Ruvuma: Wanafunzi zaidi ya 500 wanasomea katika vibanda vya nyasi

Jamii Africa

WANAFUNZI wa shule tatu za msingi zaidi ya 500 katika kata ya Rwinga wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wanasomea kwenye madarasa yaliojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi.

Uchunguzi uliofanywa katika shule tatu kati ya saba zilizopo kwenye kata hiyo ambayo ipo mjini Namtumbo umebaini kuwa  katika shule ya msingi Rwinga wanafunzi  296  wanasomea kwenye vibanda vya miti vilivyoezekwa kwa nyasi .

Mwalimu wa taaluma katika shule hiyo Onesmo Mbawala alisema idadi kubwa ya wanafunzi katika shule hiyo wanasomea katika vibanda vya nyasi kutokana na shule hiyo kuwa na upungufu wa vyumba 12 vya kusomea ambapo vyumba vilivyopo ni vinne tu na kwamba shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1975 ina jumla ya wanafunzi 592.

wanafunzi-rwinga-school

Wanafunzi wa darasa la awali wapatao 92 shule ya msingi Rwinga wilayani Namtumbo wakiwa darasani na mwalimu wao

Katika shule ya msingi Selous jumla ya wanafunzi 108 wa madarasa ya tano na sita wanasoma kwenye vibanda vya nyasi hali ambayo walimu wanasema inachangia kushusha taaluma kwa wanafunzi.

wanafunzi-selous-school

Wanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Selous wilayani Namtumbo wakiwa darasani

Mwalimu  wa taaluma katika shule hiyo Sheweji Simba  alisema shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007 ina jumla ya wanafunzi 477 huku ikiwa na vyumba vinne tu vya madarasa kati ya mahitaji ya vyumba nane hali ambayo imesababisha baadhi ya wanafunzi kusomea kwenye vibanda vya nyasi .

Katika shule ya msingi Mkapa ambayo imepewa jina la aliyewahi kuwa kiongozi mkuu wa nchi  Rais mstaafu Benjamin Mkapa pia kuna wanafunzi  wanaosomea kwenye vibanda viwili vya nyasi  kwa kuwa shule hiyo ina vyumba vinne tu kati ya mahitaji ya vyumba nane.

wanafunzi-mkapa-school

Wanafunzi wa shule ya msingi Mkapa wilayani Namtumbo wakiwa darasani na mwalimu wao

Mkuu wa shule hiyo Hans Mwailima alisema shule hiyo yenye wanafunzi 306 madarasa matatu yanasomea katika chumba kimoja  ambapo kuanzia darasa la tatu hadi la sita  wanasomea kwenye vibanda vya nyasi kwa zamu.

“Unajua wanafunzi wana tabia ya kutaniana hivyo endapo darasa moja wakisoma kwenye vibanda vya nyasi kila siku wenzao wanawatania hivyo kukata tamaa na wengine kuwa watoro hivyo tumeamua wote wawe wanasoma kwenye vibanda vya nyasi kwa zamu ili kujenga mvuto wa mazingira ya kusomea’’, alisema.

Mratibu elimu kata ya Rwinga Thomas Komba amekiri shule  tatu kati ya saba katika kata yake ambazo ni Rwinga, Mkapa na Selous wanafunzi kusomea katika vibanda vilivyojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi na kusisitiza kuwa shule za Minazini, Kidagulo, Migelegele na Mandepwende ndizo shule pekee katika kata hiyo ambazo hazina vyumba vya madarasa vilivyoezekwa kwa nyasi.

“Shule zangu  tatu za Rwinga,Mkapa na Selous katika kata yangu zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa hali ni mbaya tunafanya jitihada za kuhamasisha jamii ili waweze kujitolea kufyatua tofali kuzichoma kwa kushirikiana na serikali  ili kupata vyumba zaidi na kumaliza kero hii ya aibu’’, alisisitiza.

Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Kasimu Ntara alidai kuwa kuwa kuwepo kwa madarasa yaliojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi katika wilaya hiyo kunatokana na kuanzishwa shule nyingi za msingi.

“Mpango wa uboreshaji wa elimu ya msingi MEM nchini ulisababisha kuanzishwa kwa shule nyingi hivyo  baada ya kuondoka kwa MMEM serikali imeshindwa kumudu ujenzi wa vyumba vya madarasa jitihada zinaendelea kufanyika kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa’’, alisisitiza.

Habari hii imeandikwa na Albano Midelo, FikraPevu – Ruvuma

42 Comments
  • Miaka hamsini ua Uhuru sherehe ilikuwa ya nini sasa. Mijihela yote ile bado…….hali iko hivi. Nchi hii haifai.

  • Maskini Tanzania,hivi kweli hata hii buget ya kukimbiza mwenge nchi nzima isingetosha kuwapatia hawa watoto madawati?

    • Mkuu wacha hiyo budget ya mwenge je sherehe za muungano budget yake ilikuwa kiasi gani???? Hizo pesa sizingesogeza hata tukapata madara kama 50, kweli Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa kupanga ni kuchagua!!!!!

  • Is this a reflection of “MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA?”….the government on power should be accountable

  • Yaan tukiambiwa cc tuna mabupuru sio marais tunaona watu wanatufanyia masihara…Angalien mambo hayo. Yaani hii nchi yetu hata mtoto mdogo anaweza kuiendesha, au bora yeye anaweza akaiendesha vizuri kuliko huyo tunaemwita ni Rais. Coz hata mtoto mdogo nadhani ungempa mamlaka angeweza kulitatua hili kwanza kabla hata kugarimika na masherehe na maSemina yasio na tija kwa wananchi, isipokua kwa maslahi ya wachache.

  • Tena kwa ujinga wa viongozi wetu na wasivyokuwa na haya, huchukua picha hizi kwenda kupitishia bakuli. Hii nchi imelaaniwa, au viongozi wamefanya ilaaniwe.

  • chagua ccm kwa maisha bora
    maisha bora ndio haya kupeana ulaji kuuza rasilimali za nchi,kutenga mafungu makubwa ktk sherehe,matamasha,mavazi nk huku watoto wao wakisoma shule za kimataifa.kuna haja sasa kuamka watanzania kuachana na mfumo nyonyaji.tunalalamika hadi tuchukue hatua sasa

    • Mkuu, bahati mbaya hawa watu wa kusini licha ya maisha magumu waliyosababishiwa na ccm, ndiyo kwanza wanaikumbatia kwa juhudi zao zote.

  • Inashangaza wanajamii kusikia umasikini jirani na hifadhi ya Selous matatizo yote yanaweza kutatuliwa endapo tutarudi katika maadili Ndugu zangu viongazi wa ngazi za juu hili linawatia aibu msilale lishughulikieni haraka

  • Wala haishangazi!.Hilo ni moja tu kati ya maelfu ya maeneo hapa nchini yenye hali kama hiyo.TEMBEA UONE!! Huko ndipo CCM wanapopatia kura. Maeneo kama haya wasitarajie mapinduzi yoyote ya kielimu kwakuwa ndiyo maeneo yanayotoa na kuandaa zao tawaliwa la milele,zao bubu lisiloweza kuhoji chochote.

    Tabaka kandamizwa lisiloona wala kutambua. Tabaka linaloandaliwa kuviandaa vizazi na vizazi vya tabaka fanana lenye ubongo timamu usofanya kazi yake sawasawa, akili timamu isiyoweza pambanua, macho angavu yasoona, mikono na miguu kamili isoweza kunjuka na kureact. Ni maeneo teseka yenye faida kubwa kwa Utawala.

  • Maisha bora kwa kila Mtanzania, Rais anasafiri safari 400 nje ya nchi kwa muda wa miaka 6, utawala miaka 5, mwaka 1 U Vasco dagama.

  • Jamani lazima ifike mahali tuseme enough is enough! Watu kodi wnatoa, TRA wanakusanya hadi wanavunja rekodi then provision of social service ndo hivi! We must be wicked!!

  • Hii nchi inahitaji maombezi. Viongozi wetu hawajitambui, vipaumbele vya Taifa havijulikani na Wananchi hatujui wajibu na uwezo wetu dhidi ya Viongozi wanaotupoteza. Ee Mola itazame Tanzania, Watazame Watanzania….!

  • Inaonyesha mwamko wa elimu nchini, serikali ijitahidi kufikisha uduma hii muhimu kwa wanaoihitaji!.

  • Hayo ndiyo maisha bora kwa kila mtanzania wamejaribu wameweza na wanasonga mbele sasa sijajua kama hawa bado wanasonga nao mbele au wamewaacha nyuma

  • Masikitiko makubwa sana kwa serikali yetu,

    Kwa hakika watoto wana nyuso za furaha lakini kiuhalisia ni huzuni kubwa sana.

    By tume ya katiba

  • matatizo ni ye2 cc wnyw wapiga kura,watu hawajapata elimu ya kutosha khs upigaj kura,mambo haya kwa wenzetu kenya hayapo,km una umri wa kupiga kura haujafanya hivyo ni viboko tu maana wanajua ww ndie chanzo cha kutoleta mabadiliko!haya hayawez kwisha kwa upande we2 coz viongozi we2 wanajua hatuwez kuwafanya ki2,uchaguz ukifika wanajua watarudi tu,watanzania tunasikitisha sn.

  • Kwanza Lawama na ujinga ni za wapiga kura(watanzania) ambao tumeridhia na hali hii ya maisha tuliyo nayo, hivyo na kuiweka serikali madarakani kwa kuipigia kura. Mfano gharama za kuendeshea shughuli za wilaya zote za tanzania zingeweza kujenga shule nk. basi kwa nini serikali isibane matumizi yasiyo ya muhimu na kutafuta mbadala? tanzania ina zaidi ya wilaya 132, kila mkuu wa wilaya anapewa toyota landcruiser, tamani ya gari 1 ni Tsh 80,400,000 zidisha wlaya 132.

    KAZI KWENU WAPIGA KURA

  • “Unajua wanafunzi wakisomea kwenye vibanda vya nyasi hukata tamaa na wengine kuwa watoro’’ kwa mtaji huu wizara bado inatafuta mchawi wa matokeo mabaya???? jamani tuwe wazi hapa ni kwamba mpango wa serikali ni bora elimu kwa kila mtanzania. hata kama utaleta wazungu wafundishe kwa mazingira haya sina hakika kama wanafunzi watafaulu na hii ni kwa s/msingi ukigeuka upande wa pili s/ssecondary ndio balaaaaaaa! Nashauri serikali ibadili policy yake kuhusu elimu badala ya shule nyingi miundo mbinu hafifu + hakuna walimu basi iwe shule chache miundo mbinu mizuri + walimu wa kutosha.

  • Kwa kweli hali ni mbaya, tangu waanze kula, ni matrilioni mangapi? Hakuna anayefilisiwa tangu kesi zianze! Sioni nuru katika miaka mitatu ijayo kwa Chama Tawala

  • Lakini hawa watu wa Songea si ndio wale wale Capt. John Komba akiwaimbia ” WATANZANIA WOTE, WATANZANIA WAPUMBAZWA, WATANZANIA WOTE … WATANZANIA WATANZANIA WAPUMBAZWA. NAMBARI WANI.. NAMBARI WANI EEE, NAMBARI WANI NI CCM. WANGONI WOTE TIENI, TIENI, WOTE TIENI TIENI TIENI KWA MOYO MMOJAAAA NAMBARI WANI EEE.. NAMBARI WANI NI CCM..

    kisha wanamshangilia mgoni mwenzao; sasa leo wanalalamika nini ikiwa wanapenda uzalendo kwa kumfuhisha John Komba.

    MIZAMBWA
    INANIUMA SANA!!!

  • SErikali itumie Change ya RADA kuelekeza katika elimu kwa shule za vijijini ili vijana wetu wapate elimu bora kwa kuwawekea mazingira mazuri ya kusoma.

    MIZAMBWA
    INANIUMA SANA!!!

  • “Lakini hawa watu wa Songea si ndio wale wale Capt. John Komba akiwaimbia ” WATANZANIA WOTE, WATANZANIA WAPUMBAZWA, WATANZANIA WOTE … WATANZANIA WATANZANIA WAPUMBAZWA. NAMBARI WANI.. NAMBARI WANI EEE, NAMBARI WANI NI CCM. WANGONI WOTE TIENI, TIENI, WOTE TIENI TIENI TIENI KWA MOYO MMOJAAAA NAMBARI WANI EEE.. NAMBARI WANI NI CCM..”
    Nimeipenda hii yako MIZAMBWA; naikubali sana. Huko ndiko wanasema ccm ni baba ccm ni mama. Poleni sana.

  • Hamna wizi wala nini. Ni wivu wenu tu. Acheni wivu wa kike. Mwenye wivu ajinyonge. Maisha bora bado yaja.

  • Kazi ipo wajomba,kwa kila jambo huanza na antagonist clas so huu ndio muda wetu vijana kuleta changes ili ccm ife kifo cha natural death kwa maslahi ya taifa.

  • Marehemu Julius Kambarage Nyerere alipochukuwa nchi hii kwa wakoloni kama angekuwa mbinafsi kweli hatungekuwa pale aliptuacha na kuondoka mwaka 1999

    Nasema hivyo kwa sababu kama tukianza na elimu alijitahidi kujenga shule nyingi sana za msingi, sekondari , vyuo vya elimu, vyuo vya ufundi vyuo vikuu /Chuo kikuu Dar es salaam/chuo cha Ardhi, vyou vya elimu ya juu kama mzumbe, vyegezi nk

    Kwei nasema kwa uchungu akajitahidi kuwepo na Azimio la Arusha mwaka 1967 ili tuu kuhakukisha hakuna ufisadi katika utawala wake.

    Katika secta ya maji baada ya kurithi bwawa la nyumba ya Mungu aalijitahidi kujenga Mtera, Kdatu kuweka Umeme wa Gridi

    Katika secta ya madini alikataa kuchimba madini yaliendelea kuchimbwa ya mwadui mkataba uliokuwepo kabla ya uhuru.

    Alikataa kwasababu alijua sera za magharibi sers za trace passing sera za kuhamisha mali kwani hatuna vitendea kazi

    Lakini hebu baada ya kuondoka ni jambo gani jipya lililofanyika watanzania wenzangu dola ya marekani imeshuka tangu pale alipokufa kutoka mamia kwenda maelfu maana yake ni nini hakuna tena mazao hakuna tena pamba ya kupeleka nyingi , nchi inaagiza vitu vingi kuliko mauzo nje

    Mali asili zikaanza kuhamishwa, bustani ya bunge, wanyawa tausi, mikataba ya uvunaji wanyama Loliondo ,nk machimbo ya Gesi ambayo tulitarajia yangeinua uchumi kwa kuwasha umeme nchi nzima imekuwa ndoto

    Elimu ndiyo hii inaendelea kushuka madasara sasa yanaendelea kuwa ya nyasi baada ya miaka 50 ya Uhuru

    Hebu kila mtanzania ajiulize je hii ni vema inapendeza kuona matabaka baada ya kuvunjwa azimio la Arusha na kuanzisha Azimio la Zanzibar

    Hebu tufahamu muda wetu wa kuishi hapa duniani ni miaka 70 hebu tupendani tuache kulimbikiza mali ambazo hatuna kazi nazo tuache uchoyo .

    Kweli nasema kama Mwalimu Nyerere angekuwa mchoyo familia yake ingekuwa milionea ona baadhi ya watoto wake wamo upinzani haipendezi

    Hebu tubadilike kwani wakati mwalimu anaanzisha vyama vingi alisema kiongozi mzuri atatoka CCM sasa kwanini atoke CCM aende upinzani

    Kwanini viongozi tuliopewa dhamana ya kuongoza Taifa hili tusiwe kama Mwalimu Nyerere tubadilike ili tuwaamini viongozi waliopewa jukumu hilo

    Je kweli inaendelea kupendeza kuona baada ya nusu karne watoto wetu bado wanasomea kwenye nyumba za nyasi makuti na wachache wako kwenye shule za kulipia

    Naomba tuangalie hapa Songea kama mfano

  • ndugu yangu hii ni afadhali isiwepo hapo. Inatia uchungu sana kuiskia mdomo wa binadamu unaahidi maisha bora halafu watoto hawa wanasoma kwenye vibanda vya nyasi.
    Halafu mdomo huo huo unajisifu kuwa umeleta maendeleo. HAYA YA KUSOMEA KWENYE VIBANDA VYA NYASI? Yeyote anayesifia mtawala lazima naye anafaidika na kutawala kwao. Damn country.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *