MTOTO mwenye maumbile ya ajabu akiwa na jinsia mbili za kiume na moja ya kike amezaliwa Aprili 25 mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma mjini Songea. Mtoto huyo ambaye bado yupo hai chini ya uangalizi maalum amezaliwa akiwa na hitilafu katika maumbile yake ikiwa ni pamoja na kuzaliwa na nusu ya ubongo ambayo imetokana na hitilafu kwenye mfumo wa kichwa hadi uti wa mgongo.
Picha hii inamuonesha mtoto aliyezaliwa katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma akiwa na maumbile ya ajabu yakiwemo jinsia mbili za kiume na jinsia moja ya kike ambazo zipo juu ya kichwa chake ambacho pia kimeumbwa kwa nusu ya ubongo hali ambayo inahatarisha maisha ya mtoto huyo aliyezaliwa akiwa na uzito wa karibu kilo mbili baada ya kutimiza miezi tisa.
Muuguzi wa zamu katika wodi ya wazazi katika hospitali ya mkoa ambako mtoto huyo anaangaliwa Agness Mwinuka amesema mtoto huyo ambaye amezaliwa na uzito wa kilo moja na gramu 900 amezaliwa akiwa na jinsia mbili za kiume na jinsia moja ya kike.
“Jinsia moja ya kiume ipo kama kawaida isipokuwa jinsia moja ya kiume ipo kichwani karibu na kisogo na jinsia ya kike ipo utosini, mtoto huyu tangu azaliwe juzi hadi sasa hana uwezo wa kunyonya wala kula kitu chochote ,uchunguzi wa kitabibu bado unaendelea’’,alisisitiza.
Mama mzazi wa mtoto huyo Situmahi Mwinuka(32) mkazi wa Msamala mjini Songea anasema huyu ni mtoto wake wa nne kuzaliwa na kwamba watoto wake wengine watatu hawajawahi kupata hitilafu yeyote katika mwili.
Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Ruvuma Dk.Mathayo Chanangula akielezea hali ya mtoto huyo alisema mtoto anakabiliwa na tatizo ambalo kitaalam ni hitilafu kwenye mfumo unaoanzia kichwani hadi kwenye uti wa mgongo ambao umesababisha mtoto huyo kuzaliwa na nusu ya ubongo.
Kulingana na daktari huyo hitilafu hiyo imesababisha mifumo ya mwili kuwa na dosari ambapo kuna sehemu mbili za kiume moja ikiwa kichwani na kwamba mtoto anapolia sehemu ya kiume ya kichwani inasimama na kusisitiza kuwa maisha ya mtoto huyo ni mafupi kutokana na mifumo ya mwili wake kutokamilika licha ya kwamba mtoto amezaliwa na miezi tisa.
“Katika nchi zilizoendelea madaktari bingwa na wenye vifaa vya kisasa wanaweza kuokoa maisha ya mtoto huyo,hata kama mtoto huyo anaokolewa atakabiliwa na tatizo kubwa la ulemavu wa akiri kwa kuwa ubongo alionao ni nusu tu ya ubongo unaotakiwa kwa binadamu kamili’’,alisisitiza.
Dk. Chanangula anabainisha kuwa mama mjamzito anaweza kujifungua mtoto mwenye maumbile ya ajabu iwapo atakosa madini aina ya folic acid ambayo alisisitiza ni muhimu kwa mama mjamzito kunywa madini hayo miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito wake.
“Mama anaweza kujifungua mtoto mwenye maumbile ya ajabu iwapo katika miezi mitatu ya mwanzo katika ujauzito wake atatumia dawa aina ya flagile, dawa za minyoo, tetesakline na baadhi ya dawa za malaria kama vile SP ambayo anaruhisiwa kunywa baada ya wiki 28 na ALU ambayo hairuhusiwi kabisa kutumika kwa mjamzito kwa ujumla ni marufuku mama mjamzito kunywa dawa bila kumuona daktari’’,alisisitiza.
Katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma hili ni tukio la kwanza la aina yake mtoto kuzaliwa akiwa na hitilafu kubwa katika mifumo ya mwili wake.
Inasikitisha sana,kunahitajika Neema kubwa ya Mungu kulipokea na kulikubali.Mungu na awatie nguvu
Yote ni mapenzi ya Mungu,Hakuna la kufanya!
Mungu aweke mkono wake hatutaweza chochote.
Jamani tuombe sana MUNGU awatie neema wazazi wake inasikitisha sana
tumuombee mtoto huyu.
Mungu awatie nguvu wazazi wa mtoto huyu kukubaliana na hali hiyo. kwani yote ni mipango ya Mungu.
MUNGU NI WA AJABU. TUWAOOMBEE WAPATE MOYO WA KUMLEA VEMA
yote mipango ya mungu tumuombe huyo mama ili mungu amjaalie apate mwengine
MUNGU AWANUSURU NA MAWAZO POTOFU WAMSHUKURU KWA KILA JAMBO MUNGU WANGU AWATIE WAZAZI HAO MOYO MKUU WA KUMLEA MTOTO WAO. MUNGU MWENYE REHEMA AWAONGOZE KWA KILA MFANYALO.
Muache mungu aitwe mungu
mungu awatie nguvu wamlee vema huyo mtoto kwani ni mipango ya mungu wamchukulie kama wanavyowachukulia hao wengine ni mojawapo ya familia yao wamjali kama binadamu wengine mungu awasaidie na awatie nguvu na moyo wa huruma wa kumlelea huyo mtoto. ahsanteni
jaman awaepushe na mawazo potofu ambayo watu wanaweza kusema,pia ni jambo la kumshukuru mungu,zaid tujumuike na wazazi wa mtoto huyo katika maombi
mimi nafikiri wajawazito wafuate maelekezo ya wataalamu wa afya,kuepuka mazala kama haya
Mbutana lomsia.ruwaaaa!
Mungu, Mungu, Mungu, Mungu … hayahusiani! Hii aidha imetokea kwaajili ya hitilafu kwenye DNA iliyosababishwa na kemikali kwenye vyakula na mazingira yetu. Watanzania mmelala – kila kitu mnasema ni mapenzi ya mungu. Wapi! Mungu kweli angetaka mtoto wake azaliwe hivyo ili afaidike nini? Acheni kupumbazwa na dini!
Poleni sana na matatizo. Tusimlazimishe kuishi kama Mungu amemwandikia vinginevyo, wakati mwingine ni matokeo ya madawa na mazingira yatuzungukayo. Kila la heri, nawaombea subira kwa upendo.
glory be to god
ni mapenzi ya mungu
Acheni mungu aitwe mungu kwa mimi na wewe ambao tumependelewa tumshukuru mungu kwa kila jambo na tumuombee huyo mtoto kwa mwenyezi mungu ili amtendee muujiza amen by Bruno Mwakalyobi.
ni mapenzi ya muumbaji kwani kazi yake haina makosa,poleni sana
yote tumwachiee MUNGU
Mungu awe nawe katika maisha yake mtoto huyo, pia madaktari wamfanyie uchunguzi wa kina ili kupata nini kilifanyika kati ya mama yake na baba yake juu yakiumbe hiki
Jina la Mungu libarikiwe, hiyo yote ni kazi yake Mola, tumuombee mtoto huyu
Pole sana mama pamoja na mtoto wako, jua kazi ya Mola haina makosa Mungu awe nawe
kwa kweli hapo ndipo mtu unaanza kujiuliza maswali je mimi ni nani hata yampate yule na sio mimi.cha muhimu kukumbuka ni kwamba Mungu ana makusudi yake ili jina lake litukuzwe milele, tuache Mungu aitwe Mungu. kwa familia ni mkono wa Mungu tu unaweza kuelewa namna mama huyu anajisikia tumuombee Mungu ampe nguvu kwani yeye hutupa jaribu tuwezalo kutoka daima. jina lake lihimidiwe milele.