Amuua mkewe kwa kumcharanga mapanga kisha kujinyonga

Jamii Africa

MKAZI wa kijiji cha Byamutemba kata ya Nsunga wilayani Missenyi Hashimu France (43) amemuua mke wake Aisha Hashimu (39) kwa kumcharanga mapanga kisha naye kujinyonga katika tukio lililotokea jumatatu.

Akiongea na FikraPevu Mwenyekiti wa kijiji hicho Abubakar Idd alisema baada ya kutekeleza mauaji hayo alikusanya vitu vyote ndani ya nyumba na kuvichoma na hatimaye kujinyonga katika chumba tofauti.

Pia alisema kabla ya kujinyonga baada ya kumuua mke wake, alimfukuza mtoto waliyekuwa wanaishi naye ambaye ndiye alitoa taarifa za maujai hayo yaliyofanyika usiku.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti huyo inasadikiwa wanandoa hao walikuwa na mgogoro katika ndoa yao na siku ya tukio inadaiwa mwanamke alirudi usiku akiwa amelewa.

“Baada ya kumuua mke wake naye alijinyonga, alizichoma moto mali zote ndani ya nyumba na alimfukuza kwanza mtoto waliyekuwa wanaishi naye ambaye alitoa taarifa” alithibitisha mwenyekiti huyo.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani Kagera Vitus Mlolele amethibitishia Fikrapevu kwa njia ya simu kutokea kwa mauaji hayo.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *