Watano mbaroni Dar wakihusishwa na mauaji ya RPC Barlow

Jamii Africa
damu-barlow

KIKOSI maalumu cha vyombo vya usalama chini ya Jeshi la Polisi, kimewatia mbaroni jijini Dar es Salaam watuhumiwa watano muhimu wa mauaji ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow

Habari za uhakika kutoka vyanzo vyetu vya ndani zimethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao muhimu ambao wanatarajiwa kuhojiwa na kusafirishwa kwenda Mwanza kushitakiwa.

 

damu-barlow

Gari aina ya HILUX (T 777 BFY) linalodaiwa hayati RPC Liberatus Lyimo Barlow wa Mwanza, alikuwa akiendesha siku mauti yake yalipomkuta kwa kuuawa papo hapo kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni MAJAMBAZI Kitangiri Jijini Mwanza Tar 13/Oktoba/2012.

Gari hilo linalodaiwa kuwa ni mali ya RPC Barlow likiwa limeegeshwa katika moja ya vituo vya Idara ya USALAMA jijini Mwanza!

Habari hii inaendelea kuhaririwa kadiri taarifa zitakavyokuja…

6 Comments
  • The death of our commander Liberatus Barlow has let a big gap in the security of Mwanza city. He was a man who was really committed to his work!!!! Personnally during his ,lats day he did assist me in recovering my money that was stollen!!!

  • wakati fulani najiuliza wauaji kama hao inapobainika kuwa wana hatia na mahakama kuwahukumu kifo kisha adhabu kutekelezwa, taasis mbalimbali za haki za binadamu huja juu zikidai kuvunjwa kwa haki za binadamu; HIVI YUPI ANAPASWA KUTETEWA, muaji au aliyeuawa (wahanga)?

  • Kwanza kabisa napenda niwapongeze jeshi la polis na jopo la usalama kwa kazi yao nzuri ktk kufanikisha zoezi zima la kuwapata hawa waalifu wa mauaji ya kamanda,
    Jambo hili ni jema sana kwa hari ambayo inchi yetu imefikia,majanga mengi yanazidi kuchafua sura ya taifa letu
    ……….Angalizo….Isiishie kuwakamata tu hao waalifu lakini tunataka kuona pia hatua kali na adhabu dhidi yao zinachukuliwa ili iwe fundisho kwa wengine zisiwe tu porojo za mdomoni.

  • Pongezi kwa kazi yenu nzuri polisi.Mwisho wake tuone pia haki ikitendeka juu ya watuhumia kwani dawa ya moto ni moto rather than remaining as Laissez faire.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *