Breaking News: RPC Mwanza Liberatus Barlow auawa!

Jamii Africa
liberatus barlow enzi za uhai wake

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Barlow ameuawa usiku wa kuamkia leo katika tukio linalohusishwa na ujambazi.

Taarifa kutoka Mwanza ambazo zimethibitishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini zinasema kuwa Kamanda Barlow aliuawa baada ya kumrudisha dada yake kutoka katika kikao cha harusi ya ndugu yao huko Kitangili.

Hata hivyo, taarifa hizo bado hazijaweza kuchunguzwa na vyombo vya habari.

liberatus barlow enzi za uhai wake

Marehemu Kamanda Barlow

Taarifa zaidi tutawapatia…

Na. M. M. Mwanakijiji

30 Comments
  • Jamani Tanzania tunaelekea wapi mpaka tunadiriki kuwaua viongozi wetu na makamanda wutu wanao tulinda na kusimamia ulinzi na usalama wa raia. Eee MUNGU UTUREHEMU jamani Tanzania inaelekea wapi hadi tunadiriki kuwaua watu wasiokuwa na hatia.

    • Jamani hii nchi imekumbwa na nini matukio kila kukichaaa
      Naomba muongozo wanajamii hivi kamanda wa mkoa anakuwa hana hata wa kumlinda?

  • Hii ni kuthibitisha kuwa hali ya usalama nchini siyo nzuri na kwamba wote tuna fursa sawa ya kuathiriwa na matukio ya uhalifu! Ni wakati muafaka sasa wa serikali kufanya juhudi kama za wakati wa mwanzo wa awamu ya 4 hata tukapumua kidogo. Bila operesheni maliza uhalifu itakuwa vigumu kukomesha uhalifu.

  • Tanzania yetu inaelekea wapi?

    Huu ujambazi mpaka lini…?

    RIP Kamanda Liberatus Barlow; Hakika Taifa limepoteza mtu muhimu.

  • Ukweli sasa nchi inaelekea pabaya, kwa kiwango cha kumuua kamanda wa mkoa sii tu inaumiza ila inafedhehesha jeshi lapolisi,matukio yaliyopita yanaonyesha kukosekana kwa umakini au kufanya kazi kwa mazoea kulikozoeleka na serikali yetu,wameuwawa raia wasio na hatia serikali kimya,ameuwawa mwandishi wa habari serikali kimya,amekoswa koswa mkuu wa immigration kwa kufananishwa na jambazi pia serikali imekaa kimya sasa ameuwawa kamanda wa mkoa wa mwanza sijui serikali itachukua hatua gani? Au mpaka afe Waziri?

  • Pamoja na masikitiko yangu kwa kifo cha Kamanda Liberatus Lyimo Barlow @LLB ni uthibitisho kwamba majambazi hao watakamatwa na siku moja ujambazi
    utafika kikomo. Siku zote majambazi wanapoua lazima
    watapatikana/kujulikana tu! Hata aliyefyatua bomu lililomuua Daudi Mwangosi si tumemjua. Kumbukeni hata waliomuua kamanda masanja kule mbinga miaka kadhaa iliyopita si tumewajua. Niwapeni mfano mwingine, aliyemtesa Dk Ulimboka kwa vile hakufa hadi leo hajajulikana/amejificha anapojua yeye na waliomficha. Hata waandishi wa mwanahalisi kwa vile hawakufa ktk tukio lile hadi leo wamepotezea (waandishi wenyewe) na hatujui hatima yake iliishaje japo tunasikia kesi imeisha. Binafsi naiombea roho ya kamanda Barlow ipumzike kwa amani baada ya kuwa amelitimiza kusudi aliloumbwa kuja kulitimiza duniani!

  • Kama hali hii itaendelea hivi nadhani swala la usalama wa watu na mali zao halipo tena ukizingatia kamanda wa mkoa anauawa sasa raia wa kawaida atalindwa na nani kuna usalama hapo?

  • …..Mauaji kwenye mikutano ya siasa yasiyo na majibu hadi sasa, vurugu za kidini mbagala ambapo waislam wamechoma makanisa, kujinyoga kwa askari ambaye ameacha maswali mengi bila majibu, na sasa mauaji ya Kamanda Barlow………. Ni dalili tosha kua Serikali yetu ya CCM imekosa uelekeo na dola sasa inaelekea kutotawalika

  • Mimi binafisi sijapatwa na uchungu wowote kuhusu kifo hicho cha LIBERATUS BARLOW kulinganisha na cha DAUDI MWANGOSI.Kama polisi wameamua kuua raia wema basi wao polisi watauawa na raia wabaya (majambazi).

      • Yaani mi ndo kabisa sijaguswa hata kidogo. Kumbe hata polisi huwa wanakufa kwa risasi. Sasa inakuwaje raia wema wanauawa na polisi huku polisi wakiuawa na raia wabaya. Mungu analipa hapahapa duniani. Polisi jisafisheni ili raia wema wakusaidieni kwenye ulinzi.

  • Huyo jambazi aliyemwua Barlow ni product ya uzembe wa polisi.wamewaacha majambazi mitaani,wakipambana na wafuasi wa chadema .Wakidhani majambazi ni adui wa raia tu.Kumbe jambazi hachagui,iko siku majambazi wataingia mpaka ikulu.Kuna siku utasikia “Breaking news: Rais aibiwa mikate yote saa nane za usiku”.

  • sasa tutajifunza somo moja murwa sana nalo ni matabaka ktk kushughulikia mambo mazito (kuuwawa kwa watu wa matabaka tofaut) leo hii watu watawekwa ndani sana kesi hii uchunguz wake utaenda kwa kasi
    MWENYEZ MUNGU AMREHEMU, NAWAPA POLE NDUGU JAMAA NA MARAFIKI NA WATZ WOTE KWA MSIBA HUU

  • Sasa cha ajabu nini?!! Nashangaa watu wanavyokua wanafiki kujitia wanasikitika,kwani mbona wao wanauwa watu wasio na hatia kila siku,wanateka watu wanawatesa! Au mmesahau kuwa muosha huoshwa!! Sawa sawa tu alivyouwawa,nao waipate.

  • Mauji ya Kamanda wa Polisi yaliyofanyika hapa jijini Mwanza juzi, yanasikitisha sana, nashauri mikakati ya kiulinzi ifanyike hata kwa maofisa wa ngazi mbali mbali kwa majeshi yetu na viongozi wa ngazi mbali mbali. Kiongozi mkubwa kama yule, hapaswi kutembea usiku bila ulinzi hata kama hayuko katika shughuli za ki kazi. kwani Polisi au Mwanajeshi yeyote maisha yake popote alipo anakuwa katika mazingira ya kikazi na pia ana maadui wengi hata wale asio weza kujua wala kuhisi kuwa maadui zake. Juhudi za tahadhari zichuliwe tangu sasa.

    • swali na wazo zuri sana.?? kuna kitu tu hapa wala si bure.. au ni UAIJIPIIII nini.? maana mshikaji aliyepo si tumesikia amegoma kuongezwa muda kwa hiyo inabidi achaguliwe mwingine.. ndyo wameshaanza kupigana vikumbo, na watauana sana tu

      RIP Kamanda

  • Nahuzunika pamoja na wanaoona nchi yetu inavyo haribika hata mauaji imekuwa si kitu cha ajabu tena!

    Viongozi wetu wako wapi?! Hawajui kusoma hata kuangalia picha? Wana macho wala hawaoni na masikio yasiyo sikia?! Kazi yao nini hapo walipo? Inasikitisha!

    Barlow, ukamsalimie Kombe, Mwangosi, na wote waliokufa kifo kama chako baba!

  • Huwa nasikitika kuona double standards ktk kushughulikia matatizo yanayofanana. Mwangosi (R.I.P) hakupata uzito huu aliopewa Barlow. Sawa duniani walikuwa tofauti, sasa wote wameelekea kwa mola mwenye mizani ya haki. Huko nako sijui watakuwa na double standards. Kwa mungu ninaye muamini mimi HAKUNA kitu kama hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *