Rais Kikwete akutana na viongozi wa madaktari waliogoma Ikulu

Jamii Africa

Rais Jakaya Kikwete, amefanya kikao cha ghafla na uongozi wa madaktari ambao wameanza mgomo wao upya wakidai maslahi zaidi na kuboreshwa kwa mazingira ya kufanyia kazi ili kutoa huduma bora.

Rais Kikwete ambaye leo alikuwa akutane na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam sasa atakutana na wazee kesho, Jumamosi, Machi 10, 2012.

Ilielezwa kwamba mkutano wa wazee na Rais umeahirishwa ili kutoa nafasi kwa Rais kufanya mashauriano zaidi na wadau mbali mbali kuhusu suala ambalo Rais atalizungumzia kwenye mkutano huo.

Kama ulivyokuwa mkutano ulioahirishwa leo, mkutano wa kesho utafanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia saa tano asubuhi.

3 Comments
  • dat was a wise idea….mr President…
    The issue is that…will the minister and his deputy wth hearted revamp on doctors longterm claims, wen the kamati is resolved and those claims shifted to be solved by the respective organ(MoH)? I dnt get connection into my mind…!!

  • JK atakuwa amethubutu iwapo iatakuwa amefikia muafaka na madaktari kuliko ilivyokuwa akimwachia mtoto wa mkulima ili hali akijua hana maamuzi wala usemi…..

  • JK kuwaachisha ngazi Waziri na naibu wake ni lazima ili kutoa mfano na iwe fundisho kwa mawaziri wengine kutokuchukulia nyadhifa zao kama zawadi au urithi na huo utafunguwa ukurasa mpya wa uwajibikaji, Ngeleja nae afuatie maana Arusha umeme hakuna kila saa wanakata,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *