Hadi kufikia Januari 2018, Deni la taifa la nchi ya Uingereza lilikuwa limefikia dola za Marekani 2.5 trilioni, Japani dola trilioni 9.5, China dola trilioni 4.6, Marekani yenyewe dola trilioni 20 na India deni lake la taifa ni takribani dola trilioni 1.1, hii ni kwa mujibu wa tovuti ya www.nationaldebtclocks.org.
Haya ni mataifa makubwa duniani na kulingana na data hizi ni ushahidi kwamba yote yana madeni ya Taifa (national Debt) ambayo ni makubwa sana. Na ili kukukumbusha tu ni kwamba trilioni ina sifuri 12 hivyo viwango hivyo vya pesa hapo juu sio vidogo.
Mara nyingi huwa tunasikia kuhusu madeni makubwa ya nchi mbalimbali kila wakati kwenye taarifa za habari, na huwa tunajiuliza takwimu za madeni hayo ni kubwa kiasi gani?. Pamoja na hayo, Je, umewahi kujiuliza mataifa hayo makubwa duniani huwa yanakopa kwenye nchi gani?. Ni nchi gani huwa zinakopesha nchi hizo ambazo tayari zipo kwenye madeni makubwa sana?.
Kuna vyanzo mbalimbali ambavyo nchi hupata fedha ambayo huongezeka kwenye deni lake:
Mikopo ya Serikali kutoka kwenye mali zake
Nchi inaweza kukopa kiasi fulani cha pesa kutoka kwenye taasisi zake yenyewe. Mfano Marekali, inamiliki takribani dola trilioni 5.6 kutoka kwenye vyombo vyake vya usalama ambapo kiasi hicho ni karibu asilimia 30 ya deni lake kwenye vyombo hivyo. Kwa maneno mepesi unaweza kusema asilimia 30 ya Deni la Taifa la Marekani lipo kwenye mali zinazomilikiwa na Serikali.
Kwanini Serikali ikope pesa kutoka kwenye taasisi zake?
Hili ni swali la kuvutia sana…
Hoja ni kwamba baadhi ya Taasisi za Serikali kama vile Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Utumishi na nyinginezo huingiza fedha nyingi sana zaidi ya kiwango wanachoweza kutumia. Hivyo badala ya kuzificha fedha hizo mchagoni, taasisi hizi hununua dhamana za serikali ya Marekali (T-bonds). Kwa namna hii huisaidia Serikali kukidhi matumizi yake na wao hupata faida kubwa kutoka kwenye riba ya pesa waliyokopesha. Huu ni ubunifu wa hali ya juu.
Mataifa ya kigeni.
Kama unavyoweza kufikiria kiwango fulani cha Deni la Taifa huwa ni kutoka kwenye nchi zingine (Kiwango hiki huwa ndio ‘Deni la watu’).
Mfano Marekani inadaiwa dola bilioni 1176.6 na China, dola bilioni 1084.1 na Japani, dola bilioni 328.7 na Ireland na kiwango kinacho fanana na hicho cha ni kutoka nchi zingine, (http://ticdata.treasury.gov/Publish/mfh.txt).
Je, Mataifa haya huikopeshaje Marekani?
Mkopo mara nyingi hutolewa kupitia dhamana za Marekani. Kinachofanyika ni kuwa nchi hizi hununua dhamana kutoka Marekani ambazo hujulikana kama T-bonds. Dhamana hizi huchukuliwa kama ‘Mali miminika’ ambazo mara nyingi huwa hazipotezi thamani yake (Isipokuwa kwenye majanga yasiyotabirika, kama lile la kiuchumi lililoikumba Marekani mwaka 2008).
Na wakati mwingine nchi jirani au marafiki huweza kutoa kiasi kikubwa cha fedha kuisaidia nchi nyingine. Hii pia hujumuishwa kwenye Deni la Taifa hapo baadaye.
Wananchi nao wana sehemu yao…
Hata wananchi wa nchi husika huikopesha Serikali fedha ambazo baadaye huingizwa kwenye Deni la Taifa.
Mtu mkubwa ambaye huikopesha Serikali fedha ni Watu. Deni la wananchi hushiriki kwa sehemu kubwa kuongeza Deni la Taifa. Kama ilivyo kwa nchi za kigeni, wananchi nao hununua dhamana zitolewazo na Serikali na hii ni kama kuikopesha Serikali fedha.
Watu wengi wanataka kuikopesha Serikali fedha kwasababu wanajua kwamba pesa zao zinarudi pamoja na kiwango kikubwa cha riba.
Umeshawahi kusikia mikopo ya pande mbili? Fedha za mikopo hii mara nyingi huwekezwa kama madeni mengi au kwenye dhamana zenye kipato cha kudumu kama vile, vyombo vya usalama na ulinzi. Fedha hizi huwa na kiwango maalumu cha riba na huonekana kuwa ‘uwekezaji salama’ kwasababu hufanyika ndani ya Serikali.
Hivyo ukiwekeza kwenye mikopo ya pande mbili, ni kwamba unaikopesha Serikali fedha.
Hata hivyo, haya ni maelezo mafupi tu kuhusu vyanzo mbalimbali vya Deni la Taifa katika nchi zilizoendelea duniani; kiuhalisia deni la taifa ni dhana tata isiyoeleweka, likiwa na maelfu ya wachangiaji. Nchi hukopa fedha kutoka sehemu mbalimbali ili kukidhi mahitaji yake, ambayo mara nyingi hulenga katika kukuza uchumi wake na wa wananchi wake.