Ugonjwa wa Mafua ya Ndege waikumba Madagascar, Tanzania hatarini kuupata

Jamii Africa

Nchi tisa za Afrika ziko katika hatari ya  kukumbwa na ugonjwa wa mafua ya ndege, na tahadhari imetakiwa kuchukuliwa dhidi ya ugonjwa huo ambao unaenezwa kwa njia ya hewa.

Tahadhari hiyo imetolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ikiwa ni siku chache baada ya kuripotiwa kwa watu zaidi ya 1,300 kuwa na ugonjwa huo nchini Madagascar ambapo juhudi za mashirika ya Afya kudhibiti ugonjwa huo bado zinaendelea.

Ugonjwa huo ambao hushambulia mapafu na kumsababishia mgonjwa kupumua kwa taabu huenea kwa kasi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Repoti ya WHO inaonyesha kuwa robo tatu ya watu nchini Madagascar ambao wanadhaniwa kushambuliwa na ugonjwa huo wako katika hali mbaya.

Inaelezwa kuwa ugonjwa huo unasababishwa na bacteria aina ya vian ambaye hushambulia mapafu na asipotibiwa mapema huweza kufa ndani ya saa 72. Ugonjwa huo ni miongoni mwa magonjwa yanayosambaa kwa kasi na kuathiri sehemu kubwa ya dunia kwa wakati mmoja.

Taarifa za jarida la MailOnline linaripoti kuwa ugonjwa uliua watu milioni 50 katika nchi za Ulaya mnamo mwaka wa 1300. Linaeleza kuwa ugonjwa huo ambao unasambaa kwa kasi huku nchi za Afrika  ambazo zinatembelewa sana na watalii wa fukwe ziko katika hatari ya kupata ugonjwa huo zikiwemo Afrika Kusini, Seychelles na kisiwa cha Reunion.

Nchi nyingine sita ni Msumbiji, Tanzania, Kenya, Ethiopia, Commoro na Mauritania ambazo zinapaswa kuchukua tahadhari kutokana na kuwa na mafungamano ya karibu na Madagascar katika nyanja za usafiri na biashara.

Hata hivyo, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee ilitoa tamko Oktoba mwaka huu ambapo iliwatoa hofu wananchi na kusema kwamba imedhibiti viashiria vyote vya kusambaa kwa ugonjwa huo nchini.

Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Faustin Ndungulile alipoulizwa katika mtandao wa Twitter juu ya ugonjwa huo ambao umeikumba Madagascar  na unatishia kuenea katika maeneo mengine ya Afrika amesema wizara yake ina taarifa na inalifuatilia kwa karibu suala hilo na wanachukua tahadhari  kuwalinda wananchi na tishio hilo.

“Tuna taarifa na tumechukua tahadhari. Tamko kwa umma kuhusiana na ugonjwa huu lilitolewa na Wizara tarehe 02/10/2017” ameeleza Naibu Waziri.

Ikumbukwe siku ya jana, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) iliteteketeza vifaranga 6,400 vya kuku ambavyo viliingizwa nchini kinyume na Sheria na kukumatwa katika mpaka wa Namanga mkoani Arusha.

Hatua hiyo ilitajwa na Maafisa wa TFDA kuwa ni kujihami dhidi ya magonjwa ikiwamo ugonjwa mafua ya ndege ambao unaenezwa na wanyama jamii ya ndege.

Kulingana na Tawi la Afrika la WHO linaeleza kuwa watu 93 wamefariki kutokana na ugonjwa huo mpaka sasa nchini Madagascar na kama hatua stahiki za kuudhibiti hazitachukuliwa utasambaa katika miji mingine, ambapo miji ya Antananarivo na Toamasina ndio yameathirika sana.

Kila mwaka kesi 600 za ugonjwa huo zinaripotiwa katika nchi hiyo, lakini mwaka huu hauwezi kusambaa sana kwasababu umegundulika mapema.

Wataalam wa Afya wakikusanya mabaki ya ndege waliokufa kwa ugonjwa wa mafua ya ndege

 

Vihatarishi vya ugonjwa wa mafua ya ndege

Kadiri jinsi virusi wa mafua ya ndege wanavyosambaa ndivyo uwezekano wa kutokea kwa milipuko ya ugonjwa huu inayoathiri binadamu sehemu mbalimbali duniani unavyokuwa mkubwa. Tafiti zinaonesha kuwepo kwa hatari ya kutokea kwa mlipuko mkubwa ( pandemic) unaoweza kusababishwa na kusambaa kwa virusi hawa duniani.

Watu walio katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa wa mafua ya ndege
• Wakulima na wale wanaojishughulisha na ufugaji wa jamii mbalimbali za ndege
• Wasafiri wanaotembelea maeneo yaliyokumbwa na mlipuko
• Yeyote anayegusa ndege aliyeathirika na mafua ya ndege
• Mtu anayekula nyama ya ndege aliyeambukizwa virusi wa avian influenza ikiwa mbichi au isiyoiva vizuri au kula mayai au damu za ndege wenye virusi hao

• Aidha, watoa huduma za afya pamoja na ndugu za wagonjwa wenye ugonjwa huu nao pia wapo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya mafua ya ndege.

Imeonekana kuwa virusi wa avian flu virus (H5N1) wana uwezo mkubwa wa kuishi katika mazingira kwa muda mrefu bila kuathirika. Katika hali hii, maambukizi yanaweza pia kusababishwa na mtu kugusa maeneo walipo virusi hawa. Ndege walioambukizwa ugonjwa huu huendelea kutoa virusi kupitia katika vinyesi vyao au mate yao kwa muda wa mpaka siku kumi tangu waambukizwe.

Dalili za mafua ya ndege
Dalili za mafua ya ndege kwa binadamu hutegemeana na aina ya virusi waliomshambulia muhusika. Dalili pia zinaweza kuanza kujitokeza siku saba mpaka kumi tangu mtu anapopatwa na maambukizi ya virusi wa H5N1. Mgonjwa huwa na dalili zote za mafua makali kama vile:


• kukohoa (kikohozi kikavu au wakati mwingine kinachotoa makohozi)
• kuharisha
• kutapika
• kichefuchefu
• kupumua kwa shida
• homa zaidi ya nyuzi joto 38
• kuumwa na kichwa,
• kujihisi uchovu wa mwili,
• maumivu ya misuli ya mwili mzima,
• kutokwa na makamasi mepesi yanayotiririka bila ukomo na kuwashwa na koo.

Matibabu

iwapo utajihisi kuwa na dalili za mafua ya ndege (kama zilivyotajwa hapo juu) ndani ya siku kumi baada ya kushika ndege au mazao ya ndege wanaohisiwa kuwa na virusi vya H5N1 au iwapo ulisafiri kwenda eneo lenye mlipuko wa mafua ya ndege ni vema kwenda hospitali.

Epuka kunywa dawa za kuua virusi wa mafua ya ndege bila kupata ushauri wa daktari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *