WATOTO wote watano waliozaliwa juzi katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma wamefariki usiku wa kuamkia jana.
Watoto hao wote watano walizaliwa salama na Sophia Mgaya (28) mkazi wa Ruhuwiko mjini hapa kwa kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma.
Mganga mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa Songea(HOMSO) Dkt. Benedict Ngaiza, alisema kuwa watoto hao wameishi kwa masaa kumi tu na kufariki dunia kutokana na kuzaliwa na uzito mdogo wa chini ya kilo moja.
Dkt. Ngaiza alibainisha kuwa watoto wote wanaozaliwa wakiwa na uzito mdogo wanakuwa na maisha mafupi, hata hivyo alisema hali ya mama wa watoto hao inaendelea vizuri ingawa bado amelezwa katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma akiendelea kupata matibabu..
Tukio ambalo halijawahi kutokea katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma limetokea Mei 24 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi huku mtoto wa kwanza akiwa na uzito wa gramu 730, wa pili 810, watatu 670, wanne 820 na watano gramu 430.
Kulingana na mganga huyo kati ya watoto hao waliozaliwa, watatu ni wa kiume na wawili ni wa kike na kwamba huu ulikuwa ni mzao wa pili kwa mwanamke huyo.
Alieleza kuwa katika mzao wa kwanza wa mama huyo alifanikiwa kujifungua mtoto mmoja na huu wa pili amebahatika kujifungua watoto hao watano ambao wote wamefariki dunia.
Pole sana dada yangu,mungu atakupa tu usijali. May your five twins rest in peace
Mpango wa Mungu wetu hauna mjadala,alipangalo yeye Mwanadamu hawezi kulipinga,tunatakiwa kushukuru kwa kila jambo.