Botswana imemuomba Rais wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC),Joseph Kabila kuachia madaraka haraka ili kuepusha kumwaga damu ya wananchi wasio na hatia.
Serikali ya Botswana imeongeza shinikizo la kumtaka Rais Kabila aachie ngazi ili kuheshimu Katiba na zaidi sana, kukubaliana na matakwa ya wananchi wengi. Taarifa ya serikali hiyo imeeleza kuwepo kwa kila dalili kuwa Congo itatumbukia katika machafuko na vita vitakavyosababisha vifo vya raia wasiokuwa na hatia.
Rais Joseph Kabila akiwa na baadhi ya viongozi wa Congo DRC
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Ushirikiano imeeleza kuwa, “Botswana inaitaka jumuiya za kimataifa kuongeza shinikizo kwa utawala wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo na kuruhusu demokrasia kuchukua mkondo wake”.
Kabila alichukua urais mwaka 2001 baada ya mauaji ya baba yake na alitarajiwa kuachia madaraka mwaka 2016 baada ya kipindi cha miaka miwili ya uongozi kuisha. Hata hivyo, amekuwa akitoa changamoto mbalimbali ambazo zimezuia Shirika la Uchaguzi kufanya uchaguzi wa Rais mwingine
Tarehe mpya ya Desemba 23, 2018 imewekwa kwa ajili ya Uchaguzi lakini wafuasi wa upinzani wanataka Kabila kutangaza kuwa hatatafuta kubadili Katiba ya nchi ili kumfanya aendelee kukaa madarakani.