CTI kukodisha Dowans; Kuiuzia Tanesco umeme?

Mwanakijiji

Habari za kuaminika toka ndani kabisa (ka nzi) zinataarifu kuwa Shirikisho la Viwanda Tanzania linampango wa kuwashaa mitambo ya Dowans baada ya kukodi mitambo hiyo toka kwa wamiliki. 

Mpango huu ambao bado unapingwa na Tanesco unaelekea kufikia hatua za mwisho baada ya vikao kufanyika leo ambapo shinikizo kama lililokuwepo wakati wa kuingia Richmond linaongezeka hatimaye Tanesco wakubali kuingia mkataba na CTI – Confederation of Tanzania Industries.

Kwa mujibu wa chanzo hicho CTI ambayo imekuwa kwenye ukasi haijaeleweka imepata wapi fedha za kukodisha mitambo hiyo na kwanini kusita kwa Tanesco kuingia kwenye mkataba mwingine hakuchukuliwa maanani. Shirika la Tanesco linadai kuwa hali ya dharura nchini imeanza kutengemaa taratibu na ya kuwa tayari IPTL na hata Kidatu wameanza kuzalisha umeme zaidi na kufidia pengo.

Mpango wa kuizungusha mitambo ya Dowans kwa mtu mwingine bado inawaletea tatizo watu wengi wenye kufuatilia tatizo la nishati nchini kwani inaonekana serikali haina uwezo wa kufikiria wala kutafuta njia nyingine isipokuwa Dowans kampuni ambayo imehusika na kashfa ya ulaghai ilipoingia nchini na kujipatia mkataba wa kampuni hewa ya Richmond. Kampuni hiyo ya Dowans imekuja kugundulika baadaye kuwa imekuwa ikitoa taarifa za ulaghai ili kuweza kujipatia mikataba mbalimbali lakini ni katika suala la Tanesco ndipo mkataba wake umejikuta na matatizo mengi.

Wakati huo huo taarifa nyingine zinataarifu kuwa Jeshi la Polisi Jijini Dar-es-Salaam limesitisha maandamano ya vijana wa CCM ambayo yalikuwa yamekusudia kufanyika kuunga mkono hutuba ya Rais Kikwete.

5 Comments
  • Did you know…
    Hydrogen is an energy carrier, not an energy source, meaning that it stores and delivers energy in a usable form.

    Jamani tuna makaa ya mawe, tuna natural gas (Songo Songo)! It is a shame for Tanzania to talk about short of Energy. What is need is long term statergic plan with respect to our natinal resources we have.
    Nimechoka kusikia kukodisha….

  • Wakati dunia inaondokana na energy sources zinazo poduce CO2 sisi ndo tunahangaika na kununua mitambo inayotumia fossils fuel kugenerate electricity, hivi maendeleo yetu kwanini yako kinyume nyume?

  • Dowans/Richmond ni 2015 plan, iliyopangwa from 2005. Ni lazima ipite, inwezekana watu walichanjiana damu!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *