Katika hali isiyo ya kawaida akinamama wanaoenda kujifungua katika kituo cha afya cha Kinesi, kilichopo kata ya Nyamunga wilaya ya Rorya mkoani Mara , wanafungiwa kondo la uzazi na kwenda nalo nyumbani baada ya kujifungua, hii ni kutokana na kukosekana kwa shimo la kutupia taka katika kituo hicho cha afya.
Mkunga muuguzi katika kituo hicho Nyakibore Bulenga anasema wanalazimika kuwafungia akinamama kondo hilo la uzazi baada ya kujifungua, kutokana na kujaa kwa shimo la kutupia taka za aina hiyo.
“Tumeshatoa taarifa kwa mganga mkuu wa wilaya lakini hakuna kilichofanyika kama unavyoona mwenyewe” analalamika.
Naye mganga mkuu wa kituo hicho Ngocho Marwa anasema ni miaka miwili sasa hawana shimo la kutupia takataka za aina hiyo, na tayari uongozi wa kijiji ulishapewa taarifa lakini hakuna kilichofanyika.
PICHA: Makazi ya wahudumu wa afya wa kituo cha Kinesi
“Tunajisikia vibaya kuwabebesha akina mama taka za aina hiyo, ila hatuna namna kwani tukilazimisha kujaza ndani ya shimo lililopo, basi mbwa hufanya sherehe kwa kusambaza taka hizo na kuhatarisha afya kwa wagonjwa” anaeleza.
Pamoja na tatizo hilo la kukosa shimo la kutupia taka, kituo hicho cha afya kinakabiliwa na uhaba wa maji hali inayowalazimu wajawazito kuja na maji wanapokuja kujifungua.
Habari dada, habari nzuri.
lakini, habariinahusu shimo la kutupia kondo la nyuma halafu picha inaongelea makazi ya wauguzi. its not relevant weka picha ya shimo hilo. Au uonyeshe akina mama wakija na maji, wakati wa kujifungua.
Asante.
Ni kweli kabisa, kichwa cha habari na picha ni tofouti kabisa
Ni kweli picha na story ni tofauti kwani nilikatazwa kuweka picha inayoonyesha shimo lililojaa placentas kwa kile niliambiwa si maadili ya uandishi.