Unataka kuoa au kuolewa? Fahamu kundi la damu la mweza wako

Jamii Africa

Kuna vitu vingi vya kuzingatia unapomchagua mtu kuwa mwenza wa maisha yako. Jambo mojawapo la kuangalia ni kundi la damu.

Sio kitu kinachozingatiwa na watu wengi wakati wa uchumba lakini fahamu kuwa utofauti wa makundi ya damu unaweza kusababisha matatizo kwenye ndoa. Matatizo hayo yanaweza kutokea wakati wa ujauzito na kumuweka mtoto ambaye hajazaliwa katika hatari.

 

Mfumo wa Makundi ya Damu

Tunapokutana au kujuana na wapenzi wetu, aina ya damu ni miongoni mwa vitu tunavyoshirikiana. Unaweza kusema nina kundi la damu A+ au B-. Lakini unafahamu alama hizo zinamaanisha nini?

Hizo alama ni viashiria vya makundi ya damu zetu. Ni Mfumo wa makundi ya damu tunayomaanisha wakati tukisema ‘A+’ au ‘B-‘ ni mfumo wa ABO na Rh. Zaidi ya hapo tuna mifumo 30 mingine ya makundi ya damu ambayo hutokana na antijeni 300 (seli ndogo ndogo) ambazo zinaunda kinga ya mwili.

                                     Chembe chembe za damu

 

Mfumo ABO wa makundi ya damu

Mfumo ABO unatokana na kuwepo au kutokuwepo kwa antijeni A au B kwenye tabaka la seli za damu. Kama una kundi A la damu, ina maana una antijeni A na hivyohivyo kwa kundi B la damu. Lakini vipi kama una kundi AB au O la damu? Kundi AB la damu linaashiria kuwa una antijeni zote za A na B na kundi O linaashiria kuwa huna antigeni yoyote kati ya A na B.

Jambo linalofuata ni kwanini hatuhamishi damu kutoka baadhi ya makundi kwenda kundi jingine?

Kimsingi, kama una kundi A la damu, mwili wako utatambua seli za kundi B la damu kama kitu kigeni na kutengeneza kingamwili (anti-A) dhidi yake. Vile vile kwa watu wenye kundi B watatengeneza kingamwili (anti-A) dhidi ya seli za kundi A la damu.

Hizi kingamwili anti-A na anti-B zitatambua antijeni A na B na zitapingana au kupishana na kusababisha seli kufa. Kwa kesi ya kundi AB la damu, hakuna kingamwili ikiwa na maana kuwa mtu yeyote mwenye kundi lolote la damu  anaweza kumpa mtu mwenye kundi AB.

Kwa upande mwingine, mtu mwenye kundi la O la damu anaweza kutengeneza kingamwili zote mbili ikiwa atakutana na kundi lolote la damu, lakini upungufu wa antijeni yoyote inarahisisha kuchangia.

 

Mfumo wa kundi Rh la damu

Mfumo wa Rh una zaidi ya antijeni 50. Zinazopatikana kwenye mwili wa binadamu ni 5: D, C, c, E na e. Kati ya hizi antijeni D ni muhimu sana kwenye mfumo wa Rh. Kuwepo au kutokuwepo kwa antijeni D kunawakilishwa na alama za chanya (+) au hasi (-).

Ikiwa mtu mwenye damu yenye Rh hasi (Rh-) atakutana na mtu mwenye damu yenye Rh chanya (Rh+), mwili utatengeneza kingamwili ambazo zinataangamiza seli. Hata hivyo, ikiwa damu ya Rh hasi ikihamishiwa kwa mtu mwenye damu ya Rh chanya, hakuna mgongano utakaotokea kwenye antijeni au kingamwili.

Sasa ukisema una AB+, ina maana una antijeni A, B na D, lakini ukisema una O hasi, inaashiria kuwa hauna antijeni yoyote na kingamwili zote.

Kwanini ni muhimu kulinganisha makundi ya damu na mwenza wako?

Hata kama kuna utofauti wa makundi ya damu hauathiri wanandoa, unaweza kuwa tatizo wakati wa kupata mtoto. Utofauti wa mfumo wa ABO sio jambo kubwa, lakini sio kwa mfumo wa Rh. Kutofautiana au kutoingiliana kwa Rh ni tatizo kubwa ambalo linaweza kumuathiri mama na mtoto.

Wanasayansi wanaeleza, kuwa kutokuingiliana kwa Rh kunatokea wakati mama ana Rh hasi na kichanga kina Rh chanya. Ikiwa damu ya kichanga (yenye Rh chanya) ikivuja na kukutana na mzunguko wa uzazi wa mama (ambao una Rh hasi), seli za kichanga zitatambulika kama ni za kigeni.

Matokeo yake mama atatengeneza kingamwili inayoitwa Rh immunoglobulin G. Hizi kingamwili zitapita kwenye mfuko wa uzazi na kushambulia seli nyekundu za damu za kichanga kilichopo tumboni. Na seli nyekundu za damu zikiharibika zinatengeneza ‘bilirubin’ ambazo zinasababisha mtoto apate ugonjwa manjano (jaundice).

Kesi kama hizo za kuvuja kwa damu ya kichanga kwenye mzunguko wa uzazi hutokea zaidi wakati wa kujifungua/kuzaa. Kwasababu hiyo, mama hatengenezi kingamwili za kutosha, mtoto wa kwanza hawezi kudhurika.

Kutokea kwa hali hiyo kutaendelea kuongezeka kwa mimba zinazofuata kama kichanga kitakuwa na Rh chanya. Na matukio mabaya zaidi kusababisha upungufu wa damu mwilini (Anemia) na kuzaliwa kwa mtoto aliyekufa (stillbirth).

 

Jinsi ya kutibu

Ikiwa mtoto atazaliwa na Anaemia, ataongezewa maji na huduma ya mionzi ya (bilirubin lights) ili kumtibu na maradhi hayo. Mionzi hiyo inatoa miale (emitting rays of 420-470 nm) inayobalisha bilirubin kwenye mfumo ambao unarahisisha kuondolewa mwilini. Ikihusishwa na kuongezewa maji kunafanya mchakato ufanikiwe kwa haraka.

Kama mtoto atakuwa ana hali mbaya anaweza kuongezewa damu akiwa kwenye mfuko wa uzazi. Sindano inaingizwa kwenye mfuko wa uzazi kwa kutumia mashine ya ultrasound. Uongezaji wa damu unafanyika mara kwa mbili au tatu kabla mtoto hajazaliwa.

Hata kama matibabu ya Anaemia ni mazuri na yanaweza kuleta matokeo chanya, kinga au uzuiaji ni chaguo zuri. Matibabu ya ‘Rho (D) immune globulin’ yanaweza kutumika kumtibu mama mwenye upungufu wa chembechembe za damu wakati wa ujauzito.

Ikiwa kuna dalili kuwa seli za Rh-chanya zinaweza kuingia kwenye mzunguko wa uzazi, matibabu hayo yanaweza kufanyika katika wiki ya 28 hadi 32 ya ujauzito na saa 72 wakati wa kujifungua.

Uzuiaji wa kutoingiliana kwa Rh ni rahisi sana kuliko maumivu na ugumu unaotokea wakati wa matibabu. Wanandoa wanatakiwa kupima ili kubaini uwezekano wowote wa kutofautiana kwa damu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufanya maamuzi.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *