Mbinu za kupata habari

Latifa Ganzel

Wakati mwingine inakupasa kukaa hadi katika vilabu vya pombe , unywe  hata kidogo japo hujazoea, hii inakusaidia kujua kero, matatizo na hata malalamiko ya wananchi kuliko kukaa ofisini na kusubiri kuletewa taarifa, mara nyingi unakuta taarifa sio sahihi.

Hapa nilipokaa nimepata taarifa kuwa wananchi wa eneo Mahilo yaani hapa tulipo katika milima ya Matogoro wengi kwa sasa hawana shughuli za kufanya baada ya kuzuiwa kulima katika mabonde ambako kuna vyanzo vya maji vya mto Ruvuma ambapo ilikuwa tegemeo lao.

Kazi kubwa iliyobakia kwa sasa ni ya kukaa vilabuni, na vijana wengi kukaa vijiweni, hatari yake wengi wanaweza kujitumbukiza katika wimbi la ujambazi.

Pia wananchi hawa hawaoni faida yeyote wanayoipata kutokana na vyanzo vya mto Ruvu na lipasi vilivyopo katika milima ya Matogoro kwa kile walichodai kuwa hawanufaikia navyo, Souwaso nayo inadai inatoa ajira kwa badhi ya wananchi wa maeneo hayo kulinda vyanzo hivyo.

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *