CHADEMA Yabeza Bajeti; yasema ni “Upotoshaji Mkubwa”

Jamii Africa

Chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA kimesema kuwa makadirio ya bajeti ya taifa kwa mwaka 2011/2012 yaliyosomwa na Waziri wa Fedha Bw. Mustafa Mkulo yamejaa upotoshwaji mkubwa na kimewataka wananchi wasizugike kirahisi kwa ahadi motomoto zilizomo ndani ya bajeti hiyo. Katika tamko lake kwa vyombo vya habari jana Waziri kivuli wa Fedha kupitia chama hicho Bw. Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini) amesema kuwa “tumeshtushwa na upotoshaji mkubwa wa kitakwimu na kimaudhui uliofanywa na serikali kwa lengo la kuwajengea matumaini hewa wananchi kuwa watapata nafuu ya maisha kupitia bajeti hiyo wakati hali halisi haipo hivyo.”

Akifafanua juu ya kile ambacho chama chake kinaona ni “upotoshaji mkubwa” Bw. Zitto ametoa mifano mbalimbali kama mashtaka dhidi ya serikali ya Chama cha Mapinduzi kinachotawala Tanzania. Mfano mmojawapo unahusiana na sekta ya Nishati na Madini na hasa kwenye suala la umeme ambapo Bw. Zitto amesema kuwa “Wakati Waziri akitaja kuwa kipaumbele cha kwanza cha bajeti hiyo ni kumaliza tatizo la Umeme na hivyo kutamka kwamba ametenga shilingi 537 Bilioni, , upembuzi uliofanywa na Kambi yetu ya Upinzani kwenye vitabu vya bajeti (Kitabu Namba II na IV) vilivyotolewa na serikali yenyewe, umebaini kuwa Wizara ya Nishati na Madini imetengewa jumla ya kiasi cha shilingi 402,402,071,000 kwa mujibu wa fungu la 58. Fedha hizo zimegawanywa katika mafungu ya Matumizi kawaida shilingi 76,953,934,000 na kwa upande wa bajeti ya Maendeleo zimetengwa shilingi 325,448,137,000.”

Kutokana na hilo Bw. Kabwe amesema kuwa “Shilingi Bilioni 325 zilizotengwa katika Bajeti ya Maendeleo ya Wizara ya Nishati na Madini zinatosha kwa mradi mmoja tu wa umeme wa 160MW, 100 Dar es Salaam na 60 Mwanza. Hakuna mradi wowote mpya wa umeme unaonekana katika Bajeti. Ni dhahiri kuwa kauli ya Mkulo ililenga zaidi kuwajengea wananchi matumaini hewa kuliko kuchukua hatua za kweli za kumaliza tatizo la umeme.”

Kama hilo halitoshi Bw. Zitto alienda mbele zaidi na kuhoji kile ambacho kinaonekana kama ni kuongezeka kwa bajeti ya mwaka huu kulinganisha na mwaka jana. Katika taarifa yake hiyo ambayo aliitoa kama Waziri Kivuli wa Fedha na nakala yake kupatikana na Fikra Pevu Bw. Zitto amesema kuwa “Wakati Waziri na Serikali wanataka kuwaaminisha Watanzania kuwa bajeti ya mwaka huu imeongezeka kuliko ilivyokuwa mwaka 2010/2011, ukweli ni kuwa hakuna ongezeko halisia (real term increase) lililofanyika. Bajeti iliyopita ilikuwa kiasi cha shilingi 11.6 trilioni wakati mwaka huu wa 2011/2012 serikali ina bajeti ya jumla ya shilingi 13.525 trilioni. Kati ya ya fedha hizo za mwaka 2011/2012, kiasi cha shilingi 1.901 trilioni ambazo ni sawa na asilimia 14.06% ya bajeti yote, kitatumika kulipia deni la Taifa.”

Kutokana na hilo Chama hicho kimehitimisha kuwa “Kwa mantiki hiyo, mtaona kuwa fedha kwa ajili ya kuendesha serikali pamoja na kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo zitabaki kuwa ni kiasi cha shilingi trilioni 11.624 ambazo ni sawa na fedha za bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010/2011 (Japo thamani ya shilingi imeanguka ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwaka 2010/2011). Tunasisitiza kuwa hii si bajeti ya maendeleo, hii ni bajeti ya madeni.”

Licha ya hayo Chama hicho ambayo tangu kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi kimeonekana kuendelea kujizolea mashabiki na wanachama wengi zaidi huku kikitoa upinzani mkali kwa CCM kimehoji dhamira ya kweli ya serikali kubana matumizi yasiyo ya lazima, hasa linapokuja suala la Posho. Bw. Zitto ameandika kuwa “Wakati Waziri akisema Bungeni kuwa Bajeti ya mwaka 2011/2012 itapunguza posho kama sehemu ya mkakati wa serikali wa kuthibiti matumizi, nanukuu “kupunguza malipo ya posho mbalimbali yasiyokuwa na tija (uk.53)”, ukweli ni kuwa Bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012 imetenga jumla ya shilingi 0.987 trilioni ambazo ni sawa na asilimia 13 % ya bajeti yote ya serikali kwa ajili ya kulipa posho chini ya vifungu vinavyojulikana kama “Personnel allowances (non discretionary na In-kind”).” Kutokana na mtazamo wake huo Bw. Zitto ametoa angalizo kuwa “ kauli ya Waziri Mkulo kuwa serikali itapunguza posho sio kweli. Tunautaka umma wa Watanzania usikubali kurubuniwa.”

Hata hivyo katika tamko lake hilo Bw. Zitto hakuonesha ni jinsi gani umma wa Watanzania utaweza kukataa kurubuniwa na viongozi au wafanye nini ili kulazimisha serikali kusema ukweli.

Pamoja na hilo Bw. Zitto ameonesha kuwa serikali haijawa mkweli linapokuja suala la posho mbalimbali na kuwa japo kwa upande mmoja serikali inaonekana kupunguza posho upande mwingine imetengeneza mfumo wa kuendelea kuhalalisha posho. “Wakati Waziri akisema kuwa ili kuthibiti matumizi watapunguza posho mbalimbali, kwenye hotuba yake uk.66, waziri amependekeza kufanywa kwa marekebisho ya sheria ya kodi ya mapato SURA 332 na anasema kwenye (i) “kusamehe kodi ya mapato kwenye posho wanazolipwa wafanyakazi wa serikali na wanaofanya kazi kwenye taasisi zinazopata ruzuku kutoka kwenye bajeti ya serikali” .” Bw. Zitto akahitimisha kuwa “Hii inaonyesha dhahiri kuwa kauli ya Kufuta au kupunguza posho ilitolewa na Serikali ili kupumbaza wananchi lakini haina udhati.” Miongoni mwa taasisi ambazo zinapokea ruzuku kutoka serikalini kutokana na bajeti ni pamoja na vyama vya siasa nchini. Hivyo watendaji wa vyama vya siasa vyote nchini hawatokatwa kodi kwenye posho zao endapo mapendekezo ya Mkulo yatapitishwa kama inavyotarajiwa.

Kutokana na hilo la posho Bw. Kabwe amesema kuwa “Kambi ya Upinzani Bungeni imeshtushwa na kushangazwa na hatua ya Serikali kutenga zaidi ya robo ya Bajeti kulipa Madeni na Kulipana Posho (Asilimia 27 – 14% kulipa madeni na 13% kulipa Posho mbalimbali).”

Bw. Zitto ameahidi kuwa atakaposoma bajeti mbadala ya upinzani wiki ijayo “itakuwa inajali masilahi ya Watanzania yenye lengo la kukuza Uchumi wa Vijijini (rural growth) na itajikita katika kupata vyanzo vipya vya mapato na kubana matumizi ikiwemo kufuta Posho mbalimbali.” Hata hivyo, haieleweki ni kwanini mwaka huu Watanzania watarajie CCM wataacha bajeti yao na wachukue ya Chadema kwani hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Chadema au upinzani kuanda bajeti mbadala ambayo mara kadhaa huko nyuma imeonekana kujaa mambo mengi mazuri ambayo CCM imeyachukua na kujipa sifa yenyewe huku Chadema kikiendelea kuwa kisima cha mawazo ya kuisaidia CCM kutawala zaidi.”

Hotuba ya Zitto ya bajeti mbadala itatolewa Jumatano ijayo tarehe 15 Juni, 2011 saa tano asubuhi. Kuna wasiwasi hata hivyo kuwa hotuba yake inaweza kukumbana na “khitilafu za kiufundi” ambazo zitasababisha vyombo vya habari kushindwa kuirusha moja kwa moja kwa mamilioni ya Watanzania kama ilivyotokea mwaka jana na hakuna lolote ambacho upinzani wanaweza kufanya kubadilisha hilo.

Mwandishi Wetu – DODOMA

3 Comments
  • Hilo la kuongeza bajeti huku kinacho ongezwa ni kulipa posho kipo wazi kwamba bajeti ina bakipalepale sawa na ile ya mwakajana hapo watz hata ambao hawajasoma waone wazi.
    KUBWA ni hili la kufuta kodi kwa wazalishaji na wasafirishaji w maua nje ya nchi,ni hatari kwani wawekezaji kuzidi kuja inamaana Eneo kubwa la Ardhi litazidi tumiwa kwa kilimo hicho cha biashara kinacho wafaidisha wazungu kwani:Adhi wanayo itumia wakiondoka hua haifai tena kwa kilimo cha chakula sababu ya kemikali nyingi wanazotumia na zina waadhiri sana waTanzania huku wakiondoka hawafanyi LadReclamation.Sasa tumeona bonde la Rubada wakulima wameacha panda mazao ya chakula na kupanda Maua yakusafirishwa nje,Tayari hapo Mustafa mkulo sera yenu ya kukabiliana na njaa pitia Mkukuta haitafanikiwa huku pia kemikali hizo zitachangia ongezeko la joto na hapo ukame utazidi hivyo mkakati wa kupunguza ongezeko la hewa chafu(co2)hautafanikiwa.Sasa nini mnafanya Ndugu yangu Kikwete na Mkulo?Mlienda darasani kukariri maarifa si kuelewa?au mnaelewa sema ni ukoloni mamboleo wa kutimiza matakwa ya mzungu? Bajeti isifikirie Afya za Watanzania si pesa haramu.Bajeti gani inayo weka mslahi ya wazungu mbele huku ya waTanzania nyuma?

  • serikari mnatupereka wapi,other members from other parties were are you you waiting for kabwe to say about the embezzlement of minister of financial is a shame to you ‘Big up to Zito of coarse you after for tanzanians benefits.

  • mimi naungananao kuipinga nakuikataa bajeti ya serekaki hiihaija jikita katika maeneo mhimu ya kijamii kama vile elimu,afya,na kuangalia maisha ya watanzania wakiwango cha chini ambao ndo wengi sana badala yake wameendelea kungangania posho na kuongezewa misha hara na kutembelea magari ya kifa hari ya gharama kubwa….

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *