Kikwete akutana na Viongozi wa CHADEMA; Mazungumzo kuendelea J’tatu

Jamii Africa

Kikwete akisalimiana na Mbowe Ikulu jijini Dar es SalaamRais Kikwete ameanza mazungumzo na viongozi wa CDM kuhusu mustakabali wa mchakato wa kuelekea Katiba Mpya. Mkutano huo ambao uliombwa na viongozi wa CDM kufuatia mkutano wa Kamati Kuu Jumapili iliyopita ulikuwa na makusudio ya kuleta mapendekezo ya Chama hicho kwa Rais Kikwete ili kumshawishi kutotia sahihi mswada wa Sheria ya Kusimamia Mchakato wa Katiba ambao uko mezani kwake na unaotarajiwa kutiwa sahihi wakati wowote.

Katika taarifa ya viombo vya habari baada ya mkutano huo wa leo Kurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu imesema kuwa mkutano huo ulifanyika katika mazingira ya kirafiki ambapo pande mbili zilikubaliana kuendelea na mazungumzo zaidi siku ya Jumatatu. Viongozi wa CDM waliwasilisha kwa Rais mapendekezo yao ya mambo gani ambayo wanaamini yanakosekana katika mswada uliopendekezwa na jinsi gani ni muhimu kuyazingatia kabla wao kama chama hawajatoa ushirikiano katika mchakato huo. Taarifa ya Ikulu imesema kuwa ni baada ya kupokea mapendekezo hayo ndio Rais Kikwete aliomba apewe muda ili pamoja na viongozi wenzake waweze kupitia mapendekezo hayo ili kuweza kuwa na msimamo mzuri.

Mkutano unatarajiwa kuendelea tena kesho Ikulu Dar-es-Salaam. Hata hivyo inaratajiwa kuwa pamoja na mkutano huu na viongozi wa CDM Rais Kikwete anatarajiwa kuzungumza na viongozi wa taasisi nyingine japo haijajulikana vikao hivyo vingine vitafanyika lini na kama vitafanyika kabla ya mswada haujatiwa sahihi kuwa Sheria.

PICHA: CHADEMA wakutana na Kikwete Ikulu


Wakiwasili viwanja vya Ikulu


Wassira akiwapokea Ikulu.


Membe akiomba udhuru akahudhurie mazishi ya maaskofu waliokufa ajalini. Mazishi yamefanyika Pugu jijini Dar es Salaam


Viongozi wa CHADEMA baada ya kupokelewa Ikulu


Rais Kikwete akiwapokea



 

Walioketi toka upande wa kulia wa Rais; Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa CDM Taifa), Said Arfi (Makamu Mwenyekiti Bara), Said Mzee  Mohammed (Makamu Mwenyekiti Zanzibar), Prof. Baregu (Kamati Kuu), Tundu Lissu (Mnadhimu wa Upinzani), John Mnyika (Mbunge) na Prof. Safari (Mjumbe wa Kamati Kuu).


Rais Kikwete na ujumbe wake akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa CHADEMA ikulu jijini Dar es Salaam. Nini kinaendelea, tutege masikio maana kwa mtazamo wangu tofauti zetu zitaondoka tu kwa kukaa pamoja na kuafikiana maafikiano kwa manufaa ya taifa letu, kila upande kuwa tayari kuvumilia vinginevyo ngangari si suluhisho la matatizo na nguvu ya dola ni kuleta taharuki zaidi ya mwafaka.

JK akisalimiana na Lissu

Habari na M. M. Mwanakijiji (Picha na Ikulu)

 

1 Comment
  • Tunapaswa kuwa wa wavumilivu kwa maamuzi yoyote yatakayokuwa yamepatina katika kikao hiki cha ndani cha hawa mahasimu wawili wa siasa.

    Cha msingi ni kuendelea kuwaombea ili pande zote mbili ziweze kuelewana kwa amani kwa kile kitachokuwa kimewekwa mezani.

    Maana haiwezekani mawazo yote ya pande zote mbili yatakuwa sawa lazima kwa namna moja ama nyingine waangalie ni kp kmepungua na kipi wanatofautiana ili kupata suluhisho kwa njia ya amani.

    Mungu awatangulie

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *