Ni kawaida ya watu wengi kuangalia utabiri wa hali ya hewa kabla ya kutoka nyumbani na kwenda katika majukumu ya kila siku. Tunapata taarifa za hali ya hewa kupitia vyombo vya habari au simu za mkononi zenye intaneti.
Kimsingi inasaidia kufanya maamuzi ya kubeba mwamvuli au miwani ya jua. Utabiri wa hali ya hewa pia unawajulisha watu juu ya majira na nyakati zijazo ili waweze kujiandaa na chochote kinachoweza kutokea.
Umeyafanya maisha yetu kuwa rahisi, lakini umewahi kujiuliza au kustaajabu ni jinsi gani vyombo vya habari vinafahamu hali ya hewa itakayotokea kwa kipindi fulani kijacho?
Jinsi mifumo ya hali ya hewa inavyofanya kazi
Jibu la la swali hili lisilo na mwisho linajikita zaidi kwenye mahesabu na uchunguzi wa data na takwimu. Vyanzo mbalimbali kama vituo vya hali ya hewa, setilaiti, maboya ya baharini, meli na ndege za biashara zinakusanya taarifa na data maeneo yote ya dunia.
Kwa muktadha huo, kila siku vyombo hivyo huchunguza data nyingi kwa wakati mmoja.
Kompyuta mpakato za kawaida tunazotumia kwa matumizi binafsi haziwezi kuchambua data kubwa za hali ya hewa. Kinyume chake zinachambuliwa kwa kutumia kompyuta zenye utendaji mkubwa wa kimahesabu (Supercomputers).
Wanasayansi wanatumia kompyuta hizo kutengeneza utabiri. Pia wanatumia njia za kimahesabu za kuangalia mwenendo wa hali ya hewa iliyopita na geografia ya eneo husika.
Picha iliyopo hapo chini inaonyesha chati ya utabiri. Mistari ya njano inawakilisha eneo lenye upepo wa kawaida au mkali, na mikunjo ya rangi nyekundu inawakilisha mawingu meupe; kimsingi ni mawingu ya tufani, maeneo hayo yanauwezekano mkubwa wa kupata vimbunga na mvua ya m awe. Mistari ya kijani inawakilisha mwelekeo wa upepo.
Data za uchunguzi ni nini?
Data za uchunguzi ni orodha ya vitu vinavyoathiri hali ya hewa kwa namna moja au nyingine. Lakini kila kitu kina faida zake.
Joto na unyevunyevu
Moja ya mambo ambayo tunayoangalia kila siku ni joto. Ongezeko la joto ardhini kwa kiasi kikubwa huchochea mvukizo (evaporation) na matokeo yake ni uwezekano wa kuongezeka kwa mvua au barafu.
Shinikizo na Upepo
Kulingana na shinikizo la hewa tunapata maeneo ya aina mbili- maeneo yenye shinikizo kubwa la hewa na maeneo yenye shinikizo dogo la hewa.
Tunafahamu kwamba vitu vinatembea kutoka kwenye maeneo yenye mgandamizo mkubwa wa hewa kwenda maeneo yenye mgandamizo mdogo wa hewa. Hivyo hivyo, upepo huvuma kutoka kwenye maeneo yenye shinikizo kubwa kwenda kwenye maeneo yenye shinikizo dogo.
Kasi ya upepo huamuliwa na tofauti ya shinikizo la eneo husika. Ikiwa utofauti utakuwa mkubwa na kasi ya upepo itakuwa kubwa. Tofauti ya joto katika maeneo hayo mawili ina matokeo mbalimbali ikiwemo mvua za mara kwa mara au vimbunga na ngurumo.
Kiwangoumande
Ukiangalia glasi ya maji baridi kuelekea kwenye jua au majani kwenye bustani wakati wa asubuhi lazima utaona matone ya maji yakichuluzika. Matone hayo ya maji yanaitwa umande.
Kama joto liko kwenye kiwango cha chini, hewa inachanganyika na mvuke wa maji. Kutokea hapo tunaanza kuona maji au mvuke kwenye vioo au madirisha. Joto katika tukio hilo linaitwa kiwangoumande ‘dew point’.
Kwa siku yoyote kama joto na kiwangoumande viko karibu, kinachotokea ni kiwango kikubwa cha mvuke. Kiwango kikubwa cha mvuke wa maji kinasababisha unyevunyevu mwingi na baadaye kuathiri hali ya hewa ya eneo husika.
Hata hivyo, vigezo vya uchambuzi vinaweza kuwa vigumu na hali ya hewa siku zote itabaki kwa kiasi fulani kutotabirika. Hata kama ndio hivyo, naamini uelewa wetu wa mwenendo na utabiri wa hali ya hewa umeongezeka na kuyafanya maisha yanayotuzunguka kuwa rahisi zaidi!