Je, unapenda kuishi maisha marefu zaidi na kuendelea kufurahia uhai na raha za dunia hii? Basi jibu lake ni dogo tu; “kodolea matiti ya wasichana wadogo.”
Jibu hili ni matokeo ya utafiti wa kisayansi uliofanywa na wanasayansi mabingwa wa kutafiti ongezeko la umri wa kuishi kwa wanaume.
Daktari bingwa na mtaalamu asiyepingika duniani aliyefanya utafiti wake kwa wanaume wa Ujerumani kwa muda wa miaka mitano, Karen Weatherby, anaeleza kuwa wanaume wanaokodelea matiti, hasa yaliyosimama na ‘kuumbika vizuri’, wanaongeza muda wao wa kuishi.
Anasema, "wanaume wanaofanya hivi, huongeza miaka minne au hata mitano ya kuishi, ikilinganishwa na wale wasiopenda kukodolea macho matiti (wengine wakiyaita maziwa ya mabinti).
Dk. Karen anasema muda mzuri unaoweza kumuhakikishia mwanaume ongezeko la umri, ni kutumia zaidi ya dakika saba mpaka 10 akitazama matiti hayo.
"Kutazama matiti ni hatua kubwa ya kuongeza muda wa kuishi kwa wanaume na ni sawa na kufanya mazoezi ya nguvu, yanayochoma mafuta kwa muda wa nusu saa," anaongeza daktari huyo bingwa.
Matokeo ya utafiti huo wa Dk. Karen yamechapishwa na gazeti linaloheshimika duniani kwa afya za wanaume; Men Health linalochapwa Uingereza na Marekani. Toleo lake la January, mwaka huu limebeba Makala hiyo ya utafiti. Gazeti jingine lililochapisha matokeo haya ya utafiti ni New England Journal of Medicine, la Uingereza.
Akiungwa mkono na madaktari wenzake kutoka vyuo mbalimbali vya tiba duniani, Dk. Karen anaeleza kuwa "zoezi la kukodolea matiti linaepusha pia magonjwa mengi yasiyokuwa ya kuambukiza, yanayowapata wanaume zaidi kuliko wanawake."
Dk. Karen anayataja magonjwa hayo kuwa ni pamoja na shinikizo la damu, kisukari, magonjwa ya akili na msongo wa mawazo.
Taarifa zinaeleza kuwa utafiti huo ulifanyika kwa wanaume 200 waliojitolea kufanya zoezi hilo mara kwa mara, huku wakifuatiliwa na watafiri, ambao hatimaye walithibitisha kuwa kuna ukweli katika matokeo ya utafiti huo.
Dk. Masumbuko Kilenge wa Tabata, Dar es Salaam alipoulizwa ukweli wa matokeo ya utafiti huu na kama anaweza kueleza kwa lugha nyepesi, nini kinasababisha ongezeko hilo la umri mwanaume anapotazama matiti, alisema hana uhakika.
“Sina uhakika na wala sijawahi kusoma popote, lakini kwa kuwa ni matokeo ya utafiti wa kisayansi, inawezekana kabisa kuwepo kwa ongezeko hilo linaloelezwa,” alisema na kuomba muda akajisomee, labda anaweza kuwa na ushauri zaidi kwa wanaume.
Katika Tanzania, kwa mujibu wa takwimu za mwaka jana zilizotolewa na taasisi ya kimataifa ya kufuatilia uzazi, vifo na maisha ya binadamu, wastani wa maisha kwa mwanaume wa Tanzania ni miaka 60 wakati wanawake ni miaka 64.
Kama ni kweli matokeo ya utafiti huo, basi wastani wa umri wa wanaume wanaokodolea matiti unaweza kufikia miaka 65 na kuwapiku wanawake.
Magazeti makubwa ya Ulaya, Amerika na Asia yameuchapisha utafiti huo na kueleza kuwa ni mafanikio makubwa katika jitihada za kurefusha umri wa wanaume kuishi. Miongoni mwa magazeti hayo ni pamoja na New York Post, Sunday Times, Washington Post na New Delhi Times.