2 Watimuliwa Geita Gold kwa kudai Chama cha Wafanyakazi

Jamii Africa

Wakati taifa bado linafuatilia habari za mgodi wa Barrick huko Tarime, habari nyingine ambazo zimepatikana zinadai kuwa viongozi 2 (mwenyekiti na Katibu) wa wafanyakazi kwenye mgodi wa Geita Gold huko Mkoani Geita wamefukuzwa kazi hapo jana huku wakipewa siku tatu kukata rufaa baadaya kuongoza maandamano ya kudai chama chao cha Wafanyakazi Migoni kisajiliwe kitu ambacho kinadaiwa kupingwa na menejjimenti kwa madai kuwa “idadi” ya wanachama haijatimia licha ya wafanyakazi hao kudai kuwa idadi imeshatimia ya kuweza kuundwa kwa chama cha kudai haki na maslahi ya wafanyakazi.

Upande wa menejimenti unadai kuwa wafanyakazi hao wamefukuzwa baadaya “kuwatukana” uongozi kwenye mabango yao ambayo yalitumika kudai chama chao cha wafanyakazi. Hadi hivi sasa imekuwa ngumu kwenye baadhi ya migodi kuunda vyama vya wafanyakazi wakati kwenye baadhi yao vyama hivyo vipo. Mgodi wa Kahama Mining unao chama cha wafanyakazi migodini (TAMICO).

Kuna mambo mengine ambayo yamo mikononi mwa vi-nzi na yataweletwa ili kuonesha harakati ambazo zinafanya kuzuia wafanyakazi kujiunga pamoja kupigania na kudai haki zao hasa huko migodini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *