Lowassa kutetewa ndani ya CCM?

Jamii Africa

Kwa wiki kadhaa sasa kumekuwa na dalili zinazoonesha kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Bw. Edward Lowassa anaandaliwa utetezi wa kina ndani ya CCM ili kuweza kumuokoa na mashinikizo ya kutakiwa kujivua gamba. Uchunguzi wa FP ambao umekuwa ukifanyika sehemu mbalimbali na kufuatilia harakati hizo unaonesha kuwa utetezi huo unaandaliwa kufanyika katika ngazi ya wenyeviti wa CCM wa baadhi ya mikoa pamoja na kundi la vijana  wa CCM ambao watajaribu kujenga hoja kuwa Lowassa apewe nafasi ya wazi ya kujitetea ndani ya CCM na vile vile kuwahoji au kutaka wapinzani wake ndani ya CCM wahojiwe kuhusu tuhuma mbalimbali dhidi yake.

 

Hatua mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa ndani ya CCM ili kuokoa jahazi hasa kama vikao vya CCM vitatumiwa kutengeneza ngao ya utetezi wa Lowassa dhidi ya tuhuma mbalimbali. Kinachotarajiwa hasa kutokea ni kuweka mashambulizi dhidi ya viongozi wa CCM ambao wamekuwa wakipiga kelele ya chama kujivua gamba hasa Samwel Sitta, Nape Nnauye na baadhi ya wabunge ambao wanaonekana kugongana na Lowassa. Kwa baadhi ya watu hata hivyo wanaona kuwa juhudi zote hizi kubwa zinaonesha tu kuwa Lowassa hana nguvu kubwa kiasi ambacho kinadhaniwa au kuaminiwa na baadhi ya watu na kwamba mwisho wa siku juhudi zake zitagonga mwamba.

 

Tuneandelea kufuatilia.

1 Comment
  • HAIWEZEKANI KUWAPO WENYEVITI NA MAKATIBU WA VIJANA WA MIKOA 17 DODOMA BADO LOWASA APENDWE BAADHI YA VIJANA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *