Shule ya msingi ya Kinyambwiga iliyopo kata ya Guta wilayani Bunda, inakabiliwa na uhaba wa madarasa na madawati hali inayowapa wakati mgumu walimu na wanafunzi wa shule hiyo.
Kutokana na hali hiyo wanafunzi wanalazimika kusomea chini ya miti huku wakikalia mawe na wengine wakikalia mabanzi.
Mwalimu wa somo la stadi za kazi darasa la sita B Kastori Mng’ong’o, anasema inamwia vigumu kufundishia chini ya mti kwani watoto wanakosa utulivu na kuiita hali hiyo kwamba ni “msingi mbaya kwa wanafunzi hao.”
Anasema wanafunzi wakiwa hapo nje wamekuwa wakipoteza utulivu pale wanapoona mtu au gari linapita, na kuondoa usikivu ambao ni mhimu sana kwa mtoto katika kujifunza.
PICHA: Wanafunzi wa darasa la tano, Shule ya Msingi Kinyambwiga wakiwa darasani
Mwanafunzi wa darasa la sita Ubwe Juma anasama inampa wakati mgumu kupangilia mwandiko wake, kwani mara nyingi mawe anayoandikia hutingishika na wakati mwingine kudondoka kabisa.
Anasema pamoja na mwandiko kuwa mbaya bado suala la usafi kwao ni gumu kwani mawe hayo yana vumbi na kujikuta wakisoma huku wakiwa wamechafuka.
PICHA: Wanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Kinyambwiga wakiwa darasani
Mwalimu mkuu wa shule ya Kinyambwiga Leornald Mukama anasema kumekuwa na mipango ya kujenga madarasa lakini bado wanasubiri kwani yeye hana uwezo wa kufanya lolote.
Mkubwa hayo ndio mambo ambayo tunataka sisi watanzania,maana kwa sasa serikari yetu imechangan`ya utendaji na siasa.ndio mwisho wake unakuwa hivyo,lakini kama ingekuwa huko kwa wenzetu.waziri husika inatakiwa ajiudhulu.
It is simply incredible and unacceptable in such a wealthy country!
Yaani ukiwaona watoto walivyochafuka utadhani wajenzi, ndio hivyo tena desturi ya viongozi wetu kujiuzulu bado haijawafikia.
Hivi kweli elimu Tanzania namna hii itaendelea?