwasababu mwendo kasi ni hatari unaweza kuleta majuto makubwa kama tahadhari haitachukuliwa mapema.

Wote tuna wajibu wa kulinda uhai wa binadamu, tuchukue tahadhari wakati tunaendesha magari katika makazi ya watu ambako ndiko kuna mazingira hatarishi yanayoweza kusababisha ajali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *