Sera zinakwamisha maendeleo ya sekondari za kata!

Eva-Sweet Musiba

Afisa Elimu Taaluma, Elisanguo Mshiu anasema kuwa shule za Sekondari za kata ni mkombozi katika kuinua elimu Mkoa wa Mara ingawaje kuna changamoto mbalimbali zinazozikabili shule hizo ikiwa ni pamoja na  kutokuwa na ufaulu mzuri tangu shule hizo zilipoanzishwa mwaka 2005/2006.

Anasema katika mtihani  wa mwaka 2011 ufaulu  ulikuwa asilimia 53.61 ambapo jumla ya wanafunzi 9,020 sawa na asilimia 53.61 walifaulu na 7,806 walishindwa sawa na asilimia 46.39, ambapo  daraja la kwanza  walikuwa 1,020 sawa na asilimia 0.61,daraja la II walikuwa  271 sawa na asilimia 1.61 na daraja la III walikuwa 987 sawa na asilimia 5.87 na daraja la IV walikuwa 7660 sawa na asilimia 45.52 walioshindwa walikuwa 7,806,kwa takwimu hizo unaweza kuona kuwa kiwango cha elimu Mkoa wa Mara bado kiko chini.

Mwaka huo huo hakuna shule ya kata hata moja iliyofaulu kimkoa hata kitaifa,takwimu zinaonyesha kuwa Shule za binafsi pia za kidini ndizo angalau zilipata ushindi kimkoa lakini kitaitaifa zikawa pia zimekaribia kushika mkia.

SHULE

UFAULU KITAIFA

KIMKOA

Makoko Seminari

94

1

Kowak Girls Sekondari

61

2

Ikizu Sekondari

94

3

Musoma Technical

104

4

Nyabihore

114

5

Tarime

143

6

Chief Wazangi

156

7

Isenye Sekondari

161

8

Mwembeni Sekondari

162

9

Mara Sekondari

168

10

Mwaka huo huo walioandikishwa kufanya mtihani walikuwa 16,329 kwa shule za Serikali katika vituo 162 ambapo waliofanya mtihani walikuwa 15,716 sawa na asilimia 96.25 utoro mashuleni walikuwa 613 sawa na asilimia 3.75 ambapo matokeo yaliyoshikiliwa kutokana na kushindwa kulipa ada ya mtihani kwa muda mwafaka na ili kukomboa matokeo yako unapaswa kulipia Sh. 90,000 kwa mujibu wa kanuni za baraza la Mitihani ambalo liliundwa mwaka 2013 chini ya sheria iliyounda  baraza la mitihani Tanzania  ya mwaka 1973.

Mbali na matokeo hayo Afisa Taaluma anasema kuwa pamoja na wanafunzi kutopata ufaulu huo,lakini shule za kata ni mkombozi kwani zimefundisha watoto ustaarabu, kujitambua kiutaifa, uzalendo, kutambua sheria za nchi na kuzitunza,ambapo wanapohitimu wanakuwa raia wema kutokana na elimu waliyoipata kwani wengi wao wanakuwa wamepata stadi za maisha (Life Skills) pia zimesaidia kuchangamana katika jamii na kusababisha ushirikiano kati yao.

Shule za kata zimechangia  kupunguza mimba za utotoni, watu wanafahamu kuwa huyu ni mwanafunzi, hivyo kumwoa ama kumpatia ujauzito ni kinyume cha sheria na endapo akibainika anapata kifungo cha miaka 30 jela.

“Mtoto anamaliza darasa la VII  akiwa na miaka 13 ana 14 kweli huyu mtoto unaweza kumwajiri,anapokwenda Sekondari anapevuka akili na kutambua jambo na kufnaya kazi pia kupata ajira,mikoa mingine kuna shule za kata ambazo wanafunzi wanafaulu na kwenda mpaka vyuo vikuu na wengi wao wanajiunga VETA,kozi za ualimu, Shahada na ndio hao hao wanaotoka katika shule hizo”Alisema Mshiu.

Shule za Sekondari za Serikali zilizopo Mkoa wa Mara zina jumla ya wanafunzi 79,282 kati ya hao wavulana wakiwa 47,916 na wasichana 31,367 ambapo Kidato cha IV-Vi ukiongeza za binafsi una  jumla ya wanafunzi 88,703 wavulana wakiwa 51,288 na wasichana 37,415.

Kwa upande wa wazazi, Lona James Mkazi wa kijiji cha Matare, Nyamongo Wilaya ya Tarime anasema kuwa mtoto kukosa malezi ya wazazi na ufuatiliaji kwa masomo yake na kujua mwenendo wa masomo ya mwanae ndio chanzo cha wanafunzi kutofaulu katika mtihani wa wao.

“Tatizo linalochangia watoto wengi kutofaulu ni watoto kutokuwa na wazazi,ama kuwa na mzazi mmoja labda Mama peke yake ni tatizo, Mama huyo huyo atafute chakula,fedha kwa ajili ya karo,ladda ni Mama lishe inakuwa ngumu kwani tumekuwa tukijishughulisha sana na kutafuta fedha na kusahau kuangalia maendeleo ya mtoto hili ni tatizo kubwa Mwandishi”Alisema Lona.

Naye Mkuu wa Sekondari wa Baruti ambayo ni moja wapo kati ya Shule za kata zilizopo katika Manispaa ya Mji wa Musoma, Mkoani Mara, Anna Nshama anasema utawazi umeharibu wanafunzi.

“Utandawazi umeleta shida, wanafunzi wamekuwa wakija na simu za mkononi na mwalimu awapo darasani akifundisha wao wanachezea simu hasa wanafunzi wa kike,kwa bahati njema tumeshika simu zao zipatazo 10 na kuwaita wazazi wao ambao pia wanakataa  kutowanunulia simu hizo, wazazi walipewa somo la kujua shria za shule kuwa ni marufuku mwanafunzi kuwa simu za mkononi, wakazichukua lakini wakifika nyumbani kazi ni zile zile za kutafuta wenzao kwa  mitandao mbalimbali face book, hata kuangalia picha zisizofaa, badala ya kuzingatia masomo ili tatizo kubwa sana tunaiomba Serikali iangalie upya wanaotengeneza mapicha hayo,Taifa litakuwa la watu wasio na maadili”Alisema Nshama.

Aliongeza kuwa kwa upande wa wavulana pia tatizo pia lipo kubwa, wanavaa mavazi yasiyofaa, (mtepeto) suruali au kaptula inashuka mpaka nguo ya ndani inaonekana, unywaji wa pombe aina viroba, wanakunywa kwani vinauzwa bei ndogo anaweka mfukoni anakunywa,huku ni mwanafunzi.

Lawana pia zikiwaendea wazazi ambapo kwa mara nyingine tena, Mwalimu Mkuu anatanabaisha kuwa, wazazi wasipokuwa makini na watoto wao, Mmomonyoko wa maadili unakwenda kwa kasi sana,kwani adhabu zinapotolewa kwa wanafunzi wanawafokea walimu.  

Akizungumzia   juu ya sheria ya vikobo ameiomba Serikali kurudisha adhabu hiyo kwani inamlea mwanafunzi na walimu bila kumchapa viboko mwanafunzi hawezi kuendelea mbele.

“Wanafunzi wamekuwa hawana heshima, hapo awali fimbo zilisaidia sana kumrekebisha mwanafunzi lakini sasa Mh! sheria hii ya fimbo tatu na nne ya nyongeza ya Mwalimu Mkuu hazitoshi,mwanafunzi anahitaji usimamizi wa hali ya juu na sisi walimu tunataka kuwaweka kwenye mstari ili waweze kupata maisha  bora, lakini tukiende hivi hivi kama watoto wa kizungu hatutafika” Alisema Nshama.

Alisema kuwa tatizo jingine la Shule hizi, bado wanafunzi wengi hawazikubali kuwa ni shule halali na ni nzuri kwao, pia wana dhana kuwa wanaweza kuishi maisha mazuri bila kuwa na elimu, dhana hii ni potofu kwani elimu ndio kitu kikubwa katika maisha hayo.

Shule ya Sekondari Baruti ni moja ya shule za kata zipatazo 13 zilizopo katika Manispaa ya Musoma, ina jumla ya wanafunzi   587 wavulana wakiwa 278 na wasichana 309, ambapo ina mikondo 11 ambayo haitoshelezi, Shule ingepaswa kuwa ni mikondo 16, lakini mikondo iliyopo mpaka sasa ni 9, ambapo kwa mwaka huu Shule imepokea wanafunzi wanaoingia Kidato cha I ikiwa ni jumla ya wanafunzi 164, wavulana 85 wasichana 79.

Pamoja na ufaulu duni katika shule hiyo, pia kuna changamoto mbalimbali za sera za vyama vya siasa ambapo lawama kubwa zilitolewa kutoka kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuwa sera zake zimesababisha wazazi kutolipa ada na shule  kudaiwa Jumla ya Sh. Milioni 8   nyingi zikiwa za vifaa vya maabara (chemicals) kwa ajili ya kufundishia wanafunzi .

Sera ya CHADEMA ya Elimu ni kukosomesha wanafunzi bure kuanzia Shule za Msingi hadi Chuo Kikuu.

Sera hiyo imesababisha wanafunzi kutochukua vyeti vyao ambapo kuanzia mwaka 2010-2012 kuna jumla ya vyeti vya kuhitimu kidato cha IV vipatavyo   155 ambavyo   wazazi wanadaiwa fedha za ada za wanafunzi.

Shule kutokuwa na walimu wa masomo ya Sayansi, kemia, fizikia, baiolojia, na Hisabati pia ni changamoto kubwa iliyopo katika Shule hiyo.

Lawama ikatolewa kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi kutotoa mwelekeo mzuri wa shule za kata ni nani mmiliki wake ni Wizara ama Tamisemi, Mwalimu Mkuu anasema.

Shule za kata zipelekwe Serikali Kuu kwani Tamisemi zinaingiliana na sera za vyama vya siasa, huo ndio utakuwa ufumbuzi  wa tatizo ili Shule ziweze kujiendesha .

Takwimu zinaonyesha kuwa shule ya sekondari Baruti haina ufaulu mzuri kwa mtihani wa kidato cha IV kuanzia mwaka 2010-2013.

MWAKA

DIV. I

II

III

IV

0

2010

0

0

1

35

108

2011

0

0

3

71

46

2012

1

1

1

35

55

2013

0

6

21

52

56

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *