Uporaji wa ardhi wachangia njaa na umasikini

Jamii Africa

MWANAHARAKATI kutoka nchini Zimbabwe Magreth Dongo amesema umasikini na njaa vinavyochangiwa na uporaji wa ardhi ya wananchi vinaweza kuwafanya wananchi wakate tamaa na kulazimika kushinikiza serikali kurudisha ardhi yao.

Akitoa mada katika tamasha la jinsia linaloendelea katika viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jijini Dar es salaam mwanaharakati huyo alisema  wananchi wana haki ya kudai mabadiliko na kuishinikiza serikali kama ilivyofanyika nchini mwake.

Alisema ni makosa kumlaumu Rais Robert Mugabe kuwa aliwanyang’anya ardhi wazungu wachache bali hali hiyo ilitokana na shinikizo la wananchi masikini ambao waliendelea kukabiliwa na njaa huku ardhi ikimilikiwa na watu wachache.

Alisema kutokana na ardhi ya nchi hiyo kumilikiwa na wazungu wachache kwa muda mrefu wananchi walikasirika na kudai ardhi yao kuondolewa mikononi mwa wachache huku akitoa mfano wa wananchi wa Loliondo ambao wako katika mgogoro na mwekezaji.

Aidha alisema pamoja na changamoto zilizopo hivi sasa za kupigania umiliki sawa wa ardhi alijivunia kuwa nchi hiyo imepiga hatua na kuwa wakulima wadodo wa vijijini ndiyo hulilisha taifa na wala sio wafanyabiashara wakubwa.

Aidha katika tamasha hilo baadhi ya wananchi kutoka Loliondo walitoa madai ya ardhi yao kuchukuliwa na mwekezaji huku wakilaumu serikali kuwa pamoja na kupeleka tume nyingi za kuchunguza mgogoro huo hakuna hata moja iliyotoa majibu.

Mmoja wa wananchi hao Kijoolu Kakeya alisema wanataka kulindwa katika ardhi yao na kushirikishwa katika maamuzi huku akiituhumu serikali kuwa imeshindwa kuwalinda na badala yake inamnyenyekea mwekezaji.

Pia mwenyekiti wa kijiji cha Arash Kiaro Orminis alisema ni aibu kwa kiongozi wa serikali kama yeye kuilalamikia serikali yake dhidiya vitendo vya unanyasaji vilivyofanywa na polisi wakati wa oparesheni ya kuwahamisha wananchi wa vijiji nane  ili kumpisha mwekezaji.

Akihojiwa na FikraPevu juu ya madai yaliyotolewa na wanaharakati Ofisa Ardhi Mwandamizi kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba Maendeleo ya Makazi Grace Gulinja alisema migogoro yaardhi nchini ipo mingi na kudai kuwa sheria za ardhi za hapa nchini ni bora ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika.

Alisema kuna masuala ambayo hawana uwezo nayo katika mgogoro wa Loliondo huku akilaumu baadhi ya wanasiasa katika maeneo mbalimbali yenye migogoro kuwa wanaathiri baadhi ya maamuzi.

Alipoulizwa ukimya wa Serikali kutoa majibu ya tume nyingi zilizoundwa Ofisa huyo alisema kuwa majibu hayatatolewa na kuomba asiulizwe zaidi kuhusu suala hilo ambalo limedumu kwa miaka kadhaa bila kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.

2 Comments
  • ni makosa kumlaumu Rais Robert Mugabe kuwa aliwanyang’anya ardhi wazungu wachache bali hali hiyo ilitokana na shinikizo la wananchi masikini ambao waliendelea kukabiliwa na njaa huku ardhi ikimilikiwa na watu wachache.
    Napia ni HAKI kumumlaumu kiwete kuachia uchumi wetu kumilikiwa na watu wachache,wananchi waanze shinikizo pia atatue tatizo hili hata kwa utaifishaji(Nationalization) au kodi maalimu kwa matajiri kama(surtantax),na kufuatilia njia za upataji mali kwa matajiri wakati na wakubwa sambamba na ukaguzi mali na pesa haramu.
    Tz ijue cc pia tunaugua ugonjwa mkubwa wa watuwachache kula keki ya taifa,ndiyo maana ajira zinapungua kila cku,rasirimali zinaibiwa,kiongozi anatoa maeneo kwa suti n.k,n.k kisingizio ni uwekezaji na soko huria,ambavyo hatu viingilii na kuvisimamia kwa karibu.
    Tz tusikubali ukoloni mamboleo kwa sera za kipuuzi hata kama raisi anazikubali sera za wanyonyaji I.M.F na world bank eti kupunguza waajiriwa,kushea gharama za matibabu na afya kwa mtu anaye ishi kwa 400TSH,NI UJINGA…..C UZALENDO…….

    Tunaona maeneo yanachukuliwa na wawekezaji wakuja wanabaki walinzi na vibarua.
    Mashamba yanapandwa maua,na JOaftra inapelekwa nje,mazao ya chakula hayapandwi…Njaa isituuwe na ili ongezekom la joto na wakulima bado tegemea mvua,wengi wana tegemea kuchoma mkaa na kuni kaboni na njaa vitatuacha?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *