Utunzaji nyaraka za serikali katika kijiji cha Magalata

Kulwa Magwa

NYARAKA mbalimbali za serikali na kumbukumbu za ofisi ya kijiji cha Magalata, kilichoko katika wilaya ya Kishapu, ziko hatarini kuharibika na kulowana na maji iwapo mvua zitanyesha.

Sambamba na kuharibika kwa nyaraka hizo, iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa huenda zikatoweka kutokana na utunzaji wake kutokuwa mzuri.

Nilishuhudia utunzaji wa nyaraka hizo usiokuwa mzuri baada ya kuingia katika ofisi hizo, hivi karibuni, ambapo alijionea zikiwa zimerundikwa kwenye boksi lililojaa vumbi huku likiwa chini.

nyaraka-serikali

Pia alishuhudia nyaraka hizo, zikiwemo stakabadhi za malipo ya fedha zikiwa zimewekwa bila kufuata utaratibu wa utunzaji unaoambatana na kuwekwa kwa kufuata tarehe na kutunzwa kwenye mafaili husika.

Kutokana na kujaa vumbi kwa kumbukumbu hizo, baadhi ya nyaraka ni vigumu kuzisoma bila kuzikung’uta na nyingi nyinginezo zimeanza kuchakaa kwa kutosomeka vizuri.

Aidha, kutokana na ofisi ya kijiji hicho ‘ilivyochoka’ huku paa lake likiwa na matundu kibao, iwapo mvua zitaanza kunyesha kuna hatari nyaraka hizo kulowana na maji.

Akizungumzia utunzaji wa nyaraka hizo, Mwenyekiti wa kijiji hicho, Bulugu Mipawa, alisema kwa sasa hawana njia nyingine ya kuzitunza, isipokuwa watakuwa na utaratibu maalumu baada ya kukamilisha ujenzi wa ofisi unaokusudiwa kuanza baada ya kumalizika kwa msimu wa mvua.

wajumbe

Mwenyekiti wa kijiji cha Magalata, Bulugu Mipawa (kushoto) akiwa na Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Jiyenze Ng'wandu (katikati) na mjumbe wa serikali ya kijiji, Gilagida Kachemba

“Tunataka kuanza kujenga ofisi ya kijiji chetu mvua zitakapomalizika kunyesha, ila kwa sasa hatua jinsi – lakini nikuhakikishie kwamba hazitalowana, “alisema Mipawa.

Mwenyekiti huyo alisema iwapo mvua zitakuwa kubwa, nyaraka hizo wataziweka juu ya meza wakati wakiendelea kusubiri muda wa ujenzi wa ofisi utakapofika, na kwamba hawana mpango wowote wa kuzihamishia sehemu nyingine ila zitabaki ofisini hapo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *