Wageni wanaoingia nchini kupimwa homa ya manjano

Jamii Africa

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema inaendelea kupima na kutoa chanzo ya ugonjwa wa homa ya manjano kwa wasafiri wanaoingia nchini ili kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo  kwa wananchi.

Katika taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Mpoki Ulisubisya imeeleza kuwa Tanzania haiko katika nchi  za Afrika zenye tishio la kukumbwa na ugonjwa wa homa ya manjano lakini tahadhari ni muhimu kwasababu nchi jirani zinazotuzunguka zinakabiliwa na ugonjwa huo.

“Hata hivyo, upatikanaji wa mdudu wa homa ya manjano na mazingira ya uzalianaji yanatuweka katika hatari ya kupata ugonjwa wa homa ya manjano ikiwa virusi vitaingia nchini. Ikiwa tumezungukwa na nchi zenye ugonjwa huo inaongeza uwezekano wa Tanzania kuathirika na virusi hivyo,” ameeleza sehemu ya ripoti hiyo.

Kutokana na hatari hiyo, wasafiri kutoka katika nchi zenye maambukizi ya ugonjwa huo wanalazimika kupima na kupata chanzo kabla ya kuruhusiwa kuingia nchini, isipokuwa wale wenye vyeti vinavyosibitisha kuwa hawana maambukizi ya homa ya manjano.

“Chanzo ya homa ya manjano ni lazima kwa wasafiri wanaotoka  nchi zilizo na hatari ya kusambaza ugonjwa huo. Hii pia inahusisha wasafiri wanaosafiri na ndege za masafa marefu ambao wanapita katika nchi hizo kwa saa 12 au zaidi,” imeeleza taarifa hiyo.

Ugonjwa wa homa ya manjano ni hatari sana na umewekwa chini ya uangalizi wa kimataifa. Kulingana na Kanuni za Kimataifa cha Afya (IHR) za mwaka 2005 zinauchukulia ugonjwa huo kama ni dharura ya kimataifa  ili kuhakikisha hauthiri idadi kubwa ya watu duniani.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeiweka Tanzania kwenye ramani ya nchi ambazo haziko kwenye hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo lakini imetoa tahadhari ili kujikinga na maambukizi mapya ambayo yanaweza kuingia  kutoka nchi zenye virusi vya homa ya manjano.

Nchi  za Afrika zilizo kwenye hatari kubwa ya kusambaza virusi vya homa ya manjano ni Angola, Benin, Burkina Faso, Burundi,  Jamhuri ya Afrika ya Kati, Congo, Ivory Coast, Chad, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Equatorial Guinea, Gabon, Ethiopia na Ghana.

Nchi zingine ni Gambia, Guinea, Guinea Bissau, Kenya, Liberia, Mali, Mauritania, Niger, Nigeria, Rwanda, Senegal, Sierra Leone, Sudan Kusini, Uganda na Togo.

Lakini nchi zilizo nje ya bara la Afrika kama Argentina, Bolivia, Brazil, Colombia, Ecuadol, Guyana, Panama, Peru, Suriname, Trinidad na Tobago na Venezuela, nazo zitahusika katika chanzo ya homa ya manjano.

Hata hivyo, watanzania wanaosafiri kwenda katika nchi zilizotajwa hapo juu, watatakiwa kupata chanzo ya homa ya manjano siku 10 kabla ya kusafiri ili kujikinga na virusi baada ya kurejea nchini.

“Kwa watanzania wanaosafiri kwenda nchi zenye hatari ya kusambaza homa ya manjano wanatakiwa kupata chanjo siku 10 kabla ya kusafiri,” imeeleza ripoti hiyo.

 

Ugonjwa wa homa ya manjano ni nini?

Ugonjwa huo unaenezwa na mbu aina ya aedes wenye virusi vya viitwavyo  “ Hepatitis  B “ (  HBV) ambavyo hushambulia zaidi ini la mwanadamu.  Virusi hivi visipotibiwa hutengeneza uvimbe kwenye ini na kusababisha saratani ya ini ambayo husababisha kifo.

 Homa ya manjano ni tatizo linaosababisha ngozi yako, midomo na sehemu nyeupe ya jicho kuwa ya njano kutokana na kuongezeka kwa rangi ya bilirubini katika damu inayotengenezwa kwenye ini baada ya kuvunjwa kwa seli nyekundu za damu.

Hali hii inaweza kuambatana na kinyesi cheye rangi ya udongo mfinyanzi au kutoa mkojo mweusi, mwili kuwasha, kutapika kukosa hamu ya kula na uchovu.

Ugonjwa  wa  manjano  hauna  tiba  isipokuwa  mgonjwa   akiwahi  hospitali  atapatiwa dawaza  kupambana  na  virusi  kuvipunguza  nguvu  za  kupambana  na  ini., kupandikizwa  ini  ambapo ini lililoathirika huondolewa na kuwekwa jingine japokuwa ni vigumu kupata ini salama.

Ukigundua kuwa umeambukizwa ugonjwa huu unashauriwa kuacha kutumia pombe, dawa za kulevya, na vitu vingine vinavyoathiri utendaji wa ini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *