Mfumo Mpya wa Mabenki kuruhusiwa kuhodhi Akaunti za Pesa za Kigeni kwa wateja wao…

Lara Williams

Leo naomba tutazame kwa kina hili suala la kwenda na wakati na la kiutandawazi ambapo benki za kibiashara na za umma zimeruhusiwa kuwafungulia akaunti za pesa za kigeni wateja wake.

Kuna akaunti za pesa nyingi za kigeni lakini ambazo ni maarufu sana ni akaunti za Dola, ambapo mteja awe mzawa au mgeni atatunza akiba yake na benki ila kwa pesa ya Dola tu. Itampasa kuweka na kutoa Dola tu. Pesa za kigeni nyingine maarufu katika mfumo huu ni akaunti za Paundi na Yuro (Euro).

Ni hatua kubwa katika ukuaji wa sekta ya kibenki na pia ni uboreshaji wa huduma zake kwa wateja wake na wanachi kwa ujumla. Hili limewafaa sana wale raia wa kigeni wanaoishi humu nchini au kuja kutembea kwa muda flani kuweza kupata huduma za kibenki bila kushurutishwa kubadili pesa zao kama hapo awali, na kunufaika ama kupata hasara kutegemeana na thamani ya kubadilishia pesa yao kwa mda huo.

Tukilitizama hili jambo kwa jicho la tatu, tunaweza kugundua kuwa huu mfumo umezidi kushusha thamani ya shilingi na kufanya upatikanaji wa pesa za kigeni kuwa mgumu na mzunguko wake kupungua sanaaa. Watu wengi wamekuwa wagumu kubadilisha pesa zao za kigeni ama kubadilisha kidogo kidogo pale anapohitaji sana tu. Ugumu huo umesababishwa na ukweli kuwa pesa za kigeni hususani Dola, Paundi na Yuro zinapanda bei kila kukicha, hivyo kwa kutokubadilisha pesa zao wanauwezekano mkubwa sanaa wa kunufaika na ongezeko la thamani la pesa hizo za kigeni pindi watakapoziuza.

Kushuka kwa thamani ya shilingi mara kwa mara kumewakatisha tamaa wafanyabiashara na wahifadhi pesa wengi na kuwahamasisha kukimbilia huu mfumo wa kuhifadhi pesa kwa mtindo wa Dola, Paundi, na Yuro. Wafanyabiashara huhifadhi pesa ndogo sana kwa shilling na nyingi katika pesa za kigeni.

Kama hata watanzania wenyewe tunaikimbia pesa yetu ya Shilingi na kujizatiti kuweka akiba katika pesa za kigeni je, tutegemee wageni wafanye nini endapo wazalendo ndio wanaongoza kumiliki akaunti za pesa za kigeni? Je, shilingi inaelekea wapi? Mamlaka zinazohusika akiwepo mkubwa wao Benki Kuu ya Tanzania walitazame hili kwa jicho la tatu.

Mwisho, natoa heshima ya kipekee kwa Rais Mstaafu Ndugu Benjamin Mkapa, kwa mifumo yake thabiti ya kusimamia shilingi na kuhakikisha ilisimaa imara. Kwa vipindi vyote viwili vya utawala wake Dola ilisimamia kati ya Shilingi 800 hadi 1,000. Naomba  na wahusika serikalini wajikumbushe na kujiuliza kidogo, ‘wale wenzetu waliwezaje’?

1 Comment
  • Suala la matumizi makubwa ya pesa za kigeni nchini kwetu linachochewa na wenye mamlaka ya kulidhibiti. Hapa wala tusimng'unye mamneno, Benno Nduru anatakiwa atueleze watanzania amefanya nini kudhibiti matumizi haya mabaya? Hakuna nchi hata moja duniani inayotaka pesa yake iwe strong na inaruhusu matumizi ya pesa za kigeni kiholela kama ilivyo hapa kwetu! Can you imagine, imefikia hata wenye nyumba wanapangisha nyumba zao interms of USD! And mind you our economy is Shilling economy, what the hell is this guy doing? Enzi za mwalimu hata kuonekana na dola ilikuwa balaa na shilingi yetu ilikuwa strong, leo hii sababu ya utandawazi mpaka hata bei ya vyumba hotelini tunachajiwa kwa dola! Mkubwa wa benki kuu katulia anakula mshahara wala haumizi kichwa! Commercial banks kwa nini isitolewe BOT circular ya kustopo mara moja ufunguaji holela wa account za pesa za kigeni mpaka kuwe na ulazima tena kwa idhini ya BOT? Leo hii nikichoka kuwa na shilingi kwenye wallet yangu naingia benki nanunua dola bila hata kuulizwa! Shame on you BOT director!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *