Zanzibar hali bado tete baada ya vurugu za Muungano

Jamii Africa

WASIWASI mkubwa umetanda kwa siku ya pili mfululizo katika mitaa ya miji ya Zanzibar baada ya askari wa jeshi la polisi kupiga mabomu ya kutoa machozi ili kuwatawanya wafuasi wa taasisi za kidini zinaozongozwa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI). Wafuasi hao ambao walikusanyika katika makao makuu ya polisi mkoa wa mjini magharibi Madema jumamosi jioni, kushindikiza kutolewa kwa viongozi wao wanaoshikiliwa kituoni hapo.

Kamishna wa jeshi la polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa aliwaambia waandishi wa habari kuwa wafuasi hao wamefanya uharibifu mkubwa ikiwa pamoja na kuchoma moto makanisa mawili na kwamba watu saba wanaotuhumiwa saba wamekamatwa na jeshi hilo. Akizungumzia kuhusu hali hiyo ofisini kwake Ziwani Mjini Unguja Kamishna Mussa alisema kwamba jeshi lake litaendelea kuwasaka na kuwatia mikononi wote waliopanga fujo hizo pamoja na viongozi wote wa jumuiya ya Uamsho.

“Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar ndio iliyohusika na kuwachochea vijana kukusanyika na kufanya uharibifu ikiwemo kuchoma moto gari, kupanga mawe barabarani na kufanya hujuma mbali mbali kinyume cha sheria. Tutaendelea kuwasaka kwa gharama zote” alisema Mussa wakati akihojiana na FikraPevu.

Kamishna alisema kwa sasa mikusanyiko yote ya mihadhara ya kidini na vyama vya siasa lazima ipate kibali cha polisi vyenginevyo jeshi lake litatumia nguvu za ziada kutawanya mikusanyiko hiyo ili kulinda sheria za nchi, amani na utulivu.

Maeneo kadhaa na mji wa Zanzibar hasa Darajani na Michenzani ambapo muda wote ni sehemu ambazo zenye harakati nyingi za biashara jana zilikuwa zimebakia tupu kutokana na askari waliojihami kufanya doria katika mitaa yote na kuripua mabomu kila penye kikundi cha watu waliokusanyika wakinywa kahawa. Mitaa hiyo ilikuwa imechaguliwa na mawe, matufali na magogo yaliowekwa barabarani kuziba njia kuzuwia magari yasipite huku mipira ya magari ikiwashwa moto na vijana hao.

Hata hivyo Kamishna wa Polisi alijizuwia kuhusisha harakati za Uamsho na chama cha siasa pamoja na kukataa kutaja majina ya viongozi ambao tayari wanashikiliwa na jeshi lake. “Mpaka sasa hivi sina majina yao kwa jumla lakini tumewakamata viongozi wa Uamsho na tunatendelea kuwasaka lakini jina moja tu ndio ninalo ambalo ni Mussa Abdallah Juma” alisema Kamishna huyo.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Bishop Dickoson Maganga alisema watu wasiojulikana walivamia kanisa lao eneo la Kariakoo Mjini Zanzibar majira ya saa 4.30 usiku na kuvunja ukuta, kuchoma viti vya plasitiki pamoja na gari yake. “Nasikitika na tukio hili ambalo tayari tumeiarifu polisi ambao jana usiku walifika hapa wakishirikiana na kikosi cha kuzima moto na kufanikiwa kuuzima moto huo ambayo kwa habati nzuri haujaathiri paa la kanisa letu” alisema kiongozi huyo. Alisema kundi la watu ambalo lilikuwa likitoa maneno ya kashfa na kutishia maisha ya waumini waliokuwa wakifanya ibada usiku huo kukatisha ibada hiyo pamoja na kusababisha uharibifu wa mali ya kanisa hilo yenye thamani ya zaidi ya shilingi millioni mia moja. Kutokana na hali hiyo jumuiya ya Uamsho imetoa taarifa yake kwa vyombo vya habari kwa kukanusha kuhusika na kuchochea watu kuchoma kanisa pamoja na kuharibu mali za watu.

Hata hivyo Katibu wa Jumuiya hiyo, Abdallah Said alisema katika taarifa hiyo kwamba jeshi la polisi linapaswa kubeba lawama kwa yote yaliotokea kutokana na kuvunja sheria na kuwakamata viongozi bila ya utaratibu wa busara. “Uislamu ni dini ya amani na inahimiza mashirikiano na utulivu na hatuwezi kuwatuma watu kwenda kuvunja makanisa na kuharibu mali kwa sababu ndani ya imani zetu tunajua hilo ni kosa na jambo ambalo halifai katika maarisho ya dini yetu” alisema Sheikh Abdallah.

Taarifa hiyo ilisema pia kwamba Uamsho imekuwa wazi katika kudai maslahi ya Zanzibar na sio vyenginevyo na kuahidi kufanya hivyo kwa njia za amani na iwapo watakuwa wamekosea basi wapo tayari kufikishwa katika vyombo vya sheria.

“Ni lazima polisi wajue kwamba tupo tayari kufanya kazi kwa misingi ya kisheria na hata kwa kujisalimisha tupo tayari lakini ukamataji busara na sheria haukubaliki na ni vigumu kwa wafuasi wetu kuwadhibiti wasilalamike, tunachokitaka ni kura ya maoni haraka na hilo tutaendelea kulidai” alisisitiza Katibu wa Jumuiya hiyo katika taarifa yake. Wakati viongozi wa Uamsho wakiendelea kutafutwa na jeshi la polisi nyumba ya kiongozi aliyeongoza maandamano juzi Sheikh Farid

Hadi Ahmed inadaiwa kuvunjwa milango usiku wa manane alipokuwa akitafutwa na jeshi la polisi. Hata hivyo taarifa hizo zimeshindwa kuthibitishwa na jeshi la polisi iwapo ni kweli polisi ndio waliofanya kitendo hicho au laa lakini wanafamilia wanasema waligongewa milango na kutakiwa wafungue baada ya kutofungua walisikia kishindo kikubwa cha kusukumwa milango hiyo, nyumba iliyopo eneo la Mbuyuni Mjini Unguja. Vijana katika mitaa ya Zanzibar jana walionekana wakiwa na hamasa kubwa wakidai kuendelea kuungana na viongozi wao kudai haki ya Zanzibar pamoja na kutaka Zanzibar huru kutoka ndani ya mikono ya Muungano.

“Sisi tunachokitaka Zanzibar yetu watupige mabomu, watuuwe, watukamate lakini tunataka Zanzibar yetu na hatusikii lolote” Vijana walisema katika nyakati tofauti.

12 Comments
  • Sio kila mhalifu niwakupelekwa Polisi
    Nimesema hivyo nikiwa na maana kwamba, Suala la hawa wanao jiita wana uamsho sio la Juzi wala jana, nila mda merefu sasa, Nakumbika kituo kimoja cha Televisheni waliwahi kujadili moja ya Mada na hasa wakigusia juu ya Uwepo wa kundi hili na harakati zake za Kuharibu Amani ya nchi hii, lakinni kama hatoshi vyomdo vya habari vingi tu vya Nchini viliripoti juu ya Uwepo wa Watu hawa wasiopenda Aman
    Nikwamba kwakuwa sasa inaonekana SUALA hili kuota mizizi, Naimba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tz. Iliingilie kati.
    Kwanza kuwakamata
    Pili kuwapeleka Mirembe Dodoma
    Tatu Wapimwe Afya ya akili
    Nne Majibu yapatikane
    Tano na Mwisho wapate adhabu kwamujibu wa matokeo ya vipimo.
    Siamini kwa mtu mwenye akili Timamu tuamini kama anaweza kufanya madudu yakuchoma Nyumba za Ibada Moto haingii akilini.

    Naomba niwaaminishe Watanzania wapenda Amani wenzangu hawa watu si wazima Lazima wanawenda wazimu tu.
    Nononoooooooooooooo I, say Noo the Big No hawa ni wagonjwa JAMANI. TAIFA LIELEWE HIVYO.

  • wazanzibari ni wanafiki tena wana roho za kikatili nfuu hata wanyama… wabara tunanyanyaswa kila leo, tunatishiwa maisha kila kukicha. mbona wao huko bara wanaishi kwa amani?……bora tu huu muungano uvunjwe kwani mimi sioni faida tunayoipata zaidi ya wao kutunyonya… by tha way kama uislam ndo unafundisha ukatili kiasi hicho basi hii si dini kabisaaaaa. ukiangalia historia mara nyingi ndo wanaanzisha machafuko almost nchi zote. tuwaelewe vipi……

  • Vurugu za Zanzibar
    Kuna wanaoabudu dini na kuna wanaoabudu Mungu.Siku zote waabudu dini hawawapendi wanaoabudu tofauti na wao.Ni wadini.Udini ni Ugonjwa.Ni ugonjwa wa ubaguzi.Wenye ugonjwa huu hawaamini katika co-existence ya watu wanaoamini tofauti kuishi pamoja.Ni ugonjwa wa siku ningi na wagonjwa wake wana perfect timing.Ni wajanja wa visingizio,safari hii ni Muungano.Makanisa ni alama ya Muungano?Wanadekezwa kwa muda mrefu sasa,Hii ni sehemu tu ya matokeo

    • Marehemu Julius Kambarage Nyerere alikuwa na nia ya kuanzisha bara moja la Afrika chini ya utawala wa Rais mmoja wa shirikisho la Afrika .

      Nia yake ilikuwa ni kuleta taifa lenye nguvu sauti moja na maendeleo kwa wananchi wake. Alianzia Ghana na kukubaliana na viongozi wa Ghana wa wakati huo lakini viongozi wengine walikuwa wabinafsi hawakupenda umoja

      Nini maana yake :hadi sasa bara hili limeachwa nyuma mataifa tajiri ya mashariki na magharibi yameendelea kuchota utajiri wa baadhi ya nchi za Afrika kwa sababu wamekosa umoja

      Mwalimu hakuishia hapo aliona ni vyema Tanganyika na zanzibar kuungana kwa ajili ya maslahi ya taifa letu wengi vijana hawaoni manufaa ya muungano huo lakini kiuuchumi hebu angalieni mfano umeme unatoka Bara

      Pamoja na amani visiwani kwani sultani bado ana hamu na nchi hiyo Muungano umeweka daraja kubwa na kufanya nchi iwe moja.

      Zanzibar karibuni Mungu akipenda mtapata mafuta mkinangania kuvunja muungano athari zake ni kubwa msipoangalia mtakuwa watumwa nyumbani kwenu kwasababu mataifa makubwa yatafanya kila njia kujiingiza kwa masilahi yao

      .Lakini mkibaki kwenye Muungano ni kama kuwa kitu kumoja na ni vigumu kukivunja.

      Chukueni mfano wa Taifa la Marekani lina nchi /state 51 na kila state ina gavana wake /au raisi wake kama ilivyo Zanzibar lakini kuna mambo ya muungano /federal na mambo ya nchi/state

      Federal/serekali kuu ya Muungano haiwezi kuingilia maswala ya state/ Gavana au rais wa nchi anaweza kumhukumu mtu kifo na Raisi wa nchi /Obama asiweze kusema kitu kama ilivyo zanzibar rais Shein na Jakaya Kikwete

      Ni vyema waziri wa vijana akaanzisha semina ya kuwafundisha vijana nini maana ya Muungano na sio kuwaachia vyombo vya dini kufanya kazi hiyo

      Amani na utulivu ndani ya nchi ndiyo maendeleo ya kweli lakini kama hakuna amani mauaji nchi itakuwa kama Somalia

      Tumwombe Mungu atuepushe na hali hiyo na tuombe amani ya kweli na viongozi wanaowajali wananchi wao
      Kma walivyo viongozi wa bara Rais Jkaya . Rais Shein na makamu wa rais kutoka chama cha CUF Sharifu Hamadi

      Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Zanzibar

  • hao wanaojiita uamsho wanamuamsha nani? tuwe honest kidogo nchi almost zote duniani vita zao zinaanzishwa kwa kupitia mgongo wa dini especially uislam, mi nashangaa ina maana dini ya haki au inayoonewa humu duniani ni uislam pekee? ikitokea kitu kidogo mara ooh uislam unaonewa sio haki kabisa.

    Because watu wanaabudu madhehebu tofauti na wako cool mi nataka tujifikiria what’s wrong with Islams/Muslims? ngoja nitoe mfano: juzi kuna kanisa la Efatha lilivamiwa na polisi katikati ya Ibada, wakalipua mabomu ya machozi & risasi! tusiangalie nani mwenye makosa nnachotaka tujiulize ni jee. Polisi wale wangeingia Msikitini na kupiga watu vile Waislam wangefanyaje?

    nikiotea reaction ya waislam wangeandamana, wakavamia kituo cha polisi, wangefanya mhadhara, wangesema serikali yetu ni ya Wakristo na kufanya vurugu siku 3 mfululizo! again what’s wrong with Muslims? ni kwamba wako Inferior? ni mtazamo tu.

  • nyinyi mnazugumuza vitu msivo vielewa bora waulizeni wenye kujuwa kwanini wazanzibar wamefikiya hatuwa hiyo

  • kuna msemo unasema hivi : huwezi kujua umuhimu wa kitu mpaka kiwe hakipo.Leo hii wenzetu wazanzibar hawaoni umuhimu au faida za muungano kwa sababu upo. kuna mambo mengi wanafaidika tena kuliko sisi, kwa mfano siku 1 nilikuwa ktk 1 ya hotel huko;nikaagiza juice ya nanasi nikapewa, kwa kuwa ilikuwa tamu sana nikaagiza nyingine nilijibiwa kwamba boti haijafika kutoka dar,soda ya fanta nayo pia.sasa vitu vidogo tu kama hivyo wanasubiri vitoke bara je ni vitu vingapi wanavyotegemea vitoke bara achilia mbali umeme. kama vipi huo muungano uvunjike lakini wafahamu kwamba siku wakiuhitaji tena hautapatikana. Na kwa kuwa mtaji mkuu wa visiwa hivyo ni utalii,nawaasa hao ndugu vurugu zao zisije zikaathiri hiyo secta hiyo.

  • inawezekana kumaliza tatizo la zanzibar kama watanzaania wanaona sababu ya kulimaliza penye nia pana njia
    tuache giliba tufanye yaliyo ya msingi

  • WAZANZIBARI KWANINI WASIPEWE WANACHOKITA?

    WASWAHILI WANASEMA MTOTO AKILILIA WEMBE MPE. H

    HEBU WAPEWE NCHI YAO?

    • mm ninaishi zanzibar: ninaswali mimi ni mbara AU mtanganyika nilikuwa napenda kuuliza kuwa watanganyika tulioko zanzibar tunanyanyaswa sana na wazanzibar kila ukipita mtaa utasikia wakisema hatuutaki muungano kilamtu arudi kwao je wazanzibar walioko huko bara naowanateseka au wananyanyasika kama wabara tulioko zenji haswa wanawake ndio tunapata tabu. naomba msaada nipate kujua wabara wenzangu nasi tusilate tuamke tusilate tuidai tanganyika yetu sijaona faida ya muungano na zanzibar cjaona chakung’ang’ania.

  • mi kama ndo ningekuwa president mbona ningewapa hawa wazenji hiyo nchi yao wanayoidai..na hawa wazenji ambao wapo huku bara ningewapa siku 30 warudi kwao wote. then kuja bara ni kwa viza… na pia umeme wetu watalipia kwa bei nzuri tu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *