Ngorongoro yakabiliwa na Uhaba wa Chakula; baa la njaa laja

Jamii Africa

TARAFA za Ngorongoro, Sale na Loliondo zilizopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha zinakabiliwa na baa la njaa.  Mpaka  sasa taarifa  zinaonesha kuwa Tarafa ya Ngorongoro inahitaji zaidi ya tani 1500 za mahindi, tarafa ya Sale na Loliondo zinahitaji zaidi ya tani 1000 .

Kutokana  na kilio hicho cha msaada wa chakula, kamati maalumu imelazimika kuundwa ili kukutana na Rais Jakaya Kikwete kumueleza juu ya tatizo hilo. Mkutano huo uliofanyika jana juu ya majadiliano ya upatikanaji wa uhakika wa chakula uliwashirikisha wadau wa maendeleo na jamii inayoishi ndani ya hifadhi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).

Akizungumza  katika mkutano huo Mbunge wa Jimbo hilo, Saning’o Ole Telele alisema, tatizo la chakula wilayani humo kwa ujumla limesababishwa na ukame mkubwa. “Wananchi wanahitaji chakula kwa sasa kitakacho watosheleza hadi Januari 2012,”alisema Telele.

Kwa upande wake Katibu wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro James Moringe alisema, pamoja na NCAA na Baraza hilo kutenga fedha za ununuzi wa mahindi bado kunahitajika msaada zaidi kutoka serikalini.

Naye mwanasheria wa PWC, Melau Alais akichangia katika majadiliano hayo alisema, ni itakuwa ni vyema kama chakula hicho kikipatikana ndani ya Juni na Julai Mwaka huu. “Mkutano huu umeitishwa baada ya kufanya tafiti na kubaini upungufu mkubwa wa chakula katika wilaya ya Ngorongoro,”alisema Alais. Mkutano huo uliandaliwa na Baraza la wafugaji Wanawake (PWC) uliwateua mbunge wa jimbo hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya, Elias Ngolisa,Mwenyekiti wa PWC Metui Ole Shaudo kuongoza ujumbe utakaokwenda kumuona Rais Kikwete.

Mbali na viongozi hao kushiriki mkutano huo, wengine walioshiriki ni pamoja na  baadhi ya wananchi wanaoishi maeneo hayo, viongozi wa mila, vijiji na madiwani.

Habari hii imeandikwa na mwandishi wa FikraPevu tokea Karatu

6 Comments
  • Na kwa Bajeti hii hakika njaa ita imaliza nguvu kazi Tanzania kwani bajeti inadanganya kuwa ina lengo la kupambana na njaa wakati wawekezaji na wasafirishaji wa Maua wamefutiwa kodi ili wazalishe kwa wingi sasa hapo wote tuna fahamu jinsi kilimo hicho kinavyo tumia kemikali nyingi ambazo ni hatari kwa Watanzania wamazingira yale na wote kwa ujumla.Maeneo hayo pia yakiachwa hayafai tena kwa kiliomo cha chakula na hao wawekezaji hawafanyi Ladreclamation.Hatari ni pale hadi wakulima wandani wanaposhawishiwa kuacha kulima mazao ya chakula na kupanda maua kwa msaasa wao wawekezaji.Sasa je kwa watukuacha kupanda mazao ya chakula,maeneo kuachwa yakiwa hayafai kwa kilimo cha chakula kwa kisa cha Ardhi kuharibiwa na kemikali,pia kwa kemikali kuongeza ongezeko la joto kweli hapo njaa itaiacha mikoa ya Tanzania hasa ile mikame kama kigoma AU maeneo ya Sale,Loliondo n.k?Serikali gani isiyo na FIKRA PEVU?

  • jamani serikari mngekuwa mnaongeza bajeti na watanzania wote wananufaika nayo na siyo wele tu walioko juu ya mti na hao wenzangu chini ya mti wanakufa kwa majanga mbalimbali kam njaa ukame nk kama ilivyo Ngorongoro na sehemu nyingine Tanzania
    so what am ask as economist to our gvt is creat condusive environment as result of encouraging investiments so as to increase high standard of the people among tanzanians who crying for better social welfare.

  • ndugu zangu napenda kutowa pongezi kidogo kwa viongozi wa ngorongoro walio pata waso hii kutangaza swala la njaa linalo wakabili wananchi wa ngorongoro.
    swali ni kwanini wananch wa ngorongoro tuve njaa wakati wa serikali wa Kikweti ? wakati serikali wa nyerere,mwinyi, mkapa wameamuwa kuwapati wafugaji wa ngorongoro kilimo wa kijikimu ili wasife njaa. je kwanini serikali ya Rais kikwetie akubali wafugaji wa ngorongoro wafe njaa na kuwanyima kilimo ndogo wa kijikimu???
    Swali la pili: kwa nini serikali wa CCM wamekua kimiya kwa muda murefu wakati wananchi wa ngorongor wanakufa njaa?
    LAWAMA kwa viongozi wa olbalbal waliokuwa mbali na wananchi yao wano kufa njaa.
    naomba waandishi wa habari waende ngorongoro washudie maafa ya njaa huko ngorongoro na wahoji wananchi wa ngorongoro.
    by m.k.olesembeta

  • Ngorongoro inatupa taabu tupu, kwani serikali wanatambua kuwa wafugaji tunaoishi Ngorongoro wametufutia kilimo ya kujikimu, Ardhi hatuna ni serikali na UNESCO/IUCN, mikopo hatupati kwani benki gani wa kumpa mtu asiye na hati yoyote besa ya mikopo, Ngorongoro Conservation ambayo ndiyo mama hawezi kamwe kutoa mikopo, je ni lini maisha ya Ngorongoro kwa wenyeji itabadilika? Kwani serikali wasikubali tugawane mapato yanayopatikana kutokana na Watalii wanaoingia pale. Wakati bajeti ya NCAA sasa ni 53 Billion kwa mwaka. Mimi ninafikiria kupewa mahindi imepitwa na wakati, serikali kutufanya kuku watu wanao ishi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro waache. Inaniuma kuliko jinsi ninavyo andika

  • Nawapongeza vijana wanao towa maoni yao kuwasaidia wananchi kupata maelekeo ya kujitambua wao ni kinani ndani ya hifadhi ya ngorongoro.

    Naomba niwahulize maswali tu kwa leo:

    KWAKUWA TUNAJUWA KWAMBA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO INA MAJIKUMU YA KUWAENDELEZA WANYEJI HAO WA NGORONGORO.JE WEMEFANYA NINI KTK MIAKA 50 YOTE? WAKATI WATUNYIMA ELIMU WAKATI NDIYE UKOMBOZI YA KILA MWANADAMU.WAMETUNYIMA KILIMO YA KIJIKIMU? MBAKA SASA WANACHI WANAKUFA NJAA.

    JE BARAZA LA WAFUGAJI WANAFANYA NINI? WAKATI WAFUGAJI WA NGORONGORO WAMENYIMWA CHAKULA YAANI KILIMO YA KIJIMU? TUMEONA BARAZA WAPO TU KAMA KIBARAKA YA NCCA.KASABABU WANATAKIWA WAPNGANE MNYANYAZO SINAZO TOLEWA NA NCCA.

    JE MWAKILISHI ANAYE TUWAKILISHA WAFUGAJI NDANI YA BODI YA NGORONGOROANAFANYA NINI? WAKATI WAFUGAJI WANAKUFA NJAA?

    JE SERIKALI YETU YA CCM WATOWA TAMKO GANI KWA HAWA WFUGAJI WANAO KABILIWA NA NJAA KALI?

    NAOMBA BAZARA LIUNDWE UPYA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *