Makumbusho ya Tanzania hayana uasili

Latifa Ganzel

Hili ni gogo la kihistoria ya nchi ya Msumbiji ambalo lilikuwa likitumika kwa viongozi wa nchi hiyo Eduardo  Mondrane Aliyekuwa Rais wa chama cha Frelimo na mkuu wa majeshi wa chama hicho Samora Mashel  kukaa na kujadili mbinu mbalimbali za kupambana na Wareno mwaka 1968 eneo ambalo linajulikana kama Congreso, eneo hili limehifadhiwa kiasili kwa kuachwa miti ya asili inayovutia sambamba na kujengwa nyumba za nyasi na miti zilizokuwa zikutumika wakati huo, eneo ambalo linavuitia na ni moja ya kivutio cha utalii kutokana na madhari yake, hapa kwetu Tanzania katika makumbusho  mablimbali ni kinyume kwani hakuna utaratibu wa kuhifadhi kihistoria kama ilivyo Congress, kwani katika makumbusho mengi hapa nchini vimewekwa vitu ambavyo sio vya asili na maeneo mengine hakuna kabisa, tunapaswa kujifunza kutoka kwa wenzetu.

Ingewezekana hata sisi kuweka makumbusho katika maeneo mbalimbali ya kihistoria ikiwa ni pamoja na katika kijiji cha Mkenda kilichopo mpakani mwa Msumbiji na Tanzania eneo ambalo Msumbiji walianzia kupanga mashambulizi yao ya kumtoa Mreno  kabla ya kuingia Congress.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *