Dhamana kwa watuhumiwa si mwisho wa kesi-Polisi

Jamii Africa

ZANZIBAR JUMATANO APRILI 11, 2012 Jeshi la Polisi limewataka wananchi kutovunjika moyo na kuacha kushirikiana na Jeshi hilo katika kukomesha vitendo vya kihalifu kwa kuwaona watuhumiwa waliokamatwa wakiwa nje kwa dhamana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Kamishna Msaidizi Aziz Juma Mohammed

Rai hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Kamishna Msaidizi Aziz Juma Mohammed, wakati akitoa elimu juu ya utii wa sheria bila shuruti na Ulinzi Shirikishi.

Kamanda Aziz amesema kuwa idadi kubwa ya washukiwa wa wanaokamatwa hutuhumiwa kwa makosa yanayotoa uhuru wa dhamana kisheria kwa mtuhumiwa.

Amesema mtuhumiwa anaweza kukamatwa na kupewa dhamana akiwa katika kituo cha Polisi ama Mahakamani kwani hiyo nayo ni haki ya mtuhumiwa

Hata hivyo Kamanda Aziz amesema kuwa kila mwananchi hasa waliotendewa matukio ya kihalifu wanayofursa ya kwenda kituo cha Polisi ama mahakamani kuulizia maendeleo ya kesi inayomhusu.

Lakini amesema watuhumiwa wengi wanapopewa dhamana ya Polisi ama ya mahakama wamekuwa wakitamba mitaani kuwa wametoa hongo jambo ambalo amesema limekuwa likiongeza idadi ya tuhuma za rushwa katika taasisi za Polisi na Mahakama.

Amewahimiza wale wote wanaoshuhudia matukio ya kihalifu kuwa tayari kwenda Polisi kutoa maelezo yao na baadaye kwenda Mahakamani kutoa ushahidi wa yale aliyoyashuhudia ili kuiwezesha Mahakama kutoa uwamuzi wa haki kwa pande zote mbili.

Kamanda Aziz amesema hakuna mtuhumiwa atakayepatikana na hatia mahakamani pasipokuwepo kwa ushahidi wa kutosha kuwezesha mahakama kuthibitisha kosa.

“Ukitoa maelezo yako Kituo cha Polisi na ukaacha kwenda kuielezea mahakama juu ya kile ulichokishuhudia haitoshi na hivyo mtuhumiwa anaweza kufutiwa shitaka lake”. Alisema Kamanda Aziz.

Hivi sasa Jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar kupitia kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa wakiongozwa na Kamishna wa Polisi Visiwani humo CP. Mussa Ali Mussa, linaendelea na mkakati wake wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya utii wa sheria bila shuruti pamoja na haki za watuhumiwa.

Imeandalia na Moahammed Mhina, wa Jeshi la Polisi -Zanzibar

1 Comment
  • Viongozi wa Jeshi la polisi zanzibar hawana ukweli hata kidogo,mara nyingi askari wadogo wanafanya kazi vizuri sana na kwa bidii sana,lkn viongozi wao wanawavunja kasi,wanakamata wahalifu wa kutumia nguvu na wanakuwa wabaya ktk tukio,hafla utasikia makamanda wanapiga simu kwa wachini yao na kuwaamuru wawachie,kadhia hiyo ht kamishna wa zanzibar analo sana,ni msumbufu sana kwa maafisa wake,na ndio maana askari wengi sasa zanzibar hawataki kufanya kazi kidhati,wanamalizana hukohuko njiani,ukimkamata tu mhalifu hapo hapo utamsikia akisema ngoja nimpigie kamishna au kamanda azizi,wamecheza sana na wahalifu hd wamejenga mazoea,hata ukiangalia hao kina aziz na kamishna mussa tangu hapo hajawa kamishna alikuwa mlaji mkubwa sana wa rushwa,tunashangaa sana kupewa ukamishna.vumillieni askari wa zanzibar,kamateni wahlifu na ht km wakiwapa dhamana za uongo stahamilini tu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *