Serengeti Boys yafanikiwa kucheza Fainali za Afrika. Waziri Nape, Malinzi wapongeza

Jamii Africa

TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Vijana umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) imefuzu kucheza Fainali za Afrika.

Habari zilizoifikia FikraPevu toka jijini Libreville ambapo Kamati Tendaji ya Shirikisho la mpira barani Afrika (CAF), imeipa ushindi Tanzania dhidi ya timu ya vijana ya Jamhuri ya Congo.

Mara ya mwisho Tanzania kufaulu fainali za Afrika kwa wanaume ni mwaka 1980.

"Tunashukuru kuwa vijana wetu wametinga katika fainali za Afrika, hii ni heshima kubwa kwa Tanzania" amenukuliwa Jamal Malinzi, Rais wa TFF. 

"Jamani, hawa vijana wametuondolea aibu ya kuwa bichwa la mwenda wazimu. Watanzania kwa pamoja tuwapongeze Waziri Nape, Jamal Malinzi na TFF kwa mafanikio ya Programu yao, " alisema Ali Mchumila, mchezaji wa zamani wa Klabu ya Yanga. 

Naye Aboubakari Ali, ambaye ni kiungo wa zamani wa RTC Mara amesema ni muhimu sana kucheza fainali bila kujali matokeo. 

Jamal Malinzi amesema ili kuiandaa timu hiyo vizuri kucheza fainali mwezi Aprili, inahitajika raslimali fedha ya kutosha.

Amesema ana imani watanzania walioifikisha Serengeti Boys hapo, wanaendelea kuiunga mkono katika fainali hizi za Afrika kwa hali ya mali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *