Kwa hili Rostam hautasamehewa – Regia Mtema

Jamii Africa

Nimeamua kuandika habari hii baada ya kujishauri tangu nikiwa Igunga!

Rostam Aziz amekuwa Mbunge wa Igunga tangu mwaka 1994 ambapo mpaka sasa ni takribani miaka 17 chini ya uongozi wake. Nilikuwa sijawahi kufika Igunga kabla hivyo sikuifahamu ilivyo.Siku Rostam anajiuzulu alieleza mafanikio mengi aliyoyafanya Igunga nikadhani Igunga hali ni shwari na watu wanamaendeleo mazuri,nilivyofika sikuamini nilichokiona. Rostam alitudanganya. Katika tembea yangu yote hapa nchini sijawahi kuona Wananchi wanashida kama wa Igunga.

Mambo yafuatayo nimeyagundua katika jimbo la Igunga;

1. Wananchi wengi wa Jimbo la Igunga hawajui kusoma na kuandika mpaka vijana wadogo

2. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 13 kufuata maji kwenye Makomero tena maji yenyewe sio safi wala salama

3. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 10 kufuata shule,wengine wanaenda hadi 20

4. Kwenye kata nilizopita hawaelewi wala kuzijua shule za awali.

5. Wananchi wengi wanatembea umbalimrefu kufuata Zahanati na hayo majengo yenyewe ya Zahanati unaweza kulia.

6. Hakuna barabara za kuunganisha kijiji kimoja na kingine,njia zilizopo ni mapitio ya ng’ombe.

7. Wananchi wengi hawana vyoo wala hawana mpango wa Kujenga vyoo,wao wajenga mabafu tu yanayotumika kuogea na kujisadia haja ndogo,haja kubwa utajua mwenyewe.

8. Zipo Kata ambazo hazing mawasiliano ya simu

9. Lipo Kabila mpaka leo wanatembea uchi kama kwa King Muswati.

10. Wapo wanaotembea karibu Kilomita 13 kufuata TV waone taarifa ya habari na mambo mengine. Hii ni Kata anayotoka Dr. Kafumu

11. Na mengine mengi madogo madogo.

Rostam Aziz

1. Alikuwa ni Mbunge hivyo alikuwa na fursa ya kupiga kelele ndani na nje ya Bunge na akasililizwa.

Rostam alikuwa na uwezo wa kupunguza hayo niliyoyataja kwasababu zifuatazo
2. Alikuwa Mbunge mwenye ushawishi ndani ya chama chake hivyo angeweza kushawishi Mawaziri ili miradi iende Jimboni kwake.
3. Alikuwa Mbunge tajiri sana,kama aliweza kuipa CCM,Mabilioni ya shillingi,Kama aliweza kuhonga watu mbalimbali mamilioni ya shilingi alishindwaje kusaidia Jimboni kwake? aliishia kuwanunulia tu simu Mabalozi wa Nyumba Kumi ili wamfanyie Kampeni.
4. Alikuwa anafahamiana na wafadhili wengi tu wa Maendeleo wa ndani na nje ya nchi alishindwaje kuwashawishi wawekeze kwake?

Rostam aliyaweza haya yote lakini hakujali kwakuwa hakuwa na lengo la kuwatumikia Wananchi wa Igunga. Kwasababu hizo basi nashawishika kusema kuwa Rostam ni zaidi ya DUBWANA ni mtu anayeongoza kwa roho mbaya hapa nchini. Hana huruma hata kidogo, anajali maslahi yake tu.. Bora ulivyojiuzulu, ungejiuzulu na utanzania kabisa, ukaombe uraia wa nchi nyingine huko ughaibuni sio Afrika!

Nawasilisha!

8 Comments
  • Tatizo la viongozi wetu maendeleo katika eneo dogo tena mara nyingi wanatoa kiupendeleo uyazungumza kwa ujumla tatizo ndo hilo kwa Igunga na majimbo mengi yanayosifikaka kimaendeleo hakuna cha kujivunia ni sehemu ndogo ya jimbo ndo utazamwa na si jimbo zima.

  • Hali hii haipo kwa huyu bwana Rostam pekee. Vijiji vingi tanzania vipo hivyo. Ila haya ni matunda ya wananchi kutokukubali ukweli kuwa ccm imeoza. Wananchi amkeni!!

  • Wote tunatambua wazi kuwa kila mwanzo wa mwisho wa vitu flani hujionyesha bila kificho.

    Huu ni mwisho wa mifumo kandamizi, haiwezekani binadamu ukawa na roho mbaya kuliko huyo shetani,ni bora basi hizo pesa ulizoliibia taifa zima ungewanufaisha japo kiduchu wana Igunga kulikoni kujitapa kwenye media kuwa igunga bila wewe haina pa kwenda.

    NA BADO MPAKA MKIMBIE NCHI SAFARI HII.

    • HII NDIYO CCM, VIONGOZI WAKE WENYEWE HAWAJITAMBUI KUWA NI WAJINGA MPAKA HIVI LEO NA NDIO MAANA HAWAJASHITUKA NA KUTAMBUA KUWA WANANCHI WAMESHATOKA. HILI LINAWAFANYA WAENDELEE KUMWAGA PETROLI KWENYE NYUMBA WAISHIYO AMBAPO MKAZI MMOJA NI KICHAA AMBAYE STAREHE YAKE KUBWA NI KUCHEZEA MOTO.

  • TATIZO LA VIONGOZI WETU SIO WAZELENDO NA NCHI YAO BALI WANAJARI MADARAKA NA KULINDA VYAMA VYAO WANAFURAHI KUWA VIONGOZI NA WANAPO SHINDA KATIKA UCHAGUZI HIYO NDIYO FURAHA KWAO NA WALA SIO PALE WANAPO FANYA JAMBO LA MAENDELEO KATIKA MAJIMBO YAO……………SIO SIRI TUNAKUKUMBUKA SANA BABA WA TAIFA (RIP)

  • Tumeshachoka na uongo wa ccm, maana wanahubiri karibia sehemu nyingi za nchi hii kwamba zimeendelezwa na ccm ili hali wananchi bado wanahaha na uchungu wa maisha

  • Vitu vingine kuongelea ni aibu, haya ndio matatizo ya viongozi wetu wengi hasa wa ccm. Diwani wetu wa Goba baada tu ya kushinda ameuwa mradi wa maji ambao ulikuwa unatusaidia sana na kaongea bila aibu kuwa atatukomesha kisa tumemchagua Mbunge wa Chadema. Kwa hili hata Mungu hatomsamehe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *