Mabomu yalipuka Jeshini Dar es Salaam

Jamii Africa

mabomu-gongo-la-mbotoHALI ni mbaya katika eneo la Gongo la Mboto, kilometa chache kutoka Uwanja wa Kimataifa Ndege wa Julius Nyerere, baada ya mabomu kulipuka katika maghala ya silaha katika kikosi namba tano cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kilichopo katika eneo hilo usiku huu.

Habari za uhakika zinaeleza kwamba anga lote la kuzunguka Uwanja wa Ndege wa JNIA limefungwa kwa muda na hakuna ndege yoyote inaruhusiwa kupita eneo hilo ambalo nalo liko ndani ya kilometa kumi zilizotangazwa na JWTZ kama eneo la hatari.

Akizungumza kwa simu na Televisheni ya Taifa (TBC1), Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo amesema:

“Hali ni mbaya Kikosi namba tano maghala yamelipuka ni hatari, watu wahame, maghala yako karibu karibu sana, tunaomba wananchi wahame sasa hivi, tunajitahidi kuzuia moto unaotokana na hilo unaweza kwenda mbali sana hadi Kilomota kumi, wananchi walioko karibu na maghala ya kikosi Gongo la Mboto wasogee mbali sasa hivi.”

Wakati  Shimbo akitoa tamko hilo, hali imezidi kuwa mbaya katika maeneo yote yanayozunguka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere ambako watu wamekuwa wakikimbia na kutaharuki, baadhi wakijikuta wakipata ajali za barabarani.

“Njiani hali si nzuri magari kumekuwa na foleni na hali inatarajiwa kuwa mbaya baada ya kuwapo taarifa za uporaji,” anaeleza shuhuda mmoja aliyekuwa akitokea Gongo la Mboto kupitia eneo la Uwanja wa Ndege.

Kwa mujibu wa mtandao wa JamiiForums mashuhuda wanasema:

1. Hali ni mbaya jijini Dar, nyumba zinabomoka, watu wanakimbia ovyo!

2. Barabara ya Nyerere haitembei (kama unafikiria kwenda uwanja wa ndege ahirisha mapema), magari yameingiliana watu wanakimbia ovyo mitaani na barabarani kulikimbia eneo la maafa.

3. Dalili zinaashiria mabomu ni mengi zaidi na milipuko itaongezeka, kuna uwezekano wa kupoteza raia na watumishi (wanajeshi) wengi kufuatia milipuko hii


5 Comments
  • hali kama hii ni mbaya,jeshi linatakiwa kuhamisha raia wote walio karibu na maghala

    • Jamani Poleni na mabomu ya Gongo La Mboto.Jamani mpaka sasa .wamekufa wangapi?Serikali iwajibike kugharimu na kufidia wahanga hao.

  • this is Absurd, damn this is how we are going the world that we have Bomb’s but we dont know how to store them or we lack the technology to avert a accidental disaster, Now soo many homes are misplaced, Children lost, We arnt ready for any disaster’s no safety precautions, no saftely screenings, no emergency siuation tactics, Common people.. lets pull ourselves together and make this a better home for all….

  • Yalitokea Mbagala tuakaambiwa hayatatokea tena. Leo yametokea Gongo la Mboto tunaambiwa ni ajali. Siku zijazo yanaweza kutokea Lugalo sijui tutaambiwa nini. Still hakuna aliyewajibika kwa tukio la Mbagala. Sijui hili litakuwaje. Something must be wrong with our system.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *