CHADEMA ‘wauteka’ mji wa Arusha!

Jamii Africa

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hii leo kimefanya mkutano mkubwa jijini Arusha ambapo kimetoa ufafanuzi juu ya maamuzi yake kuwavua uanachama waliokuwa Madiwani wa chama hicho.

Ikumbukwe kuwa jana Godbless Lema alishatoa CD ya kuonyesha kilichojiri hadi kupelekea madiwani hawa kufukuzwa chamani.

Hii leo chama hicho kimekusanya umati wa wananchi ambapo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe amehutubia. Tutawaletea taarifa kwa kirefu lakini pata picha hizi kama zilivyowasilishwa na mdau wa JamiiForums:

Mbowe akihutubia umati wa wananchi hii leo katika uwanja wa NMC

Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mkutano wa CHADEMA hii leo

Kimeongelewa nini, nini kilichojiri nyuma ya pazia? Fuatilia FikraPevu kesho

KUSHIRIKI AU KUONA MAONI YA WADAU JUU YA HABARI HII, TEMBELEA UKURASA HUU – JamiiForums

13 Comments
  • chadema tumeonyesha ni kiasi gani tulivyoweza chukua maamuzi magumu na wanachama wetu wakatuelewa!

  • Ndivyo inavyotakiwa ukiwa kiongozi kuwa na moyo wa kufanya maamuzi magumu hata kama kwa wkati huo inacost but infuture kitaeleweka bravo chadema.

  • nawapongeza chadema kwakuwaonesha watz hakuna aliye juu ya chama..dr.slaa ,mbowe wote mpo makini na timu yenu..safi sana kwa kutibu jeraha kabla halijawa donda ndugu..

  • Nawapongeza sana Kamati kuu ya CHADEMA kwa kuwaondoa haraka Madumilakuwili ndani chama, sasa mshughulikieni SHIBUDA.

  • Sisi vijana tuko tayari kuleta mapinduzi ya kweli ndani ya nchi hii . Natoa wito wangu kwa wote wenye nia thabiti kuleta mabadiliko kuanza kujiandaa kwa Uchaguzi 2015

  • Huwa wanaanza hivyo..watanzania tupige kura viongozi kutokana na mafanikio na siyo ahadi.Ndio nchi itabadilika

  • Ni wazi kwamba, kilakitu kina mwanzo. Usipokuwa makini mwanzoni, upo uwezekano wa kitu hicho kukugharimu sana baadaye na hutakuwa na njia ya kujinusuru tena. Kwakuwa wameliona hilo mapema na kulishughulikia bila woga, hawana budi kupongezwa kwa dhati.

  • bravo cdm. njoon morogoro jaman…………………………….. mbona mnatutenga au sisi sio nini? come this way guyz.

  • PONGEZI KWA WANA CHADEMA.

    Nichukue fursa hii kipekee kuwapongeza wana chadema wote walioshiriki ktk chaguzi mbalimbali nchini kwa kazi nzuri mliyoifanya kwani matunda yameonekana hakika hata chama tawala walijua wanapambana na Chama ambacho si lele mama hata kidogo.

    Pili nawapongeza sana sana kwani hakika tumeshuhudia ukomavu wa kisiasa wa hali ya juu mno mnatutia moyo tunazidi kuhamasika,kwani mmekuwa na utulivu wa hali ya juu ktk kampeni kiasi kwamba wao CCM ndiyo wamekuwa wakileta uchochezi nanyi mkiyavumilia hayo yote hadi pale mlipofikia kikomo ndipo mliposhindwa kuvulia.hili la kupongezwa sana.
    Mwenyekiti wa Chama,Katibu wa Chama,kitaifa na viongozi wote pongezi pokeeni kwani mbinu zilizotumika huko zaonekana zafaa hata kwa chaguzi zingine.

    CHADEMA SONGA MBELE.

    Niwape pole sana wale wote walioumia wakati wa matayarisho ya kupiga kura ama hata kampeni nawaombea mpone haraka turudi kuendeleza mapinduzi nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *