Pichani ni afisa mtendaji wa kijiji cha Mkili kilichopo kata ya Liwundi mwambao mwa ziwa Nyasa wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.Hii ndiyo ofisi ya serikali ya kijiji ambako shughuli zote za serikali zinafanyika hapa.
Afisa mtendaji wa kijiji hicho Aratas Mwakipokile ameelezea masikitiko yake kuhusu kijiji hicho kushindwa kujenga ofisi ya kijiji yenye hadhi na hata samani hazipo.
Afisa mtendaji wa serikali ya kijiji cha Mkili Bwana Aratas Mwakipokile akiwa ofisi kwake. Anasema mazingira ya duni ya kazi yanamkatisha tamaa na kutamani kurudi wilayani Ludewa ambako alikuwa awali kabla ya kuhamishiwa kwenye kijiji hicho.
Anadai kuwa licha ya kijiji hicho kuwa na watu karibu 400,kijiji kinakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo ukosefu wa maji safi na salama kwa kuwa wananchi wanatumia maji ya mito na ziwa ambayo sio salama.
Kijiji hakina kisima wala bomba na hata wananchi wake wamekuwa wagumu kujitokeza kwenye kazi za kujitolea.
Miaka 50 ya Uhuru na Tanzania tuitakayo