KABLA YA KIFO, Kanumba alimuita mama yake Dar ili amuage

Jamii Africa

MAMA Mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mutegoa amezungumza na FikraPevu na kusema alizungumza na mwanae usiku, saa chache kabla ya kifo chake akimuita Dar es Salaam ali waagane.

Mama huyo, ambaye alikuwa safarini mkoani Kagera, anasema mwanae alimpigia simu akimtaka arudi Dar es salaam waagane kwani alikuwa na safari ya kwenda nchini Marekani.

Akihojiwa na FikraPevu leo mchana katika uwanja wa ndege wa Bukoba akiwa safarini kuelekea  Dar es salaam katika msiba wa mwanae, mzazi huyo alisema usiku wa tukio lililosababisha kifo, Kanumba alimpigia simu na kuongea naye.

Mama huyo mzaliwa wa kijiji cha Itoju kata ya Izigo wilaya ya Muleba Mkoani Kagera na ambaye huishi jijini Dar es salaam, alikuwa mkoani Kagera alikokua amekwenda kumtembelea mama yake ambaye ni bibi yake marehemu Steven Kanumba.

"Mwanangu niliongea naye usiku (Ijumaa Aprili 6, 2012) akiwa mwenye furaha na tulitaniana sana, alisema anatuma nauli nirudi Dar es salaam tuagane kwani alikuwa na safari ya kwenda nchini Marekani,"alisema mama yake Kanumba.

Alisema alipatwa na mshituko alfajiri yake kuambiwa kuwa mtoto wake alikuwa ameaga dunia. Anasema mwanae Kanumba alizaliwa Januari 8, 1984 katika hospitali ya serikali mjini Shinyanga.

Marehemu Steven Kanumba alifariki Usiku wa kuamkia Jumamosi, Aprili 6, 2012, baada ya kuanguka. Sababu za kifo chake hazijaelezwa wazi pamoja na kuwapo taarifa za kuwapo ugomvi kati yake na msichana Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu, ambaye pia ni msanii kijana. Lulu ambaye naye amekutwa na majeraha madogo, anashikiliwa na polisi kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo.

"Sina cha kuongea naomba mniombee katika kipindi hiki kigumu jana nimeongea naye kwenye simu leo naambiwa mwanangu amekufa," aliongeza katika hali ya majonzi

Kwa mujibu wa mzazi huyo Flora Mutegoa marehemu Kanumba ana baba yake mzazi aliyemtaja kwa jina la Charles Kanumba kuwa ni Msukuma mwenyeji wa Mkoa wa Shinyanga.

Alipoulizwa na FikraPevu kama mwanaye aliwahi kumweleza siri na ndoto zake za baadaye alisema alikuwa na matarajio ya kufika mbali zaidi katika sanaa ya uigizaji huku akiomba aachwe apumzike kwani maswali mengine asingeweza kuyajibu.

"Naomba mniombee hali yangu sio nzuri baba yake ni Msukuma mwenyeji wa mkoa wa Shinyanga, maswali mengine niacheni jamani," alisema.

Imeandika na Phinias Bashaya; FikraPevu – Kagera

36 Comments
 • Hata sisi wenyeji wa inchi ya DRC tunasikitishwa sana na kifo ca kijana KANUMBA. Mungu apokee roho yake. Duniani hapa, sisi wote ni wasafiri.
  Binafsi mimi naombeya mama na jamaa lote, kwani ni msiba usiyo easy kuvumilia. Vijana wenzangu hapa kwetu GOMA walizoweya kusema kwamba nilimfanana KANUMBA hata kwetu nyumbani. Kwa mjibu mimi niliwaeleza kwamba sisi wote viumbe vya mwenyezi Mungu. Basi, lakufanya ni kuhimiza Polisi ifanye kazi yake, na aliye chanzo ya kifo hiki aazibiwe kulingana na sheria za serkali ya Tanzania. Huyo dada Lulu, na wangineo nyumbani hapo wahojiwe accordingly kwani kuna sababu iliyo acha wanamwua ndugu yangu huyo.
  MUNGU awe karibu nanyinyi nyote.
  Johnson-BUTERA/GOMA-DRC

 • dah jaman watanzania pengo kubwa sana! hatuna la kufanya bwana! god kachukua kiumbe chake so tuzid kumwombea kijana na si tupo njia moja! wakati wowote kinaweza kuhappen! tusal sana! POLEN SANA WATANZANIA naPOLEN FAMILIA YA MAREHEMU KANUMBA MUNGU AWAPE UVUMILIVU!

 • Kila mtu atakufa muda wake ukifika. Kanumba ametangulia na wengine tutafuata. Cha msingi ni kutengeneza njia zetu kwa kutenda mema.

 • jaman me camin mtu adondoke tu afe?.lulu ana mambo ya ajabu anatembea na wajomba zake achukuliwe hatua haraka sana.

 • Nimesikitishwa na kifo hiki cha ghafla kwa kipenzi chetu Kanumba. Poleni sana wanafamilia na wazazi. Hatutakusahau maana umeacha mengi moyoni mwetu. Jamani kifo ni lazima. Umejitayarishaje? na je unaachia jamii yako nini? Utakumbukwa ukiondoka? fanya jambo jema la kuelimisha jamii kwa bidii kama Kanumba na utakumbukwa maana Mungu aweza kukuita saa na wakat wowote tengeneza maisha yako na Mungu wako sasa hasa ninyi vijana ili angalau uweze kufurahia maisha ya milele . Mungu wa Mbinguni aiweke Roho ya mareheu mahali pema peponi. Amina.

 • ni pigo kwetu sote, pole familia ya kanumba na wasanii wote, wote tumeguswa na msiba huu mkubwa, kifo umekuja mapema mno umemzuia kanumba kufikia dream zake alizokuwa nazo.

  R.I.P BRO, bwana aliyefufuka leo akufufue siku ya mwisho

 • Jamani Watanzania, huu msiba ni mkubwa sana kwetu, kumpoteza KANUMBAn= ni sawa na kuipoteza sanaa hapa Tanzania, ila hatuna jinsi iliyobaki tumuombee Kwa Mungu ili loho yake iwekwe mahali pema peponi. Na huyo LULU Jamani vyombo vya dola vimbane mpaka awatae hao waliomtuma kuifanya kazi hiyo isiyo yake. na shelia ichukuliwe kwa halaka sana.

 • Kifo cha Kanumba kimewagusa wengi watu wa rika na kada mbalimbali kwa sababu amekuwa na mchango mkubwa hapa duniani alitumia muda wake mwingi kuwaburudisha na kuwasilisha ujumbe wa maisha ya wanadamu kwa njia ya sanaa.

  Hakuna Bingwa atakayetembea kifua mbele kwamba yeye amezoea kifo,amezoea kufiwa,kifo hakina mwenyewe,kila ufiwapo unaona kama upo peke yako uliyekumbwa na tatizo hilo,kifo hakizoeleki.

  Mengi yametamkwa mazingira ya kifo cha Ndugu yetu Kanumba,lakini yote kwa yote Mungu amempenda zaidi baada ya kuona kazi aliyomtuma hapa duniani ameifanya kwa ukamilifu,yametimia ameenda kwa mleta na mtoa uzima.

  Mungu Ailaze Roho yake Mahala pema peponi amen.

 • Hata mimi pia ni mmoja kati ya watu walioguswa sana na kifo cha kanumba.Yote tumuachie mungu kwani yeye ni mweza wa kila alitakalo kulifanya.R.I.P STEVE

 • tangulia rafiki hatuna neno zuri zaidi ya kua tulikupenda sana mpendwa wetu steve.

 • Nimeguswa sana nikikumbuka flamu yake ya kimazingara waliipatia sana na mungu amuweke pema peponi, kutangulia ndio kugumu kila mtu atapita hapo

 • Lulu wewe ni shetani mwenye umbo la binaadamu!! umekuja kugharikisha dunia? wewe ni ibilisi usiye na haya. haya sasa umeshamtoa roho Kanumba furahi sasa. Unajidai utakunywa sumu kunywa ufutike ulimwenguni tumechona navituko vyako!!!

  • wacha kumuhukumu lulu, hakuna aliethibitisha kuwa kanumba kauawa na lulu au kasukumwa,mbona humlaumu kanumba kutembea na vitoto chini ya miaka 18??

   Hujui km ana kosa la kubaka?? walikuwa chumbani wanafanya umalaya wao, hivyo wote walikuwa ni malaya na kanumba kafa kwenye umalaya, Lulu ana makosa yake nae ya kufanya mapenzi akiwa chini ya miaka 18 na kukubali kufanywa na watu wakubwa kiumri kwake, lkn wote ni MALAYA TU.

 • Namuhurumia sana mama yako nadhani amejuta kukuzaa…. U- star siyo vituko mdogo wangu, ukiwa star mwenye heshima wengi watakuheshimu. Waswahili husema ngoma ikivuma sana haikawii kupasuka sasa hayo yamekufika. Hebu kunywa sumu uone utamu wa kutokwa na roho!!

 • Namuhurumia sana mama yako nadhani amejuta kukuzaa…. U- star siyo vituko mdogo wangu, ukiwa star mwenye heshima wengi watakuheshimu. Waswahili husema ngoma ikivuma sana haikawii kupasuka sasa hayo yamekufika. Hebu kunywa sumu uone utamu wa kutokwa na roho!!

 • Jamani jamani poleni sana nduguzangu wa tanzania kwamsiba huo,
  kwakweli kila nafsi itaonja umauti,
  kifo ca kanumba kinaskitisha mno kwasababu nica ghafla na watu kamahao huwa hawadumu, na huyo lulu asiseme uongo huwa alitumwa asemevizuri naye akamatiwe atuwa kwaharaka baada yakufanya tokeo ilo kwanini akimbie!!! alikifanya kwamakuskudi,ata samson aliwuwawaga na mkewe kwasababu ya pesa nahuyo utakuta alikubaliwa pesa. Namchukia sana lulu

 • we lulu kila mwaka una miaka 17 we miaka yako haisogei mwenzetu? nina mianka kama miwili nasikia unamiaka kumi na saba huna jipya.mala ya mwisho niliona umeandikwa kwenye gazeti kama una miaka 17 kwa nini unaenda club na kwa nini unaendesha gari na kwanini unafanya mambo ya ajabu yanayo kuzidi umri.ulijibu mwenyewe hiyo skendo kua umekua uachwe usifatiliwe maana umesha fikisha miaka ya kufanya hayo yote sasa yamekufika ya mauaji unarudisha miaka nyuma.mi naamini lulu anamiaka zaidi ya kumi na nane hayo mengine ni kujitetea wesema ukweli kama hujahusika na kifo chake ueleweke.umebakwa chumbani kwake ulikua unafata nini?na kwa nini hukukaa sebleni?huna utoto wewe mambo yako yalizidi hata uliyo yafanya.sema uongo kwa mwanadamu lkn Mungu anajua miaka yako na ulichomfanyia kanumba.

 • jamani msimlaumu lulu kwa kifo cha kanumba,hakuna anaeweza kuthibitisha kuwa marehemu alisukumwa na kanumba wakiwa chumbani,ila zaidi anaejuwa ni lulu pekee,kwa hiyo tusiwe kimbelembele kujifanya eti tuna uchungu mkubwa sana na marehemu na kutaka kumuhukumu lulu,chumbani walikuwa wawili tu na inajulikana km wale walikuwa wapenzi,km kulaumu pia mlaumuni na marehemu kufanya mapenzi na mtoto mdogo km yule ambae kisheria marehemu alikuwa anabaka,kwani hakufika miaka 18,kwa hiyo tusiwe tunajifanya eti tuna uchungu sana na kanumba kwa kuwa amefariki,tujaribu sana kuwa wawazi na tusiwe wanafik.

 • jamani kama tunaamin kuwa MWENYEZI MUNGU YUPO ninaiman ndo ataeamua kuhusu lulu na Bro kanumba, rest in peace bro, namhala

 • RIP Kanumba,msimhukumu lulu mapenzi hayaangalii umri wenyewe waliridhiana,tuwe wawazi tusiangalie upande mmoja.vp kama lulu angekufa mikononi mwa kanumba?

 • siku zako za kuishi zikifika kikomo utakufa tu.Kumbuka kila .afsi itaonja mauti,inapasa ujililie wewe na nafsi yako.

 • Du,kwa hali ya vurugu,utekaji nyara na mamboo mengine yanayoendelea Tanzania,haki ya nani akifufuka archtecture wa nchi hii,machozi lazima alie,ataanguka harafu atakufa mara ya pili,are we tired with peace in Tanzania?Sisi wengine bado tunaipenda nchi yetu na tunataka tuishi kwa amani na upendo,waliochoka na amani wahamie Syria kuna viwanja vya bure huko wanagawa,msituharibie nchi bwana.

 • watu wanomwona lulu muuaji, wajiulize je kama lulu ndio angekutwa amekufa, na ukichukulia ni mwanamke mwenye mwili mdohga je kanumba angetazamwaje na jamii. mi nadhani tuache kulaumu sidhani lulu ni muuaji, nadhani ni bahati mbaya tu inaweza kumtokea mtu yoyote. naskitika kusema kuwa mara nyingi wanawake wanaonekana ni malaya wahuni kuliko wanaume wanaofanya hivyo.watu waache kuchanganya maisha ya mtu na kifo na waache kuwatazama wanawake kama watu waovu kuliko wanaume. kiufupi wanawake wanafanya yote kwaajili ya wanaume hata kuweka makalio makubwa kuvaa nusu uchi, kukuza makalio, kujichubua wanafanya haya kwasababu ya wanaume,lulu anamatatizo yake kama binadamu lakini haipelekei yeye kuonekana kama mtu mbaya kihivyo.tuache ushabiki

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *