Kila mtu anafahamu jinsi ilivyo ngumu kujifunza lugha ya pili hasa unapokuwa mtu mzima. Katika utafiti mpya, wanasayansi wamebainisha kuwa kuna umri ambao mwanadamu akifika itampa shida kujifunza lugha mpya au ya pili (second language)
Utafiti huo uliochapishwa kwenye Jalida la Cognition, umebaini kuwa kuna uwezekano mdogo wa watu wanaojifunza lugha ya pili au mpya kuongea kama wazawa wa lugha hiyo ikiwa wataanza kujifunza baada ya umri wa miaka 10. Lakini haimaanishi kuwa haiwezekani kwasababu stadi za lugha zinaeleweka zaidi kwa watoto wenye umri mdogo.
“Inabadilika kwamba bado hutajifunza haraka”, alisema Mtafiti Prof. Joshua Hartshorne, ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo cha Boston, Marekani. “Ni kwamba unakuwa nyuma ya wakati, kwasababu uwezo wako wa kujifunza unaanza kupungua ukiwa na umri wa miaka 17 au 18.”
Wanaoanza kujifunza miaka michache baada ya umri wa miaka 10 wataweza kuzungumza na kuandika lugha ya pili, lakini siyo kama ilivyo kwa wazawa wa lugha husika.
Hata hivyo, Prof. Hartshorne amesema bado hajathibitishwa kwanini kujifunza lugha mpya kunapungua mtu anapokaribia kuwa mtu mzima. Maelezo sahihi yanaweza kujumisha mabadiliko ya mnyumbuko wa ubongo, mtindo wa maisha ambao unahusiana na kazi au chuo au hata kutokuwa tayari kujifunza vitu vipya. Lakini pia mtu anapokuwa mtu mzima kwa sehemu huogopa kujiona mjinga katika mchakato wa kujifunza.
Japokuwa inaweza kuonekana kama itawakatisha tamaa baadhi ya watu- umri miaka 10 ni mbali zaidi kwa watu ambao wana matarajio ya kujifunza lugha mpya. Pia iliwashangaza wanasayansi ambapo walifikiri kipindi cha kujifunza lugha kinaweza kuwa kirefu kuliko walivyotarajia.
Baadhi ya wanasayansi wanaamini kuwa dirisha la kujifunza lugha linafunga muda mfupi baada ya mtu kuzaliwa, lakini wengine wanasisitiza kuwa hutokea wakati wa kubarehe. Ukilinganisha na makadirio ya umri wa miaka 17 au 18 ambapo uwezo wa kujifunza lugha mpya huanza kupungua inaweza kuwa ni kweli lakini siyo kwa asilimia 100.
Utafiti huo ulitumia njia maalum kupata matokeo hayo. Kukusanya kundi la kubwa na lenye mtawanyiko wa watu unahitaji kupata mafunzo ya lugha, lakini watafiti hao walitengeneza jaribio la misamiati rafiki ambayo yaliweza kuwaletea matokeo chanya.
Jaribio hilo lilikuwa la dakika 10 likiitwa “Kiingereza Kipi?” ambapo washiriki walitakiwa kukisia lugha zao za asili, lahaja na nchi za nyumbani kwa kutumia maswali ya misamiati ya kiingereza. Baada ya jaribio, washiriki waliulizwa kuhusu lugha za asili, kama na lini walijifunza lugha zingine mahali pengine au walipokuwa wanaishi.
Jaribio hilo lilishirikishwa zaidi ya mara 300,000 kwenye mtandao wa Facebook. Karibu watu 670,000 walifanya jaribio hilo, jambo lililowapa watafiti data kubwa za wazungumzaji wazawa na wasio wazawa wa wa umri wote wa lugha ya kiingereza.
Stadi za lugha zinaeleweka zaidi kwa watoto wenye umri mdogo
Uchambuzi wa majibu ya washiriki na makosa yao uliwasaidia watafiti hao kupata hitimisho la mchakato wa kujifunza lugha katika maisha ya mwanadamu.
Kwa kuongezea kuhusu kipindi kigumu cha kujifunza lugha mpya, Prof. Hartshorne anasema matokeo ya jaribio hilo yalionyesha kuwa wanafunzi wanaelewa zaidi kwa kushirikishwa kivitendo kuliko kusoma nadharia za darasani.
“Itakuwa rahisi ukiwa mtu mzima kutembelea nchi fulani ili kujifunza lugha mpya kuliko kujifunza darasani,” amesema Prof. Hartshorne.
Anaeleza kuwa kuboresha maisha siyo chaguo. Anapendekeza kuwa ili kujifunza haraka lugha ya pili ni vema kuishi mazingira waliopo wazungumzaji wazawa, kuliko kupata ujuzi kutoka kwenye vitabu vya lugha. Ukifanya hivyo, inawezekana kuwa mzungumzaji mzuri wa lugha hata kama siyo kwa kiwango cha juu.
Njia hiyo itawasaidia watu ambao wamemaliza shule ikiwemo madarasa ya awali na shule za msingi. Ubongo wa binadamu bado unakuwa katika nafasi nzuri ya kujifunza kivitendo kuliko watafiti walivyofikiri hapo awali katika utafiti wao.
“Tunabaini kwanini huwezi kuanza kuona ukosefu wa myumbuko mpaka kubarehe, ujana na ukiwa mtu mzima,” alisema Prof Hartshorne. “Kama wanasayansi, inatuvutia zaidi kuona jambo ambalo halijavumbuliwa, lakini lazima tujikumbushe kuwa tunatakiwa kuwa makini kuhusu vitu tusivyovijua. Inanishangaza, vitu gani vingine tusivyovijua?