Maaskofu: Wakristo Mwanza msile nyama iliyochinjwa na Waislamu!

Sitta Tumma

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, Umoja wa Makanisa ya Kikristo Jijini Mwanza, umetoa tamko kali kwa kuwataka waumini wa dini hiyo kutokula nyama yoyote iliyochinjwa wa Waislamu.

Tamko hili limetolewa leo (muda mfupi uliopita) na Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN), Boniphace Kwangu, mbele ya maaskofu wa madhehebu mengine, katika kikao cha pamoja kilichoketi kwenye moja ya majengo ya Kanisa la Kwa Neema Jijini Mwanza.

Kauli hiyo ya viongozi wa kiroho imekuja siku chache baada ya kuibuka mgogoro mkubwa baina Waislam na Wakristo juu ya nani mwenye halali ya kuchinja nyama hasa maeneo ya Machinjioni, mgogoro ambao Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Sera, Stephen Masatu Wassira uliomshinda kuutatua wakati alipotua jijini Mwanza kisha kuzungumza na viongozi wa pande zote mbili.

Mbali na Umoja huo wa madhebu ya Kikristo jijini Mwanza, unaojumuisha Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), na Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), umetangaza pia kusudio la kuufikisha mgogoro huo Mahakamani, ikiwa ni pamoja na kuitaka Serikali itafsiri kisheria ni nani hasa kati ya Waislamu na Wakristo mwenye mamlaka ya kuchinja nyama.

Tayari Serikali kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Injinia Evarist Welle Ndikilo pamoja na Waziri Wassira, ilishatoa msimamo wake wa kutaka kazi ya kuchinja nyama ni ya Waislamu na siyo Wakristo.

90 Comments
  • jamani ss huku niwapi tunakoelekea ndugu zangu? Mbona hayo mambo hayana tija kwenye ujenzi wa hili taifa?

    • Nawpongeza maaskofu kwa uamuzi weni. Lakini, nasikitika kuona kuwa haki za watu wengine zinapuuzwa na kupewa watu wengine ambao wanaonekana kuwa wajuzi tu wa kuongea tu.

      Naomba serikali ijue kuwa haki ya kuchinja siyo ya waislamu tu. Je, unafikiri kuwa katika nchi ambazo hakuna waislamu je nani huwa anachinja? Tena ikumbukwe juwa kama kuchinja ni jambo la ibada nani atakayekuwa nyama iliyotolewa kwa Mungu aiyemtii?

      • Jamani, kuhusu suala la kuchinja nalo tufanye kuwa ni haki ya Binadamu KAMA TUMEMNYIMA SISI? Sisi hiyo tunayo kwenye kitabu chetu ambacho QURAAN hebu niambie ww mtanzania ambaye unataka kuwe matabaka ya iman fupi ya bila kutaka kujua ukweli niambie kuna ufunuo gani mnao ambao umesema mchinje jaribu mtu wa kufkria kwa kina na kupata majibu sahihi.

  • NAUNGA MKONO TAMKO LA MAASKOFU.KILA MTU ALE ANACHOCHINJA,KWA NINI WATU WENGINE WACHINJE VYAO NA VYA WENGINE.MSIMAMO WA KIASKOFU NI SAHIHI.KILA MTU ALINDE IMANI YAKE

    • Kaka hatuendi kiivyo hata kidogo, hii inaeleweka wazi tangu na tangu kuwa Waislam ndiyo wenye kuchinja vya halali

       

        • Kaka hapa hakuna kukalili, Ni kufahamu kitabu kitakatifu kinasema nini.. Hakuna cha karne.

        • Kwanini kabla ya hapo hamkuliona hili.Au kuna AGANO JIPYA limeshuka karne ya 21? Tafakari kwa kina,hatutafika tunapopataka ndugu yangu wa kitaifa.

      • Sisi wakristo hakuna sehemu kwenye biblia inayosema hatuna haki ya kuchinja wala hakuna maelezo ya muislamu kuchinja so wajichinjie wenyewe coz ibada zipo tofauti. Maaskofu hongereni sana kwa kuchunga kondoo wa bwana ipasavyo

  • KILA MTU ANA IMANI YAKE,MAMBO YA IMANI NI YA MTU BINAFSI NA SI JAMBO LA KITAIFA. HATA MASHULE YA KIKRISTO YARUDISHWE YAENDESHWE KIKRISTO NA WAISLAMU WAENDESHE YA KWAO KIISLAM,HATA VYUO VIKUU NA KADHALIKA,YALE YA KITAIFA YAWE YA KITAIFA NA YALE YA KDINI YAENDESHWE KIDINI KWA AJILI YA WALE WALIOANZISHA.MIMI SIONI KAMA KUBNA KUSHIRIKIANA KATIKA MAMBO YA KIIMANI KWANI IMANI ZETU NI TOFAUTI SANA.ILA KWENYE MAMBO YA KIJAMII TUSHIRIKIANE.KWANI WAISLAMU KWA NINI WASICHINJE VYAO NA KUWEKA KWENYE MAFRIJI KAMA NI VINGI SANA.

    • na hela mnazopewa wakiristo na serikali kwa ajili ya uendeshaji wa mashule na mahospitali zirejeshwe serikalini toka mwaka 1961-to date, au zipigwe total na waislamu wapewe ili waendeshe mirad yao na kila mtu awe na chake.

  • Ni vema wakapeleka mahamani hilo suala la kuchinja ili likatafsiriwe vizuri. Tusiendeshe mambo kwa mazoea.

    Wapi wameandika katika katiba ya watanzania, (biblia kwa wakristo) na (koran kwa waislamu) kuchinja ni kwa waislamu tu. Kule kijijini wazee wangu wanachinja mbona hatujasikia kuwa wamepatwa na ugonjwa unaosababishwa na wakristo kuchinja. Hayo ni mazoea na yamepitwa na wakati.

    Huko machinjioni bwana kuna ajira, kunayo maisha huko asikudanganye mtu ukizingatia na uhaba huu wa ajira. Vijana wetu pia nao wanazitaka hizo ajira.

    Vinginevyo kuwe na varieties of mabucha na maduka ya kununua nyama. Kwani nini.

    Karne hii yenye watu wengi waliosoma kila kitu wanajiuliza WHY? Lazima kuwe na sababu ya kila kitu cha 'Do' na 'Don't Do'

    Kazi ya wale waliopewa madaraka ni kutoa majibu sahihi na siyo kutoa misimamo kama huko Mwanza, eti Serikali imetoa Msimamo. Siyo rahisi hivyo kwa siku hizi waheshimiwa.

    • Serikari yetu haina dini. Kwanini viongozi waseme kuchinja Ni kwa Waislam tu? Bora iwepo Couse ya kuchinja ili anaye soma Ndo apate iyo ajira Kama ajara zingine. Maswara ya waislamu ndo wachinje hatutaki, Kwani nikitugani wanachoweka cha Siri kwenye nyama?

      • Serikali haina dini. Dini ya serikali ni ukiristo kwa sababu wanafunzi wa kiislam na wafanyakazi maofisi ya serikali wanalazimishwa kupumzika siku za Jumamosi na J’pili ambazo wakiristo wanaamini Mungu alipumzika hivyo wanawalazimisha waislam kusherehekea siku hizo ambazo ni ibada za kikiristo.

        Kwa hiyo kama wakiristo wataruhusiwa kuchinja tunaomba serikali isizifanye siku hizi kwa ajili ya kupumzika kw sbb hawaamini km Mungu anachoka Hivyo hapumziki.

  • Serikali kwanini inaingilia masuala yakiimani? Jambo la msingi serikali ilipaswa iangalie sheria za nchi kwamba je mkristo akichinja anavuja sheria za nchi? Na kwa muislamu vivyohivyo kuna sheria ya nchi inampa haki ya kuchinja?

    Wasira alipaswa kusema maneno machache kwamba katiba ya nchi haijatamka mahali popote kwa mba nani anastahili kuchinja hivyo angewaomba viongozi pande zote wajadili kwa pamoja ili wafikie makubaliano kwa amani

  • Mi naona si sahihi! Haiwezekani waziri na mkuu wa mkoa watoe tamko! Inatakiwa kuwaomba wakristo wasijiskie vbaya wanapokula nyama iliyochinjwa na muislam na vivyo hivyo waislam nao!
    Kama vp kila mtu achinje vyake, hakuna haja ya kulumbana sana ktk mambo ya dini! Ni hatar sana ndugu zangu!
    Hivyo waziri na mkuu wa mkoa awaombe radhi wakristo kwa matamshi yao

  • Itikadi ya dini ni muhimu sana tokea mwanzo ilikwa inajulikana kabisa waislamu wana njia na utaratibu ktk kuchinja tofauti na wakristo na akichinja asie mislam inakuwa haiswihi ni kibudu sasa kama wakristo wameama kutoa azimio lazima wachinje basi kuwe na bucha za wakristo na bucha za waislamu zikaguliwe na viongozi wa dini ziwekewe bango maalmu la kuonyesha nyama hiyo ni halali hili lipo dunia nzima kuna sehem maalumu za waislamu hasa ktk nchi zilizo kuwa na wakristo wengi ikiwa wanataka na wao wapate ajira basi kutenganisha ilimradi kusiwe na ulaghai maana jukumu lote atalibeba anae danganyanya

    • Mimi ni Mkristo Mkatoliki tangu kuzaliwa hadi utu uzima wangu. Nimependa maoni ya Mohammed Hussein, ana uelewa mkubwa wa kuchambua mambo ni wazo zuri kufanya hivyo.

      Lakini angalizo langu, kwa mfano kwenye sherehe za Wakristo au Waislamu (namaanisha harusi, vipaimara, komonio, maulidi, eid, xmas au pasaka) tukialikana kwenye mambo haya ya kijamii japo ni ya kidini itakuwaje kwenye masuala ya vyakula?

      Je, Mwislamu atajuaje hii nyama iliyopikwa hapa imechinjwa na mwenzake? Na Mkristo pia atakumbwa na swali hili! Tutafanyaje? Vinginevyo, uchinjaji ni kitu kidogo sana ambacho kamwa hakiwezi kutugawa na kuingia kwenye uhasama wa kiimani/kidini.

      • Ama kwa hakika hakuna kitu kibaya kama udini katika nchi, kama tumefika hapo sidhani kama kutakuwa na amani katika nchi yetu. Mimi sidhani kama kuna kipengele katika BIBLIA kinaeleza kuwa kitoweo kikichinjwa na asiyemkristo kuwa si halali kwa mkristo, lakini katika QUR-AN kipengele hicho kipo. kuwa kitoweo kilichochinjwa na asiye Muislam si halali kwa Muislam.

        • Ebu hussein tuambie nini tofauti ya  neno Muislamu na uislam? Na umesema muislamu kula kitoweo kisichochinjwa na muislamu ni haramu. Kwanini? kina madhara gani?

  • Wassira awajibika vizuri na tupe majibu ya Msingi Watanzania ukizinhatia Wakristo.

    Wamekuwa watulivu vyakutosha wamechomewa makanisa bara na visiwani bado watumishi wamepigwa risasi huko Zanzibar Miaka yote tumefuata utaratibu.

    Wao wakichinja leo tunapohoji ni tatizo Maaskofu kazi nzuri bado mchezo wa kufanyiwa fujo na waisilamu ufike mwisho

  • hapo patam mbona rahisi tu wawe na machinjio yao bucha zao . maduka yao na serKali yao hao wakiristo hakuna taabu wao ni wadini hata tuwachpe bado watabaguana dawa yao ni AK47 watanyoka.

  • NAUNGA MKONO AZIMIO LA MAASKOFU: KAMA KUNA KUHESHIMIANA KATIKA IMANI NI LAZIMA HESHIMA HIYO IJENGWE KATIKA USAWA NA UHURU WA KILA MTU KUFANYA KILE IMANI YAKE INACHOMRUHUSU KUFANYA. KINACHONENWA WAKATI WA KUCHINJA HAKIKO KATIKA TARATIBU ZA DINI ZITE MBILI WALA HAKIJULIKANI KUWA NI NINI.

    AINA YA MAAGANO YANAYOINGIZWA KWA NENO LINALOTAMKWA KATIKA KUCHINJA KWA TARATIBU ZA KISLAMU TAFSIRI YAKE KIKRISTO NI NGUMU KUYAELEWA NA KAMA HAYAELEWEKI KUINGIA KICHWAKICHWA KATIKA MAAGANO USIYOTAELEWA KUN ATHARI KUBWA SANA ZA KIIMANI AMBAZO KANISA LAZIMA LIANGALIE KWA MAKINI SANA NGUVU HII ISIHARIBU MAISHA YA IMANI YA WAUMINI WA KIKRISTO.

    KILA MTU ACHINJE CHAKE KWA IMANI YAKE NA ALE BILA YA KUSENGENYWA AU KUBUGHUDHIWA NA MWINGINE. KAMA WEWE MUISLAMU UTAPENDA UCHINJE NA KUMTAKA MKRISTO ALE, BASI NA WEWE UKUBALI KUWA MKRISTO NAYE AKICHNJA KWA IMANI YAKE NAWE UTAKULA. KAMA SI HIVYO BASI KILA MMOJA AFANYE IMANI YAKE INAVYOMRUHUSU BILA KULAZIMISHANA. KUWE NA MACHINJIO NA MADUKA YA NYAMA YA WAISLAMU NA YA WAKRISTO BASI. UGONVI UTAISHA.

  • Naunga mkono tamko la maakofu,hebu ifike mahali wakristo wote tufunguke tuuelewe ukristo wetu na imani yetu na tena tuitetee, kabla hali haijawa sawa na ile inayowapata wakristo wenzetu wa NIGERIA

  • Ndugu zangu Waislamu ni vizuri sana tukajenga utamaduni wa kuheshimiana katika imani zetu!Ni kitu gani haswa ambacho Mkristo akichinja wewe kinakutia unajisi?au ni nyie mnafanya maagano gani na mnalazimisha wenzenu kula mnavyochinja na wao wakichinja nyie hamtaki!Nafikiri tengeni maeneo yenu na migahawa yenu muandike “HALAL”.Acheni kututesa jamani!hebu ukiheshimiwa na we pia uheshimu wenzio

  • Huyo anayesema itikadi, mara hapo zamani, akazidi kujikoroga ooh kibudu: hivyo ni vitu gani hasa kwenye kuchinja? Kama siyo mazoea na ku-copy na ku-pas- mila na desturi za watu fulani bila kufikiri.

    Kibudu ni nini, nani mwenye mamlaka na utaalamu wa kutamka kitu fulani ni kibudu, tangu zamani ilikuwa inajulikana kuwa wanautaratibu wa kuchinja-nani aliweka hizo taratibu na zamani maana yake nini. Yote haya mazoea na siyo sheria za nchi. Hata hapo zamani ilikuwa inafahamika kuwa kuna baadhi ya makabila duniani yalikuwa yanahusudu ukeketaji wa wanawake, unataka kutuambia uendelee!

    Kama wanaweza waishawishi jamii na serikali iingizwe kwenye sheria na katiba ya nchi. MAZOEA HATUTAKI

     

  • Nikwamba hakuna muislam kumchinjia mkristu tena hili swala lifanyiwe kazi Mara 1! Kila mtu adumu ktk imani yake. Sisi wakristu pia tuwe na butcha zetu ili Lila mmoja ale kilicho halali kwa imani yake.

  • Tatizo waislam wamezoeshwa na kuona ni haki yao kikatiba kuchinja.Kama wakristo wachache wakichinja na waislam wakanyamaza hili jambo lisingefika huko.

    Swali la kujiuliza;

    1. Kama kuchinja ni sehemu ya ibada, mbona wachinjaji wanalipwa pesa? Je, wakienda kuswali msikitini Ijumaa huwa wanalipwa?

    2. Kama kuchinja ni haki na ni sehemu ya ibada kwao, je, wapo tayari kuchinja nguruwe?

    3. Kwa nn wachinjaji wapangwe na viongozi wa kiislam na baadhi ya mapato yapelekwe kwa viongozi km hicho si kitegauchumi cha viongozi wa kiislam?

    Busara na hekima vinahitajika katika kutatua mgogoro huo. Kushindwa kufanya hivyo watakuja wasuruhishi nchini mwetu ndani ya mda mfupi badala ya sisi kwenda kwao.

  • SHETANI AMEWEKA MIZIZI TANZANIA SASA
    WAKRISTO WA KILEO HAWATAKI KUWA PAMOJA NA WAISLAMU WAKRISTO WA LEO WANAAKILI SANA KULIKO WALE WA ZAMANI HEBU HILI BALAA LIONDOKE ANAE TAKA BUCHA LA WAKRISTO AWEKE KAMA ILIVYO KWA MIDUME INAYOTAKA KUOLEWA. KWA WALE TULIOENDA KATIKA NCHI ZA WENZETU KUNA NYAMA ZINA LEBO (HALAL) NA ISIYO NA ALAMA HIYO KWA ANAE RUHUSIWA ANAENDELEA. SHETANI KATUA NA MENGI YATAKUJA KAMA ILIVYO UTITIRI WA MAKANISA

    • Amani ya ALLAH iwe nanyi. Ndugu zangu watanzani kwanini tuhitirafiane kwa jambo ambalo lipo wazi ktk vitabu vyetu. Tusiwe watanzania wa kushabikia vitu tucvyo vifaham. Hili linatokana na kutosoma dini zetu, tumekaa kutega masikio tukisikia jambo tunaibuka kushabikia bila kuchunguza madhara yake.

      Ni hayo tu.

  • Ninaunga mkono azimio la Maaskofu kwamba kila mtu achinje chake kwa imani yake  ili asile kilicho  najisi  kwakwe.  Yamkini kuna maagano au sala inayofanyika wakati watu wanachinja nyama katika imani zao ndiyo maana waislamu wanang'angania wao wachinje na wakristo  wale vitu ambavyo hawajui pengine wananajisika kwa imani yao." KWANINI NINUNUE MFUGO WANGU ALAFU WAKATI NATAKA KULA NYAMA ETI AJE MTU ASIYE HUSIKA  ANICHINJIE" ?

    Kama waislamu hawataki kukubaliana na hili basi kuwe na MABUCHA  ya WAISLAMU na WAKRISTO  tuwe na MABUCHA YETU.

    • Wakristo hamna kharam wala halali katika suala la wanyama. Waislamu tunautaratibu wa kuchinja, Allah katuelekeza.

      • Maoni ya wengi ni mazuri ila mimi naona katika katiba ijayo hiki kipengele kiwepo na kiwe hivi: Kila mtu achinje na ale kwa mujibu wa imani yake bila kubugudhiwa na mtu au imani fulani,pili kuwe na mabucha ya kikristo na ya waislam ili kila mtu aende pale anapopaamini. Haina mantiki kama kitabu cha dini fulani kimesema nani achinje au nani asichinje ndio kifuatwe na wote kwa kua kila mtu huamini maelekezo ya kitabu chake basi hakuna haja ya mmoja kulazimisha mwenzake kuamini kitabu anachokiamini. Na kama ni sherehe ambayo itahusisha wageni wa imani tofauti mwenye sherehe atazingatia utaratibu na kuhakikisha imani ya pande zote 2 inaheshimiwa. Watanzania tupanuwe wigo wa frika zetu,(look at extra mile) amani tulionayo ikitoweka ni hasara kwa pande zote 2 na vita hii haitakuwa na mshindi kama mnavyofikiri. God bless TZ, God bless people of this land.

  • SERIKALI KWANINI ISIJIULIZE KWAMBA AKICHINJA MKRISTO KUNA TATIZO GANI ? AMA KUNA KIFUNGU GANI CHA SHERIA KITAKUWA KIMEVUNJWA ?

    JE TAFSIRI YA DEMOCRACIA NI NINI ?  SI KWAMBA WATU WAISHI KWA UHURU WA MATAKWA YAO ILA WASIVUNJE SHERIA ?  AU  TUNAPELEKWA WAPI.

  • WEKA TAMKO LENYEWE TUONE LINAVYOSOMEKA MKUU, mjadala hunoga kwa kuwa na guts, siyo chewed information

  • Naomba Mwenyezi Mungu aingilie kati suala hili, maana mambo ya UDINI yatatufikisha pabaya.  Amani itaoweka kwa ajili ya kuchinja tu.  Serikali, viongozi wa Dini zote  waingilie kati kurudisha amani na kuwaelewesha waumini wao nini kifanyike

  • Kwa maoni yangu wanachokosea waislam ni kulichukulia suala la kawaida la imani yao ya kuchinja kuwa ni suala la kitaifa hususan pale wakristo katika shughuli zao binafsi wanachinja.

    Kwa wakristo kula alichochinja muislam biblia inasemaje? Labda mgogoro uliowakumba Warumi Wakati aw Mt. Paulo unatufubdisha. Warumi wasio wakristo walikuwa wanachinja na kuombea kwa miungu yao. Wakristo wakaanza kulaumiana.
    1. Wako waliokataa kula nyama wakawa wanakula mboga.
    2. Wengine wakawa wakila nyama Hiyo. Mt. Paulo katika Warumi 14 anawaandikia akiwaasa wasihukumiane. Paulo Anaona kula au kutokula ni suala la dhamira zaidi kuliko kiroho. Ndiyo maana anawashauri.

    Yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, walakini maim hukumu mawazo yake. Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula mboga." (Warumi 14:1,2).

    Unaona, Paulo anachokiona mtu anayechinja akiomba kwa miungu Yao Paulo Anaona ni Kama haina uhusiano kiroho., aliyekomaa kiimani hula vyote akimshukuru Mungu… Just my opinion.

    Bishop Kaganga (Zanzibar).

    • Mimi ningeshauri suala la kuchinja au kula nyama na vyakula vingine si kosa bali pale mnyama anaichinjwa kwa imani fulani ndo tatizo, wakristo wamekatazwa kula nyama au vyakula vilivyotolea sadaka kwa miungu au sanamu, haijalishi uhalali wa mnyama, kinachotakiwa asiwe wa kafara kwa dini au kijimungu cha aina yeyote. Kwa wakristo ni dhambi labda ale kwa kutokujua, na Serikali inapaswa kutoingilia kati imani za watu, kuchinja haipo ktika katiba, mabucha ya serikali; wachinjaji wawepo wa dini zote ili kuondoa dhana potofu

  •  Kwa mkristo kula nyama iliyochinjwa aidha na muislamu au na mkristu si najisi, hivo kama suala ni ajira machinjioni ni suala la serikari kujiuliza kutenga machinjio na mabucha ya kikristo na kiislamu ili wote wapate ajira (wakristo na waislamu).

  • Raia mwema … "Tumekaririshwa kwa miaka 50 kuwa serikali yetu haina dini na kuwa masuala ya dini ni nje ya shughuli za serikali. Baba wa Taifa letu mpaka leo anatusuta kwa kutuhoji, “hivi tunauliza dini ya mtu katika uchaguzi kwani anakwenda kuswalisha?”

    Serikali yetu haijawahi kuwa na dini na kwa hiyo haijui kitoweo kinachinjwa kwa dini gani? Waziri Stephen Wassira amepata wapi madaraka ya kuwafundisha Watanzania dini ya kuchinja wanyama na ndege? Kule kwetu tunakula mbwa na twaweza kuuza kitoweo cha mbwa sokoni – dini gani itusaidie kuchinja ka-mbwa ketu? Mtaani kwetu Kitunda Dar es Salaam tuna bucha ya nguruwe na tunauza sokoni- dini gani ije kutuchinjia?

    Kule Kigoma nasikia (kama ni kweli) wapo wanaofurahia kitoweo cha nyoka, nungunungu, nyani na tumbili; Je, Waziri Wassira atapeleka dini gani kuchinja huko Kigoma? Yapo makabila ambayo hata hula kitoweo cha binadamu mwenzao maadam hawakumuua, dini gani itawachinjia? Ni sahihi kuhoji, maana kibudu cha mwenzako, halali ya mwingine.

    Hivi kweli dini imekuwa ni agenda ya muhimu kwa serikali hii? Mambo ya kuchinja vitoweo hujiongoza yenyewe na tangu kale hayajawahi kuwa agenda ya mtemi, liwali wala gavana. Tujiandae sasa kuona nchini kote bucha za wanaosali Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. Tunawaonea sana wasiosali popote tunapong’ang’ania kuweka dini katika kila jambo. Baada ya bucha, tutahamia kwenye vyoo vya kidini, magereza ya kidini, mahakama za kidini, na hata magonjwa ya kidini.

    Hivi sasa tuna magazeti ya kidini, redio za kidini, televisheni za kidini, zamu za kidini ikulu, shule za kidini, na vyama vyetu tunalazimisha kuvifanya vya kidini. Kama dini imekuwa ya muhimu kwa vitoweo huko Mwanza, mbona mahekalu yalichomwa moto lakini hatukumwona Wassira akiitisha mkutano wa viongozi wa dini? Padre akapigwa risasi, hatukusikia mkutano wa viongozi wa dini na ikulu. Msaidizi wa Mufti akamwagiwa tindikali hatukuona Wassira akipanda boti kwenda Zanzibar kuonana na mashehe. Ibada za Krismasi ziliendeshwa zikilindwa kwa  mtutu wa bunduki lakini hatukuona  mkutano wa ikulu na viongozi wa dini.

    Hata pale viongozi wa dini walipoomba kukutana na ikulu, walikataliwa lakini safari hii “kuchinja” kumeitoa ikulu kukutana nao. Hivi sasa viongozi wakuu wa dini nchini kote, usalama wao uko shakani na wanalazimika kujilinda lakini ikulu hiyo haijasema kitu kuhusu tishio hilo, ila inakimbilia Mwanza kufundisha namna ya kuchinja wanyama kwa kutumia dini."

  • jamani hebu tukae chini bila jazba tujadili suala hili kwa manufaa ya wafanyabiashara ya kuuza kitoweo la sivyo hali itakuwa sio shwari

  • jamani nyie wenzetu ebu tutumie busara,haya mambo ya kutoa tamko yanatoka wapi? nafikiri nyie ni wasomi tumieni elimu zenu kutatua na sio kutoa matamko.NAOMBA TUSIPOST MAMBO KWA USHABIKI THINK FIRST AND THEN DELIVERY IT.

  • Tuliyokuwa tunasikia kwenye vyombo vya habari, Hakika ndo vinanyemelea. Haya mambo ya udini yanasababishwa na nini?
    Ninachoamini viongozi wetu wanawaongoza Watanzania wenye itikadi za kiimani tofauti.
    Ya nini kuelekeza uzito upande m1?
    Tujiulize
    utaratibu wa awali ulokuwaje?
    ulikuwa na madhara gani,
    na kwa nini sasa yatokee haya?
    HOFU YA MUNGU ITANDE!!!
    Tunaelekea wapiii!!!!

  • Malumbano ya kidini yatatufikisha mahala pabaya katika historia ya nchi yetu, yatupasa kutambua kuwa hakuna itikadi imani moja ya dini iliyo bora zaidi ya imani nyingine (iwe ni wakristu, waislamu au wapagani)! hivo basi viongozi wa kiroho pamoja na viongozi wa serikali yawapasa kutumia busara na hekima katika kutatua tofauti za kiimani zinazojitokeza.

    Binafsi suala la kuchinja la kuiajiri itikadi fulani ya kiimani kuimiliki kama taass badala yake kila mwenye uwezo wa kuchinja katika mahali sahihi afanye hivo bila kigezo cha kidini! kw akufanya hivo tutaimarisha mshikamano wetu hadimu wa kitaifa!

    CHONDE CHONDE VIONGOZI MSIRUHUSU UFISADI WOWOTE WA KIUPENDELEO KATIKA HILI, KWANI SERIKARI HAINA DINI!

  • Serikali ni katiba, wasira ni mtu tu.

    Mi nashangaa mtu kachemsha, wanahangaika na maneno ya kilaza. Hivi ikiwa kila mtu aongee jambo halafu tulizingatie itakuwaje? Sioni hoja ya msingi. Wakristo anzisheni bucha zenu si kosa kikatiba, acheni kugombana wakati mnaweza kuliamua jambo hili.

  • Wakristo wa Kwanza ambao walikuwa Wazungu waliokuwa Wanatawala nchi hii waliona busara kuwepo Mahakama ya Kadhi na huu utamaduni wa Waislamu kuchinja ….!

    Lakini wamekuja wajuaji wajinga sisemi Wapumbavu wanaona kila kitu alichofanya Mtawala Mzungu Mkristo mpumbavu …sasa hili linakuwa pandora box (boksi la kubahatisha) ndani ni bahati yako lakini unaweza ukatoka na nyoka badala ya sungura…Sasa baada ya ku-undo kidotcom..Mnaonaje Waislamu wakija na hoja ku-undo siku za kupumzika maana siku zote Jumamosi na Jumapili zinawapendelea Wakristo je na wao hawana haki ya kupumzika Ijumaa.?..Mimi nimefikiri kwa sauti tu…Dini hizi sio za dot-com mkiingiza mambo ya dot-com tutakwama..! Turejee utamaduni wa uhusisno wa dini hizi ulioanza karne nyingi zilizopita na sisi tukazirithi….Hivi vionjo vya kisiasa mamboleo zitatuangamiza…

    Wakristo hawa  wa sasa wanafuata vitabu gani sio Biblia..? Wape ushauri watu wenye busara na hekima watazidi kuelewa na kuongeza hekima yao..lakini ukiwapa ushauri watu wasioshaurika…wasiotaka mifano hai …bila ya shaka Jamii yetu tumekabiliwa na uasi wa ajabu…! Maana kila jambo zuri kuna watu wanahamu ya kulifumuwa ..Sijasikia hata siku moja hawa jamaa wanavamia baa, madanguro vijiwe vya unga kuwaadabisha watuhumiwa …! Nini hichi ….

    Katika watu wanaoamini vitabu Wakristo na Waislamu ni ndugu ..Sasa hawa Wakristo wasioamini yale yaliotendwa na Mfalme wa Abyssinia siku hizi Ethiopia akawahifadhi Waislamu ..japo kulikuwa na shinikizo la Mapagani (Makuresh kutoka Makka) wakaenda na zawadi za thamani kubwa (rushwa) zao wakidai wale Waislamu ni watumwa wao  waliotoroka..Mfalme yule Mkristo alikataa rushwa zao na akatoa amri kwa Waisalmu waendelee kuishi Ethiopia na kutekeleza Ibada yao bila ya vikwazo vyovyote hadi watakapoweza kurejea nchini kwao Arabuni.! Wakristo wetu hawa kweli wanaweza kufanya kama Mfalme wa Ethiopia? Tumeingiliwa na shetani tutafute mpungaji ama sivyo tutakwisha! Ni ajabu watu kuacha mwafaka wa karne na karne na kuanza harakati za mapambano..!

    Mungu Awabariki Wakristo na Waislamu na Watanzania wote kwa jumla!

  • jamani, tunakokwenda ni wapi?

    Ni nani aliyeibua suala hili la kuchinja, alikua na madhumuni gani?

    Ni kweli kua huu ndio msimamo wa maaskofu wote au ni wa Askofu Boniphace Kwangu tu?

    Kwangu naamini serikali haina dini na wala haiko kwa maslahi ya dini fulani au kikundi fulani cha watu, BALI ni kwa ajili ya kutoa haki sawa kwa watu wote bila kujali itikadi zao.

    Naomba hekima na busara zitumike katika suala hili, leo tukisema waislam na wakristo wawe na machinjio yao kesho yataibuka masoko,hospitali, magari n.k

    Viongozi husika nawaomba kukaa chini ili kufikia muhafaka hasa kipindi tunapoelekea uchaguzi 2015, suala hili litatuletea vita,ubaguzi hata kuondoa utu wetu na maendeleo yetu kuporomoka.

    Watanzania tuishi kama watanzania, itikadi za kidini zisitutenganishe. Sisi sote ni wamoja, tudumishe umoja wetu.

  • Mdachi ktk Tanzania Daima 03 Feb 2013 ……Niliandika pia Sherehesho ya Ayaya 5 ya Surat Al-Maidah-Suraya 5 ambayo iliniletea changamoto toka kwa wadau wengi wakitaka niwafafanulie au niwaeleze neno ‘Mnasara’ maana yake nini.

    Naomba ninukuu tena ‘sherehesho’ hilo ndani ya Kurani- “Chakula cha kuchinja hakiwi halali kwa Waislamu ila kichinjwe na (a) Muislamu au Kichinjwe na (b) Myahudi au (c) Mnasara, kwa sharti lile la kuchinja sio kunyonga. Soma ukurasa 146 tafsiri ya Kiswahili Kurani iliyoandikwa na Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy; toleo la 1969-1991-aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Kenya.

    Nililazimika kuyaweka haya wazi kutokana na mzozo uliozushwa na baadhi ya waumini wa Kiislamu huko Mwanza wa kuzuia Wakristo wasichinje wanyama katika machinjio ya wote na wakapata ‘sapoti’ ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, EvaristNdikilo, japokuwa hakuna sheria hiyo ambayo hadi leo kiongozi huyo hajaielezea wazi.

    NASARA au MNASARA ni nani? Ukisoma Kamusi ya Kiswahili Sanifu toleo la 1981-ukurasa wa 210, neno hilo limeelezewa kuwa ni MKRISTO na hakuna maelezo ya zaidi. Kwa hiyo Kurani imemruhusu Myahudi na Mkristo kuchinja kwa sharti ile ya kuchinja na sio kunyonga. Aya ya 5 Surat Al-Maidah Sura ya 5-imesema, nanukuu: “Chakula cha Watu wa Kitabu (AhlulKitab) ambao ni Wakristo ni halali kwao Waislamu na hakuna maelezo ya ziada ndani ya Kurani ya namna gani Wakristo hao wamechinja.

    Hivyo, kwa andiko hilo haieleweki wale walioanzisha mjadala huu waliegemea wapi au wanalenga kitu gani kwa Watanzania.

    Ipo Hadithi ya Mtume Mohammed (S.A.W) katika kitabu cha Sahih Al-Bukhari watu walimuuliza Mtume: “Watu hutujia na nyama hatujui kama wametaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kuchinja au la!”

    Mtume akawaambia: “Semeni Bismallahi kisha mle.”

    Safari moja aliulizwa Abu Dardaa kuhusu beberu aliyechinjwa kwa ajili ya kanisa linaloitwa Jurjus, “Utakula nyama yake?”

    Akajibu: “Ewe Mola naomba msamaha na wao ni watu wa Kitabu (AhlulKitab) chakula chao ni halali kwetu na chetu ni halali kwao.”

    Akaamrisha kiliwe! Soma kitabu ‘Al-Halal wa Haram Fyl Islam’ (Halali na Haramu katika Uislamu) ukurasa 68 kilichoandikwa na Ustadh Yusuf Al-Qaradhawi toleo la 2006.

    Niliandika pia Sherehesho ya Ayaya 5 ya Surat Al-Maidah-Suraya 5 ambayo iliniletea changamoto toka kwa wadau wengi wakitaka niwafafanulie au niwaeleze neno ‘Mnasara’ maana yake nini.

    Naomba ninukuu tena ‘sherehesho’ hilo ndani ya Kurani- “Chakula cha kuchinja hakiwi halali kwa Waislamu ila kichinjwe na (a) Muislamu au Kichinjwe na (b) Myahudi au (c) Mnasara, kwa sharti lile la kuchinja sio kunyonga. Soma ukurasa 146 tafsiri ya Kiswahili Kurani iliyoandikwa na Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy; toleo la 1969-1991-aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Kenya.

    Nililazimika kuyaweka haya wazi kutokana na mzozo uliozushwa na baadhi ya waumini wa Kiislamu huko Mwanza wa kuzuia Wakristo wasichinje wanyama katika machinjio ya wote na wakapata ‘sapoti’ ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, EvaristNdikilo, japokuwa hakuna sheria hiyo ambayo hadi leo kiongozi huyo hajaielezea wazi.

    NASARA au MNASARA ni nani? Ukisoma Kamusi ya Kiswahili Sanifu toleo la 1981-ukurasa wa 210, neno hilo limeelezewa kuwa ni MKRISTO na hakuna maelezo ya zaidi. Kwa hiyo Kurani imemruhusu Myahudi na Mkristo kuchinja kwa sharti ile ya kuchinja na sio kunyonga. Aya ya 5 Surat Al-Maidah Sura ya 5-imesema, nanukuu: “Chakula cha Watu wa Kitabu (AhlulKitab) ambao ni Wakristo ni halali kwao Waislamu na hakuna maelezo ya ziada ndani ya Kurani ya namna gani Wakristo hao wamechinja.

    Hivyo, kwa andiko hilo haieleweki wale walioanzisha mjadala huu waliegemea wapi au wanalenga kitu gani kwa Watanzania.

    Ipo Hadithi ya Mtume Mohammed (S.A.W) katika kitabu cha Sahih Al-Bukhari watu walimuuliza Mtume: “Watu hutujia na nyama hatujui kama wametaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kuchinja au la!”

    Mtume akawaambia: “Semeni Bismallahi kisha mle.”

    Safari moja aliulizwa Abu Dardaa kuhusu beberu aliyechinjwa kwa ajili ya kanisa linaloitwa Jurjus, “Utakula nyama yake?”

    Akajibu: “Ewe Mola naomba msamaha na wao ni watu wa Kitabu (AhlulKitab) chakula chao ni halali kwetu na chetu ni halali kwao.”

    Akaamrisha kiliwe! Soma kitabu ‘Al-Halal wa Haram Fyl Islam’ (Halali na Haramu katika Uislamu) ukurasa 68 kilichoandikwa na Ustadh Yusuf Al-Qaradhawi toleo la 2006.

    Niliandika pia Sherehesho ya Ayaya 5 ya Surat Al-Maidah-Suraya 5 ambayo iliniletea changamoto toka kwa wadau wengi wakitaka niwafafanulie au niwaeleze neno ‘Mnasara’ maana yake nini.

    Naomba ninukuu tena ‘sherehesho’ hilo ndani ya Kurani- “Chakula cha kuchinja hakiwi halali kwa Waislamu ila kichinjwe na (a) Muislamu au Kichinjwe na (b) Myahudi au (c) Mnasara, kwa sharti lile la kuchinja sio kunyonga. Soma ukurasa 146 tafsiri ya Kiswahili Kurani iliyoandikwa na Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy; toleo la 1969-1991-aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Kenya.

    Nililazimika kuyaweka haya wazi kutokana na mzozo uliozushwa na baadhi ya waumini wa Kiislamu huko Mwanza wa kuzuia Wakristo wasichinje wanyama katika machinjio ya wote na wakapata ‘sapoti’ ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, EvaristNdikilo, japokuwa hakuna sheria hiyo ambayo hadi leo kiongozi huyo hajaielezea wazi.

    NASARA au MNASARA ni nani? Ukisoma Kamusi ya Kiswahili Sanifu toleo la 1981-ukurasa wa 210, neno hilo limeelezewa kuwa ni MKRISTO na hakuna maelezo ya zaidi. Kwa hiyo Kurani imemruhusu Myahudi na Mkristo kuchinja kwa sharti ile ya kuchinja na sio kunyonga. Aya ya 5 Surat Al-Maidah Sura ya 5-imesema, nanukuu: “Chakula cha Watu wa Kitabu (AhlulKitab) ambao ni Wakristo ni halali kwao Waislamu na hakuna maelezo ya ziada ndani ya Kurani ya namna gani Wakristo hao wamechinja.

    Hivyo, kwa andiko hilo haieleweki wale walioanzisha mjadala huu waliegemea wapi au wanalenga kitu gani kwa Watanzania.

    Ipo Hadithi ya Mtume Mohammed (S.A.W) katika kitabu cha Sahih Al-Bukhari watu walimuuliza Mtume: “Watu hutujia na nyama hatujui kama wametaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kuchinja au la!”

    Mtume akawaambia: “Semeni Bismallahi kisha mle.”

    Safari moja aliulizwa Abu Dardaa kuhusu beberu aliyechinjwa kwa ajili ya kanisa linaloitwa Jurjus, “Utakula nyama yake?”

    Akajibu: “Ewe Mola naomba msamaha na wao ni watu wa Kitabu (AhlulKitab) chakula chao ni halali kwetu na chetu ni halali kwao.”

    Akaamrisha kiliwe! Soma kitabu ‘Al-Halal wa Haram Fyl Islam’ (Halali na Haramu katika Uislamu) ukurasa 68 kilichoandikwa na Ustadh Yusuf Al-Qaradhawi toleo la 2006.

    Niliandika pia Sherehesho ya Ayaya 5 ya Surat Al-Maidah-Suraya 5 ambayo iliniletea changamoto toka kwa wadau wengi wakitaka niwafafanulie au niwaeleze neno ‘Mnasara’ maana yake nini.

    Naomba ninukuu tena ‘sherehesho’ hilo ndani ya Kurani- “Chakula cha kuchinja hakiwi halali kwa Waislamu ila kichinjwe na (a) Muislamu au Kichinjwe na (b) Myahudi au (c) Mnasara, kwa sharti lile la kuchinja sio kunyonga. Soma ukurasa 146 tafsiri ya Kiswahili Kurani iliyoandikwa na Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy; toleo la 1969-1991-aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Kenya.

    Nililazimika kuyaweka haya wazi kutokana na mzozo uliozushwa na baadhi ya waumini wa Kiislamu huko Mwanza wa kuzuia Wakristo wasichinje wanyama katika machinjio ya wote na wakapata ‘sapoti’ ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, EvaristNdikilo, japokuwa hakuna sheria hiyo ambayo hadi leo kiongozi huyo hajaielezea wazi.

    NASARA au MNASARA ni nani? Ukisoma Kamusi ya Kiswahili Sanifu toleo la 1981-ukurasa wa 210, neno hilo limeelezewa kuwa ni MKRISTO na hakuna maelezo ya zaidi. Kwa hiyo Kurani imemruhusu Myahudi na Mkristo kuchinja kwa sharti ile ya kuchinja na sio kunyonga. Aya ya 5 Surat Al-Maidah Sura ya 5-imesema, nanukuu: “Chakula cha Watu wa Kitabu (AhlulKitab) ambao ni Wakristo ni halali kwao Waislamu na hakuna maelezo ya ziada ndani ya Kurani ya namna gani Wakristo hao wamechinja.

    Hivyo, kwa andiko hilo haieleweki wale walioanzisha mjadala huu waliegemea wapi au wanalenga kitu gani kwa Watanzania.

    Ipo Hadithi ya Mtume Mohammed (S.A.W) katika kitabu cha Sahih Al-Bukhari watu walimuuliza Mtume: “Watu hutujia na nyama hatujui kama wametaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kuchinja au la!”

    Mtume akawaambia: “Semeni Bismallahi kisha mle.”

    Safari moja aliulizwa Abu Dardaa kuhusu beberu aliyechinjwa kwa ajili ya kanisa linaloitwa Jurjus, “Utakula nyama yake?”

    Akajibu: “Ewe Mola naomba msamaha na wao ni watu wa Kitabu (AhlulKitab) chakula chao ni halali kwetu na chetu ni halali kwao.”

    Akaamrisha kiliwe! Soma kitabu ‘Al-Halal wa Haram Fyl Islam’ (Halali na Haramu katika Uislamu) ukurasa 68 kilichoandikwa na Ustadh Yusuf Al-Qaradhawi toleo la 2006. ….

    • Naomba unielimishe baina ya Unasara wa nabii Isa,ule wa awali na huu uliopo sasa ni sawa?

  • NIKWELI KABISA SISI WATANZANIA  HATUNA BUDI KUENNDELEZA MIKAKATI BABA WATAIFA ALIYO TUWEKEA KWANI YEYE ALIKUA ANAJUA ANACHOFANYA ANGALIENI MAMBO  YANAYO ANZAKUTOKEA  watanzania TUNAKWENDA WAPI JAMANI

  • Hili jambo limezuka kwa maslahi ya nani? Mwalimu Kambarage alifanya hivi:

    Wakristo wakubali kula iliyochinjwa na waislamu,

    waislamu wakubali kufanya kazi Ijumaa.

    ili siku za mapumziko ziwe zile siku za ibada za ki kristo, cha ajabu hata viongozi wameshindwa kulisema hili wanatoa majibu ya nguvu yasiyo na tija

     Mimi nawaomba tuwe wamoja tusirumbane kwa vitu vilivyokwishawekewa utaratibu, maana hili liliwekewa utaratibu huo nilioueleza tangu zama za 1961

  • Tofauti ya wanavyochinja waislamu na wakristo ni kuwa; waislamu dini yao imeeleza vipi mnyama achinjwe na wataalamu wa afya wamethibitisha kuwa taratibu za kuchinja za waislamu zina faida ya kiafya kuliko taratibu nyengine. Lakini wanavyochinja kwa mfano wakristo, kwanza biblia haikufundisha jinsi mnyama anavyochinjwa.

    Sasa kama wakristo wanahisi haifai kula nyama iliyochinjwa na waislamu, basi kuwe na mabucha ya waislamu na wakristo

  • Nyama yangu anachinja mume wangu mwenyewe. asiyetaka kula aache.kama dini yako imekuambia kuchinja nyama kwa mkristo ni vibaya, hiyo ni kimpangio wako.Shida zako tu mwenyewe zimekushinda, kutatua za watu utaweza.acheni viherehere.

    Bwana Yesu Asifiwe.

     

  • Mimi naona tunapoelekea siko kabisa, miaka yote naona wanachinja waislam iweje leo wadai hayo huu ni uchochezi usio na msingi wowote ni upoteshaji wa jamii kwani viongozi wa enzi hawaja liona hili wataka tulishwe vibudu tu sasa.

  • Serikali isituchezee wakristo kwa sababu ya uvumilivu na ustaarab wetu wakristo.

    Kwa agizo hilo inathibitisha utengano uwepo.Serikali isiyo na dini haifanyi maamuzi KI-UJASILIA KURA. Mambo mengine si ya kutafutia kura. Tugawane tu mabucha kwa sababu wao hawawaamini hata viongozi wao wenye nchi. Unajua ukikuta kikundi hakitaki kuwa na utaratibu wa uongozi ndio hivyo.

    Kila mmoja huwa na kiongozi wake anaye mwamini. Nawaomba wakristo tukumbuke kuwa YESU hakutaka kuwa kiongozi wa kisiasa DUNIANI, maana yake dini na siasa ni vitu tofauti kibiblia. Lakini muda wa kusimama IMARA ndiyo HUU.

    • hata mimi nadhani sisi wakrito huu ndio muda wetu kuungana na kujilinda dhidi ya hawa waislamu  wanao abudu waarabu na kumwacha mungu.

      • Acha izo kaka hakuna anaye abudu mwarabu hapa, Tatizo  baadhi ya wakristo wanadhani kuwa, ukristo umetoka kwa wazungu….!!

         

  • Mimi nashangaa ubinafsi wa baadhi ya wenzetu wakristo, eti wakristo tumekuwa wavumilivu sana! Hivi ni nani katika nchi hii amekuwa mvumilivu! Waislamu wamekuwa wakienda kazini siku ya ibada ila wakristo wakipumzika siku zao za ibada huku waislamu wakiendelea kuchapa kazi bila kelele za kipuuzi kama hizi za kung’ang’ania kuchinja.

    Serikali imekuwa na mahusiano ya kibalozi na vatican bado ila suala la OIC likiwa gumzo na bado waislamu kwa busara zao wameamua kunyamaza. Hivi ni nani amewalazimisha kula wanachochinja waislamu!

    Nawapongeza viongozi wenye busara na kulizungumzia hili bila kujali imani zao.nchi hii ina matatizo mengi ambayo nilifikiri watu wenye akili zao wangepoteza muda wao katika haya kwa manufaa ya taifa letu.wengine ndani ya taifa hili familia moja ina watu wa dini tofauti lakini wamekuwa wakiheshimiani kwa yale ambayo yanamuhusu mwingine. Na malizia kwa kusema hivi; waislamu wameungwa mkono na serikari kwenye hili sasa wataendelea kuchinja atakaye kula sawa asiyetaka anunue ng’ombe wake achinge mwenyewe hakuna muislamu atakaye muingilia ila kuingilia imani yetu mwiko.

    NAKIRI KWA MOYO NA KUBAINI KWA ULIMI KWAMBA HAPANA MOLA HAPASWAE KUABUDIWA KWA HAKI ILA MWENYEEZI MUNGU NA MUHAMMAD NI MTUME WAKE.

    • ndugu rama inatakiwa ujue kwamba vatican ni nchi kama ilivyo pakistan,saudiarabia na qatar. kwahiyo kama Tanzania ina urafiki wa kibalozi na nchi za kiislamu kama nilizokutajia basi sio tatizo kwa Tanzani kuwa na urafiki wa kibalozi na vatican, nadhani umenielewa

  • Ndugu zangu watanzania,angalieni kwa makini bila kuangalia udini.sheikhe ponda,amekosa dhamana lulu mwenye kesi ya mauji kapewa dhamana.Tunajifunza nini?kwenye serekali yetu?.

    • ndugu sudi,

      shekh ponda ni muhuni asiyejua utawala wa sheria kwasababu kama alidhani kuwa bakwata hawajafuata sheria basi alitakiwa kama kiongozi aende mahakamani kuwashtaki bakwata lakini  kwa ufinyu wa fikra yeye alienda kuwachukuwa wahuni na kwenda kuleta vurugu na  kupora mali za yule mmiliki wa kile kiwanja

  • Kama wakristo wanataka haki ya kuchinja wapewe… kama wanaona na wao wana haki wapewe…

    Ila sasa ni lazima tuwe na mabucha ya WAISLAM na WAKRISTO.

    Hii ni kwa sababu sisi waislam hatuwezi kula nyama iliyochinjwa kwa kumtaja yeyote isipokua ALLAH (nina maana ya MUNGU muumba mbingu na ardhi na vilivyomo). Kinyume chake uchnjaji huo kwa muislam ni BATILI. Iwapo umechinja kwa kumtaja BWANA YESU, kwa imani yetu sisi umefanya SHIRK kwa sababu kwetu sisi yetu ni kiumbe wa Allah aliyemteua kuwa mmoja wapo wa Mitume wake. Hivyo ndio kusema kama wakristo na wao itikadi ya Waislam ya kuchinja kwa kumtaja ALLAH – Mungu mmoja aliyeumba kila kitu hawaitaki na ni kero kwao basi wapewe RUKSA wachinje ila tunaomba mabucha yatenganishwe kuwe na MUSLIM BUTCHERY na CHRISTIAN BUTCHERY kama ilivyo kwenye nyumba za ibada….. haina haja ya mzozo ndugu zanguni

    • Tatizo siyo kuchinja , bali tatizo ni watanzania wengi hatuna elimu ya kutosha , ili kumjuwa jirani yako , anaamini nini ? mkrito au muislam ?nini imani ya kislam inasema ,  na nini imani ya kikrito inasema je ??na pia kuwa na utaratibu mzuri wa kuweka , ili iwe wasi kujuwa nyama hii ni kwa nani? nafikiri ni zuri sana iwepo taratibu za kuweka mabucha kwa mchakatuo wa mabucha ya kikristo na ya kislam , ilo siyo tatizo , mbona tuna mabucha nyama za nguruwe uswahili , na ndugu zetu waislam wanajuwa wazi kwamba nyama hiyo kwao ni haram , na pia kuna wakristo pia hawaitumii, lakini mbona hapakuwepo na TATIZO lolote , mimi nakuunga mkono Mohamed Mauly

  • kimsingi aya matatizo ya viongozi wa dini kuingilia hadi mfumo wa mtu wa kuishi huwa yana changamoto mno.hata waislamu wanaonywa kula nguruwe lakini matokeo huwa hayako verymuch pleasing. nadhani kabla hujamwonya mtu nini ale na nini asile inabidi ujue na ubadilishe mfumo wake wa kiuchumi. hivi kipi kilianza.., dini ilileta uchumi au uchumi ulileta dini?

  • Asanteni sana kwa kunipa uwanja nitoe mawazo yangu.Habari hii haina taarifa za awali ambazo zilileteleza hali ambayo waisilamu wakaanza kudai haki yao ya kuchinja.

    Huko tulikotoka, waislamu na wakristu tumeishi kwa amani na ushirikiano wa hali ya juu, nakumbuka kijijini kwetu (Busimbe-Bikoba) tulikuwa na mchinjaji kwa jina Suleimani,bahati nzuri bado yu hai na anaendelea kuchinja mpaka leo, kwa mara ya mwisho mimi mwaenyewe nilimfuata kuchinja kwa ajili ya sherehe za upadirisho.

    Kuna tatizo hapa, tena kubwa, suruhu si mawazo ya mkuu wa mkoa na waziri Wasira (Serikali), ni juu ya wakristu na waislam wenyewe. Wakristu tunajua butcher asilimia 80 za waislam, tumenunua nyama katika hizi butcher mpaka leo hii, kwa nini mtu anataka kuleta uchonganishi. Ikiwa serikali itaingilia maswala haya pasipo uhangalifu itatupeleka katika madai mengi yasiyo ya msingi kama hospitali za waislam, kitongoji cha waislam, bomba la maji la waislam.

    Tusichezee amani yetu kwa kutoa matamko yanayotugawa

  • Haya yote yameletwa na serikali ya awamu hii…. ni hatari sana… nilishaona siku nyingi mahali tunaenda…. nasikia Mwanza leo wameanza kupigana……….. 11.02.2013

    Imefika mahali Watu wanaombea kura misikitini na makanisani… HATARI kubwa sana mbele yetu…..

    Tuwe wawazi… waislamu wamezidi sana kuwa na chokochoko…… wanachokitafuta ni hatari sana kwao…. Misikitini ndio agenda yao kwa sasa….

    MUNGU atuepushe na hili

  • Jamani hayo mambo yameanza lini tena tz, mbona tunakoelekea ni kubaya watanzania wenzangu.

    Suala la kuchinja myama kila mtu anaweza fanya kazi hiyo. Hii si nchi ya kiislam eti iendeshwe na SHARIA kwamba waislam tu ndo wanahaki hiyo eti imeandikwa katika kitabu chao. Vitu vingapi vimeandikwa humo havitekelezwi ipasavyo ije kuwa kuchinja. Vitu vya muhimu vimeandikwa katika BIBLIA kwa mafundisho na makanyo na sio jinsi ya kuchinja. Sisi sote ni ndugu kwani tumeubwa na Mungu mmoja so tuishi kwa amani.

    Mie nitakula tu nyama iwe kachinja Muislam au Christian ewala.

  • @Msafiri

    Asante sana kwa comment yako umenielimisha hata mimi,watu wengi wametoa comments zao kwa ubishi wa dini bila ya kuelimishana

    Kwa ufupi "Ahalal Kitab" wale waliopewa vitabu yaani Manasara "wakristo"-Injili,waislam-kuran,Mayahudi-Zaburi hawa kama watachinja kile kilichonchinjwa waislam wanaruhusiwa kula sasa tatizo liko wapi

    Hivi hawa masheik na maimamu kweli wameshindwa kuwaeleza watanzania hao mpaka hali imefikia hivi ilivyo fikia

    • Mheshimiwa huijuwi Tanzania , elewa nchi yetu siyo ya Waislam tu , kuna Wakristo na dini nyingine , Pia mashekhe na Maimamu ni viongozi wa waislam elewa hilo , bila kusahau kwa Quran ni kitabu kitakatifu kwa Waislam ,na SIYO KITABU CHA  UKRISTO, Nayaliyomo ndani ya Quran ni kwa ajili ya Uislam na Waislam , nasiyo kwa Wakristo, kwa hiyo kama ilivyo kwa muislam kula nyama iliyochinjwa na Muislam, NA PIA MKRISTO ANATAKA KULA NYAMA ILIYOCHINJWA KIKRISTO NA SIYO MTU MWINGINE,NA HII NI HAKI YA KIKATIBU NA HAKI YA BINADAMU ,NA PIA ITAKUWA SI HAKI KWA MKRISTO KUMHUZIYA MUISLAM NYAMA ALICHINJWA KIKRISTO,HIVYO HIVYO PIA KWA MUISLAM KUMHUZIYA MKRISTO NYAMA ALICHINJA KIISLAM ,itakuwa vizuri sana kueshimiana imani zetu bila kuingiliana , sisi zote ni Watanzania

  • Tulipofika ni pabaya mno na tunapoelekea ni pabaya zaidi, nashauri tukiweza turudi tulipotoka. Tunaelekea kuanza kugawa huduma za jamii zote za serikali na za binafsi hasa zinazohusiana na utoaji wa huduma ya chakula kama mashule, hospitali, magereza, vyuo n.k. Kwa sababu kila mmoja atataka kujua nyama imenunuliwa au inanunuliwa bucha gani au kila mtoa huduma hiyo aeleze waziwazi msimamo wake.

    Mahusiano mazuri yaliyojengeka kwa muda mrefu kifamilia sasa yanapotea hatutakaribishana tena na kula pamoja kwa uhuru. Hali hiyo haitakuwa tu na athari za kijamii bali na za kiuchumi na hivyo kuturudisha nyuma miaka kadhaa hadi pale tutakapokuwa na miundombinu ya kulitosheleza taifa kukidhi mahitaji ya kila dini. Waliolianzisha jambo hili waliangalie tena kwa makini kwa maslahi ya pamoja.

  • mimi nadhani uchinjaji unatakiwakufanywa na serikali bali sii waislamu wala wakristo. yaani kwa kufuata taratitu za wataalamu wa mifugo. pia  nadhani hakuna aliye na haki juu ya mwingine  ,wote tu watanania na sote ni sawa

     

  • Yapo makundi matatu mpaka sasa:
    1) Watakaokula nyama iliyochinjwa na Muislam Au Mkristo
    2) Mkristo anayetaka nyama iliyochinjwa na Mkristo
    3) Muislam anayetaka nyama iliyochinjwa na Muislam. Sasa wote ni Watanzania, Wote tumeumbwa na Mungu na kimsingi Mungu anatupenda wote, aliyehukumiwa tayari ni shetani.

    Ili nchi iendelee utawala wa demokrasia, haki na maendeleo ni muhimu. Kwa hiyo tusifikie kupigana na kumwaga damu. Hakuna aliye ni Mtanzania zaidi au aliyeumbwa na Mungu akapendelewa zaidi. Sasa naishauri serekali kwa kuzingatia haki, uhuru, na demokrasia na pia ziko nchi yingi zenye Wakristo na Waislam na wamefanikiwa kutatua tatizo kama hili kwa amani.

    Nashauri
    1) Serekali iwe na bucha zake na wachinjaji wachinje tu bila kutamka maneno ya dini yake, yeye awe na kazi kuchinja. Hapo watu watakuwepo walio huru kula nyama wakiwemo Wakristo, Waislam, Wahindu, Washinto na Wapagani ambao hawajaingizwa kwenye mjadala huu.
    2) Wakristo wawe na Mabucha yao yaandikwe YESU NI BWANA au BUCHA YA KIKRISTO, HII ITAWEZESHA MKRISTO ASIYETAKA NYAMA ILIYOCHINJWA NA ASIYE MKRISTO AWE NA PA KUPATA KITOWEO KWA UHURU KABISA
    3) WAISLAM wao pia wawe na bucha zao ili Muislamu asiyetaka NYAMA ILIYOCHINJWA NA ASIYE MUISLAMU APATE PA KUPATA KITOWEO. kAMA wengi walivyopendekeza mabucha hayo yanaweza kuandikwa HILAL, AU BISMILLAH AU MTUME MUHAMAD JINA LOLOTE LITAKALOSAIDIA KUWA HAPO IPO NYAMA INAYOKUBALIKA NA WAISLAMU.
    4) Nawaomba viongozi wa dini zote wawe wakomavu na wawaelimishe waamini wao kuwa na uwezo wa kuvumiliana na kuyatatua matatizo mezani sio kwa mapanga, majambia na bunduki. Tukifika hapo tujue ni shetani anafanya uchochezi ili aongeze watu kwenye ufalme wake na apate damu ya kunywa pia shetani kwa kutumia roho 3 atawachochea viongozi wa dunia wapigane pale Har magedoni
    5. Nawaomba Maaskofu wakuu watangaze makanisani mote tutumie silaha ya maombi ya kufunga nakuomba kila jumamosi na jumapili ya mwisho wa mwezi – Mungu aiponye Tanzania

    6. Nawaomba Watanzania wenzangu wa dini zote , makabila yote, rangi zote TUJIZOEZE KUTATUA MATATIZO YOTE KWA KUTUMIA MEZA.

    Mimi ni Mtanzania mwenzenu, MVUMILIVU SANA KATIKA KUITAFUTA AMANI, NIMEOKOKA, sitaki neno la Bwana Yesu lidondoke chini. Bwana Yesu wewe unayetusikia daima ibariki Tanzania.Wabariki viongozi wetu. Amen.

  • Mimi siungi mkono tamko la Maaskofu hawa. Ni vema wakatambua vita vyetu si juu ya damu na nyama, vita vyetu ni katika ulimwengu wa Roho.

    Lazima viongozi wa Kikristo tuwe wakweli tatizo sio Muislamu kuchinja, bali tatizo ni Tamko la Viongozi wa Serikali kutamka kwamba Watu flani ndio wanahaki ya kuchinja. Miaka yote Wakristo tumekuwa tukichinjiwa na Waislamu si kwasababu wanahaki ya kuchinja bali ni kudumisha Undugu na Urafiki zaidi. Serikali haina Dini wala Haina tamko lolote lilosahihi kwamba kuna dini au dhehebu fulani lenye mamlaka ya kuchinja.

    Lakini nawalaumu sana Viongozi wenzangu wa Kikristo kwa kulichukulia jambo hili kanakwamba linatuharibia au kutupa hasara yoyote Kiroho. Ni vema wakaelewa kuongoza Binadamu ni ngumu sana, na Mtu mzima akikosea katika tamko wewe uliye wa Imani mrejeze kwa upole wala usimtake mpaka aombe msamaha kwenye vyombo vya habari, Viongozi wengine wakinyamaza kimya ndio tayari wamejua walikosea wapi.

    Fanyeni kazi ya Mungu acheni malumbano yasiyo na maana, Hubirini Neno la Mungu. Muda umekwisha Yesu yuko karibu kurudi, miaka yote mmekula nyama ambazo hamjui zimechinjwa je. Fanyeni kazi ya Mungu watumishi wa Mungu nawaomba acheni maneno wala malumbano.

  • DHEHEBU

    Mimi ni mkristo,mkatholic, Lakini katika ukoo wetu kuna Wakatolic,Waislamu, walokole wa madhehebu mbalimbali na maoni yangu ni haya

    MAONI

    nyama nzuri ni ile iliyopikwa vizuri, ikaiva, imetoka katika mnyama aliyehainishwa ama kuhalalishwa kuliwa na watu na mara itokeapo akaletwa katika meza kama kitoweo asiwepo wa kuuliza swali juu ya oooh mnyama gani, oooh nani kachinja. kwa maana kisicholiwa na watu wa imani fulani basi mwenye kaya inabidi aseme kinagaubaga kwa wageni wake ili wajue kama wanashiriki ama hawashiriki na ndiyo ilivyokuwa

    IPI DINI NZURI

    Dini nzuri ni ile inayothamini utu, uvumilivu, uthamini wa imani ya mwenzake, isiyo na inayoamini kwamba binadamu wote ni sawa na wanahaki ya kuabudu, pasipo kejeli. hapa sasa ndipo mambo yanapoharibika

    Tafsiri za vitabu vitakatifu imeingiliwa! Ki ukweli. wale wanaopewa dhamana ya kuvitafsiri wanavichukua tu kama mtu amayesoma GAZETI LA RISASI, kwamba kakuta tu picha ya msanii anaanza ku- COMMENT! Angalia sana hapa.PHILOSOPHY inabadilika, yaliyotokea enzi za Musa siyo ya leo! imani ni itikadi, hujui mtu anapenda vipi dini yake na yuko tayari kuitetea. ukikuta mvumilivu kama mimi nitakaa kimia alafu nitakutazama,hilo langu ni jibu tosha juu ya mtazamo wako wa upotoshwaji ama upotohaji unaofanya kwangu abudu hata chini ya mbuyu siwezi kukuuliza maana sijakutana na mungu hata siku moja akaniambia dini halali. tatizo ni kuchinja tu!!! mimi sijakubaliana, kuna jingine. Tumekula nyama waliochinja waislamu hata hatujakinaika, ndiyo kusema baadhi ya madhehebu wana allege na imani ya watu wengine? Katika dunia hii huwezi jitosheleza mwenyewe lazima umtegemee na jirani. utafiwa, utauguliwa, utapata harusi, je ni wakati muafaka wa kuacha kuzikana kama tulivyozowea? kusalimiana kama kawaida yetu?

    MWISHO

    Hii siyo Tanzania ninayoifahamu kuna mtu, kitu kinaivuruga/ wanaivuruga kwa maslahi yao je, wajua tone moja la amira laweza chachua donge late? wote toeni macho maana tukimaliza waislamu tutarudi; na wewe ni Mkatholic, msabato. pentecoste,muanglikana. hakuna kupona visu, mapanga, majambi! Kwani unabishi nini yale ya Ireland ya kaskzini yanatofauti gani na niyasemayo? Lord's resistant amarmy Uganda si yana uelekeo huo?

    waislamu wakimaliza wakristo wanaanza kutazamana alafu wanaambizana; wewe si mshia weye, ala ila wewe ni msunni, ooh baathi n.k Nina ushahidi bwan Ya Wataleban je?

    hakuna aliyezaliwa akawa na imani yake aliyoanzisha mwenyewe akiwa mtu mzima labda wachache mno walio slim ama kubatizwa wakiwa watu wazima! wengine tumerithi imani za wazazi wetu tu!

    UTANDAWAZI

    Hebu tazama usiishi kama uko Saudi Arabia kwenye uislam tu na dini nyingine nyongeza ama uko Uingereza kwenye ukristo tu na dini nyingine nyongeza. Vumilianeni, bado mnahitajiana kwa asilimia 99. Tena kwa nchi zenyewe maskini hivi, mtu unaomba mpaka kiberiti kwa jirani wa dini tofauti kabisa. watoto wote wa kiislamu na kikristo wanakaa kwenye mawe, zao kafaulu  div 3,4 na 0 ni za kufikia div. 1 na 2 ni anasa! ha ha

    Tena kwa wanaotoka katika familia bora wakati sisi tumetoka zetu njaronga huko kigoma hatujui kuvaa hata viatu, tukaruka na 1 za point 7. A nyingine unawaachia wasahihishaji na waziri wao. leo mko busy na kuchinja, mtoto kaenda shule ama la atajijua wewe ili mradi umezaa. kwa nini asijiingize kwenye makundi ya wabishi wa dini mpaka kuua? ndiyo, sasa kama 240,000 wana zero unafikiria nini? sasa ni bora kuliko siku ile akikamata hiyo AK 47 akakudai urithi ukingali hai!!

    Nadhani sasa ni muda wa kukaa na kutafuta adui yetu. Yupo mahali lazima tuna matatizo mengi sana tanzania moja wapo likiwa kuanguka kwa elimu

    walianza walimu kugoma, Yes, siku nyingi sana! alafu wakafuata watoto kugoma! ndiyo sasa utafaulu vipi wakati hata daftari haufunui kutwa kijiweni na kwenye vibanda umiza kutazama jack-chan wengine hawajui kuandika wanaandika majina yao kwa herufi kubwa na ndogo, muulize mchezaji wa mpira anfahamu mpaka wako wangapi kwao, ma file yalisha jaa hakuna space for colonial economy. Alafu wazazi nao wakagoma. sasa je? si walianza kuandamana na watoo kwenda kumsuta mwalimu anayetoa adhabu kwa mtoto mtukutu badala ya kushirikiana? siku hizi watoto kule mashuleni! da ule wala siyo usharobaro Ngwea naomba tu utafute msamiati.

    Tafuteni mambo ya kujadili bwana na yaliyopita yaonekane kama bahati mbaya tu.Ama tu employ ARMY da hapana bwana nimekosea hata mimi sitoweza kuandika haya maana nafahamu nitakuwa na ekari 2 kijijini. Maana katiba ya coup de' tal huwa ni declaratory na ni jinsi kiongozi wa kijeshi anavyoamka ndivyo inavyokuwa kwa siku hiyo.

    Wa TZ tunapendana sana

    Kalenza Sospeter.

    aka DIPLOMAT

    LLB

    ST.AUGUSTINE UNIVERSITY OF TANZANIA

    [email protected]

  • UMOJA NI NGUVU, UTENGANO NI UDHAIFU!

    Namshukuru Mungu kuwa kwa neema zake suala hili limepata ufumbuzi na sifikiri kama yanaweza kutokea tena masuala yoyote yenye kupingana na msemo wa waenga wetu ambao bila shaka kila mmoja wetu anaujua na kuutumia sana. Nimeuandika hapo juu ili mwenye kujisahau, akisoma hapo atafakari kwa undani fikra na matendo yake juu ya nchi yetu, Tanzania.

    Mimi ni Mkristo Mkatoliki, lakini natambua wazi kuwa ukatoliki wangu haunifanyi kuwa Mtanzania, ni Mtanzania kwa sababu nimezaliwa na Watanzania. Na niko huru kuwa Mkristo, kuyaamini, kuyaheshimu na kuyatii ya kikristo. Na pia kuyaheshimu ya imani nyingine za watanzania wenzangu.

    Hata hivyo katika yote, mimi kama msomi, bado ninayo nafasi ya kuyaangalia kwa jicho pevu yale yote ya pande zote bila kumhathiri yeyote.

    Ni wazi kila imani iko na kitabu Kitakatifu. Na pia iko na MAPOKEO yake ambayo kwayo, inasimama na kujiimarisha. Hata hivyo, yale yaliyoandikwa katika vitabu hivyo na yale yaliyo katika Mapokeo, sharti yafuatwe kwa kuzingatia tafsiri sahihi, jambo ambalo linahitaji UWELEDI wa hali ya juu kuyaelewa Maandiko Matakatifu siyo kwa nguvu za kibinadamu, bali kwa nguvu na mwanga wa yule tunaye mwamini.

    Kuhusiana na suala hili, naomba nitoe mfano mmoja tu unaoweza kutuonesha ni kwa vipi kutokuyaelewa vizuri maana ya Maandiko Matakatifu na Mapokeo ya kiimani, kunavyoweza kusababisha hatari kubwa, kama walivyoelezee wachangiaji wengi. Mfano ni huu:

    “Kijana mmoja aliishi na babu yake tangu akiwa na umri mdogo sana. Familia hiyo ilikuwa inaishi na kutii imani fulani ambayo babu wa kijana ndiye aliyeisimamia katika familia na kuongoza taratibu zote za ibada zao za kila siku…..”

    “…. kama walivyo watu wengi, babu huyo alikuwa mfugaji wa wanyama tofauti na kati ya hao, alikuwemo PAKA. Kila mtu anajua ni kwa jinsi gani paka wa kufugwa huwa karibu sana na mmiliki wake. Basi pamoja na urafiki huo kati ya babu na paka wake, bado paka huyo alionekana kusababisha USUMBUFU MKUBWA wakati wa IBADA kwa kulia lia …nyaaaau….nyaauu…. na kumpandapanda babu…rafiki yake….”

    “…. katika kutafuta utulivu wa ibada ndani ya familia, babu aliamua kuwa ANAMFUNIKIA KWENYE KIKAPU HUYO PAKA kila muda wa ibada ulipokuwa unafika.”

    “Sasa yalikuwa ni mazoea na yule kijana tangu akiwa mdogo alikua akiona babu yake akimfunikia paka kwenye kikapu kila kabla ya kuanza kusali na kumfunulia baada ya kusali…”

    “…. unajua nini sasa….? Kijana hakuwahi kuuliza kwa nini, bali yeye alikua akawa mtu mzima na akaendelea kufikiri kuwa KUMFUNIKIA PAKA KWENYE KIKAPU kabla ya kusali na KUMFUNUA baada ya kusali ni SEHEMU YA IBADA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
    Kwa hiyo akakifanya hicho kitendo kwa heshima yote hata baada ya babu yake kufariki….”

    “…. baada ya miaka mingi, naye akiwa sasa mtu mzima zaidi, yule paka akazeeka akafa…. na kilichotokea ni kwamba, huyu kijana … amabaye sasa alikuwa mtu mzima…. akashoindwa la kufanya…. kusali AKAACHA kwa sababu HAKUNA PAKA…. kumtafuta paka mwingine akashindwa kwa sababu hajui ni PAKA YUPI hasa anahitajika kwa ibada…….Kwa hiyo familia yake ikaacha kusali kabisa na imani yao ikapote!!!!!!!!!!!!!!!!”

    Kati ya maswali mengi ya kujiuliza, JE, NI KWELI PAKA ALIKUWA SEHEMU YA IBADA?
    Jiulize maswali mengi na ujijibu kutoka na adithi hiyo.

    Lakini pia, mfano mwingine ni hai kwa namna yake,

    Kwa wanajiografia, na watu wengine wenye uweledi katika nyanja hiyo, na wengine ambao wamewahi kuona aou kutembelea maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati, hawawezi kushangaa aina ya mavazi yanayovaliwa huko bila kujali imani fulani. Kama kuna ambaye kwa bahati mbaya hajui, basi kwa ufupi tu, ni kwamba maeneo yale kwa hali ya aina yake yameathiriwa na ukame, ni majangwa mengi, vumbi jingi, na wakati mwingine baridi jingi, n.k. kutokana na geografia ya eneo moja na lingine.

    Kwa mantiki hiyo, na aina ya uvaaji inatakiwa kukidhi mahitaji ya afya za watu wa maeneo yale. Tunajua kuwa imani nyingi zenye kujiheshimu na kuheshimika husisistiza mavazi ya heshima pia. Lakini je, ni sehemu ya imani ulimwenguni kote kuvaa mtindo ambao unashangaza na kutia wasiwasi jamii inayokuzunguka? Mfano hapa Dar es Salaam, kwa hali ya joto kali tunalolishuhudi na kulihisi, kweli hata Myahudi akishuka hapa, si analazimika kutafuta tu mavazi yanayoendana na mazingira na hali ya hewa ya hapa? Na ni mara ngapi imeshuhudiwa kuwa watu fulani huvaa mavazi fulani ili watu tufikiri ni waamini wa imani fulani, lakini mwisho wa siku sisi wenyewe ndo tunajikuta hatarini kwa kuyaamini hayo?

    Wito wangu ni kwamba, tujifunze vizuri na kuyaelewa vizuri matakwa ya imani zetu na kuyaishi bila kuvunja au kuhatarisha AMANI ya nchi yetu.

    Watanzania tuko na mambo mengi ya kupigana nayo, umasikini uliotopea vijijini na mijini, uhuru wa kweli, amani ya kweli, elimu imara, huduma bora hospitalini, uchumi imara, magonjwa hatari, siasa chafu, nk. Hebu tutumie mioyo yetu, nguvu zetu, akili zetu zote kupigana vita dhidi ya haya mapungufu tuliyonayo kuliko vita ya shibe ambayo kwayo tumbo kamwe halirithiki!

    Nakushukuru kwa kuchukua muda kusoma maoni yangu.

    Tanzania Nchi yetu, Wajibu wangu, Taifa kwanza.

  • Vita hii haitaishia hapa kama hatutarudi nyuma na kujua chanzo cha uchinjaji katika bucha zetu.

    Waasisi wetu marehemu Julius Kambarage Nyerere na Raisi wa Zanzibar Abedi Amani Karume waliona mbali sana na wakafanya uamuzi mzuri sana kwa vizao vyote kwa kuepusha shari.

    Wakristo bibilia inasema vyote ni halali na mle na mnywe hakuna mahali bibiia inazungumzia namna ya kuchinja mnyama. Kwa waislamu hiyo ni tofauti kuna namna ya kuchinja.

    Kwa kuondoa huu utata na kuleta upendo kati ya watanzania kuwa nyama ichinjwe na mwislamu mwenye masharti na iliwe pia na mkristo ambaye hana masharti.

    Wakristo hawakukatazwa kuchinja majumbani mwao lakini kama unaona sherehe au chakula chako unataka kumkaribisha mwislamu basi waliwatafuta waislamu au mwislamu wa karibu akasaidia kuchinja ili kile chakula kiliwe na wote.

    Huu ulikuwa ni upendo ulipita upeo wakristo na waislamu kukaa pamoja kula pamoja kuoleana, kuzikana na kadhalika.

    Hili la sasa nani achinje sijui limetoka wapi labda ni swala la AJIRA wenye kumiliki mabucha wanataka kuajiri ndugu zao labda hawa wenye mabucha ni wakristo na wanataka wao ndio wachinje nyama ya wote hii haitawezekana ni uadui tayari upendo hautakuwepo tena.

    Tutafute kiini tujue ni sababu gani hili jambo limeibuka.Maaskofu walitakiwa kuzima moto na siyo kuwasha moto kwa kusema wakristo wasinunue nyama zilizochinjwa na waislamu ni kuanzisha ugomvi na uhasama mkubwa.

    Hawataishia hapo kwenye uchinjaji chukua mfano nyumba ya mwislamu imeoa mkristo au nyumba ya mkristo imeoa kwa mwislamu nini kitafanyika baada ya hili la nyama.

    Mpasuko kwenye jamii uaanza, kuoa kwa waislamu kutakoma aidha kuoa kwa wakristo kutakoma baada ya hapo ni nini kitafuta mashule mengi yatabadilishwa yawe ya uislamu pekee na ukrsto pekee nini baadaye mipaka na hatimaye mauaji na uharibifu wa mali.

    Mimi ningefikiri maaskofu wangetumia busara na amani wanayofundisha kuleta upendo makanisani kwenye jambo hili na siyo kuzidi kuchochea mafuta ili moto uzidi kuwaka.

    Tujifunze kwa wenzetu wa mataifa yenye waislamu na wakristo wanaogombana kila siku kama Palestina na Israeli au Naigeria na Sudani jee watanzania mnataka tufike huko.

    Bucha na wachinjaji waachiwe waislamu, aidha bucha ziwe za wakristo lakina wachinjaji wawe waislamu kwani kulikoni ,msiangalie faida tu angalieni na hasara ya kubadili mfumo huo ni mauaji mengi na uharibifu wa mali zaidi

    Rais Kikwete alikemea taifa na kusema waislamu na wakristo wabadilike hii ni kauli mbio tubadilike kwa kila kitu ambacho kinaonekana kinawasha moto wa udini

    Haukuwepo udini enzi za utawala wa mwalimu Nyerere kweli TUBADILIKE waacheni waislamu wachinje.

    Mungu ibariki Tanzania

  • Haya mambo kwa kweli yaangaliwe kwa undani sana, kwani mimi sidhani ukristo siku zote hawakuona nani anaepaswa kula nyama iliyochinjwa na asiyekuwa mkrito kwa muda wote huo, eti mpaka wamu hii ndio wanagundua hawapaswi. Kwa waislam ni haram kula nyama ya nguruwe na kilichochinjwa pasipo kutajwa jina la Muumba wa mbingu na ardhi.

    Hilo tamko la kanisa sidhani kama liko sawasawa kwani halitoki kwenye biblia kwa mtazamo wa mafundisho yao.

  • Kwani Kenya, Uganda, Afrika Kusini au nchi yoyote ambayo haiongozwi kidini, ila kuna Waislam na Wakristo wanatumia utaratibu upi wa kuchinja? Tanzania si kisiwa labda serikali ipate maoni kutoka serikali za nchi nyingine zenye watu wa imani kama za kwetu kuhusu uchinjaji, kwani wenye miiko ya uchinjaji wa nyama hapa tanzania baadhi husafiri nje ya nchi, je huko utaratibu wa nchi hizo ni sawa na wa tz? kwa nini tz tusielewane?

  • Haya ni matunda ya kuwepo vyama vya kisiasa vilivyosajiliwa kwa taratibu husika lakini matendo ya viongozi wa vyama hivyo ni ya kidinidini hadi bungeni, Na pengine ni matokeo wa vyama vya kisiasa visivyo vya kidini lakini washirika wao wakubwa na vyama rafiki kwao ni vyama vya kidini vya nje ya nchi, kwa mfano CHristiAn DEMocrAtic union cha nchini Ujerumani ni moja ya vyama vya kidini vyenye mafungamano na vyama vyetu vya kisiasa nchini.

    Vyama vya aina hii ni rahisi kubeba agenda zao za kidini na madai ya wanaotaka kuchinja kwao hiyo ndio kilio cha nguvu ya umma itakayoenda kuwapa madaraka ya nchi na watu wa imani zingine kwao ni kama hawajawahi kuwa na malalamiko ya kiimani.

  • Waongo wanakula njama iliyochindwa na waislam tatizo lilikuwa katiba ,zilikuwa mbinu za kuitisha serikali ili waislam wasipewe kadi na kujiunga OIC. Tutaendelea kuomba mpaka tutakapopata .HISTORIA huwa na tabia ya kujirudia utake usitake.  TANGANYIKA Hiyoooooo!!!!!!!!!!!kama vile Congo Brazzavilleeee!!!!!!!!

    Sheherekea leo lakini ipo siku nasi tutasheherekea….hata hamsini ijayo………UMEMUONA KAGAME KUAMBIWA AONGEE NA WAHUTU ANAVYORUKA…….ANAIJUA TABIA YA HISTORIA…..

  • Waongo wanakula nyama iliyochinjwa na waislam tatizo lilikuwa katiba ,zilikuwa mbinu za kuitisha serikali ili waislam wasipewe kadhi na kujiunga OIC. Tutaendelea kuomba mpaka tutakapopata .HISTORIA huwa na tabia ya kujirudia utake usitake.  TANGANYIKA Hiyoooooo!!!!!!!!!!!kama vile Congo Brazzavilleeee!!!!!!!!

    Sheherekea leo lakini ipo siku nasi tutasheherekea….hata hamsini ijayo………UMEMUONA KAGAME KUAMBIWA AONGEE NA WAHUTU ANAVYORUKA…….ANAIJUA TABIA YA HISTORIA…..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *