WAKATI Polisi wakiendelea kukosolewa kwa kutumia nguvu kubwa kuzuia matukio ya uhalifu,polisi mkoani Kagera wamemuua kwa risasi mchimba madini mdogo wilayani Biharamulo ambaye jina lake halijafahamika.
Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na kamanda wa polisi mkoani hapa Henry Salewi maujai hayo yalifanywa na polisi baada ya kutaka kulidhibiti kundi la wananchi waliodaiwa kutaka kumchoma moto Samwel Marwa kwa tuhuma za kuiba madini ya dhahabu.
Alisema katika jitihada za kumuokoa kijana huyo asichomwe moto kwa wizi wa madini polisi walimpiga risasi mtu huyo na kuwa baadhi ya askali waliotoka katika kituo cha polsi Mavota walijeruhiwa kwa mawe na wananchi.
“Askali wawili wamejeruhiwa kwa kushambuliwa kwa mawe na wachimbaji wa madini,walitaka kumuokoa mmoja wa wachimbaji wadogo ambaye alikuwa katika hatari ya kuchomwa moto kwa tuhuma za kuiba madini”alisema Salewi
Maujia hayo yalifanywa na askali wa kituo kidogo cha Mavota kwa kushirikiana na askali wa oparesheni wa wilaya ya Biharamulo na kuwa marehemu laikuwa miongoni mwa wachimbaji wadogo waliokuwa wakimuadhibu mtuhumiwa.
Pia Salewi alisema baadhi ya wananchi walitoa taarifa za kuwepo kwa kundi kubwa la vijana lililokuwa linamwadhibu mtuhumiwa wa wizi wa madini ambapo maujai hayo yamefanyika juzi katika eneo la mgodi wa madini ya dhahabu wa Tulawaka unaomilikiwa na kampuni ya Barrick.
Alisema watuhumiwa wanne wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano na kudai kuwa wamekamata lita tatu za mafuta aina ya petrol yanayodaiwa yangetumika kukatisha uhahi wa mtuhumi ambaye aliokolewa huku mwingine akiuwawa na polisi.