*Adaiwa kuharibu kamera ya Channel Ten
MLINZI wa Mchungaji Ambilikile Masapila, Fred Nsajile anayedaiwa kuwa ni ‘Ofisa wa Usalama wa Taifa’ anadaiwa kuharibu kamera ya Mwandishi wa Kituo cha Televisheni Channel Ten Jamila Omar.
Mbali na kuharibu kamera, mlinzi huyo anadaiwa kumkwinda mdada huyo na kumwamuru aondoke eneo la kutolea huduma nyumbani kwa Mchungaji Masapila.
Tukio la mwandishi huyo kukwidwa na kuharibiwa kamera yake lilitokea juzi wakati kampuni ya Vodacom ilipokwenda kuzindua huduma zake kijijini Samunge ambapo Jamila alikuwa moja ya waandishi waalikwa wa tukio hilo.
Akizungumzia tukio hilo mmoja ya watu waliokwenda kupata huduma ya Mchungaji Masapila, Julian Masawe (35) alisema, mara baada ya kumaliza shughuli ya Vodacom walishangaa kumuona mlinzi huyo akianza kumkaribia mwandishi huyo.
“Tumeshangaa kuona huyu dada anazodolewa bila kujua tatizo liko wapi wakati yeye anaonekana amekuja kufanya kazi ya hili tukio sasa huyu mlinzi sijui imekuwa akaanza kumkaribia,” alidai Masawe.
Tayari suala hilo limefikishwa kituo cha Polisi Loliondo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Awali kabla wakati shughuli ya makabidhiano ya simu ikifanyika nyumbani kwa Mchungaji Masapila, mlinzi huyo alidiriki kumzuia mwandishi huyo kuchukua picha za makabidhiano ya simu aliyopewa Mchungaji.
Hata hivyo kutokana na hekima na uelewa wa umuhimu wa vyombo vya habari Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Elias Wawalali alilazimika kuingilia kati mvutano huo na kuamuru Jamila aendelee na kazi yake.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kwamba baada ya Mkuu wa wilaya Wawalali kuondoka eneo hilo ndipo mlinzi huyo alianzisha tena ugomvi na Jamira akimwamuru kuondoka haraka eneo hilo kwani shughuli iliyompeleka pale ilikuwa imemalizika.
“Kazi iliyokuleta hapa imemalizika tafadhali ondoka haraka sana, hapa nyumbani kwa Mchungaji,” alisikika akiropoka kwa nguvu mlinzi huyo na kusababisha wananchi kumshangaa.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Jackson Sandea na Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Michael Lengume na baadhi ya polisi waliokuwa nyumbani kwa Mchungaji walifanikiwa kuzima vurugu hizo baada ya kumzuia mlinzi huyo na kumtaka asiendelee kupambana na Jamira.
Kwa upande wake Jamila akizungumzia tukio hilo alidai kusikitishwa zaidi na kitendo kilichofanywa na mlinzi huyo, ilhali Mchungaji Masapila tangu aanze kutoa huduma hiyo alikuwa na uhusiano mzuri na vyombo vya habari.
Alisema taarifa za vyombo vya habari ndizo zilizosababisha wananchi wengi kuifuata huduma hiyo Samunge,wakiwamo pia viongozi wa Serikalii ambao pindi wanapotaka kwenye wamekuwa wakitoa taarifa kwa vyombo vya habari.
“Hiki kitendo si cha kiungwana kabisa mbali na kumtaka aniombe radhi na kulipa kamera ya ofisi nitaangalia utaratibu wa kumchukulia sheria, amenidhalilisha mbele ya watu wakati nipo kazini,” alidai Jamila.
Kutokana na kuibuka kwa mgomgoro huo na matukio mengine ya vurugu baina ya mlinzi huyo na wananchi, Mwenyekiti wa Kijiji cha Samunge, Lengume aliomba kuwapo na utaratibu wa zamu kwa walinzi wanaoletwa eneo hilo.
Tukio la Jamila kuzuiliwa kufanya kazi yake linadaiwa kuibua matukio mengine ambayo baadhi ya waandishi walijikuta wakipata msukosuko kutoka kwa ofisa usalama huyo.
Waandishi wengine waliojikuta kwenye wakati mgumu wa kufanya kazi zao ni mwandishi wa habari mwandamizi wa gazeti la Mwananchi Nevile Meena na mpiga picha wa gazeti hilo Emmanuel Herman.
Dear Editor,
Mr. Freddy is an employee of Ministry of Home Affairs Dept of Refugees and is based in Kasulu Mtabila camp as government representative. To our knowledge the man was among government employees sent to help patients and relatives in Loliondo when there was an influx of people who wanted to have Babu’s herb. His was to deal with the need of tents since at the time there was heavy rain pounding the country. He was not sent to pretend to be the spokesman of the Babu. He used the chance simply because he allegedly comes from Babu’ place of
origin! What he is doing there is to exploit the name of Babu while pretending to be an Government Intelligence officer. He is simply a civilian with questionable character which has been a dilema and this, all refugees will tell you. They have been his PUNDA for long! He has been beating them and at the same time going about with their daughters. In North Western Region and even his employers in the Ministry will testify that. Now he is pretending to carry Bible as if he is saved, nonsense. He is hoodwinking the old man to believe he is saved where as not. Let Director of Refugee explain if true he is saved! Because she is one of those being hoodwinked and think his man is clean.
What happened to Jamila and others is his typical behavior. Ask any refugee, they will tell you the beating and order for incarceration is from Mr. Freddy is the order of the day.
Secondly, let the public know that he is simply a normal civilian though the way he contradicts people, one would imagine he is from state house, Military inteligence or anybody of that. He is not. Follow up more from the ministry and you will have his real picture.