Bauxite ni mchanganyiko wa madini ya chuma na aluminium,ambayo ina rangi tofauti,unaweza kuwa njano,nyekundu,nyeupe,blue na hata kahawia. Bauxite pia inapatikana zaidi katika ukanda wa kitropic
Bwana mazingira Richard Lukwaro anasema bauxite ina matumizi mengi,kutengenezea simenti,kula kwa akina mama,mafuta ya kulainisha mitambo,kutengeneza vyombo, na sisi hapa kijijini tunatumia kama rangi ya kupakaza nyumba.
Bwana Lukwaro pia ni msomi na mtafiti, aliongeza kwa kusema madini haya yana asilimia 2.5 ndani yake madini ya dhahabu,pindi unapoichuja.
Mhifadhi mkuu wa msitu wa Shengena bwana frank Mahenge alisema viwanda vingi vya hapa kwetu hujengwa karibu na udongo mwekundu ambao kwa ujumla wake huwa na madini ya chuma na aluminaium.
Aliongeza bauxite ina mchanganyiko wa asilimia 50% chuma na asilimia 50% aluminium,na huwa inaangaliwa vigezo hivyo.
Bwana Isaac Chala,kutoka Kenya anayehusika na kupokea madini hayo, alisema madini ya bauxite ni mchanganyiko wa aluminium na iron ambayo kwa hapa kwetu (Kenya), hutengenezewa simenti(saruji).
Kamishina msaidizi injinia Benjamini Mchwampaka alisema haya ni madini ya viwandani kwa Kenya ambako hupelekwa kuuzwa, hutumika katika viwanda vya simenti, kule Mombasa na Nairobi.
——————————————————————————————————-
BAUXITE NI NINI NA MATUMIZI YAKE
1 Comment
Hoja ya kuwa bauxite inayopatikana Tanga na kupelekwa kenya ati ktumika katika viwanda vya cement haingii akilini..
Kamz hayo ndio matumizi yake kenya mbona Tanga kuna viwand viwili mbona wao hawatumii.
Tungependa kusikia toka kwa geologist wakibongo wakifafanua suala hili jambo.
Vinginevyo vyuo vyetu havitoi wataalamu isipokuwa waliongia chuo kikuu na kutoka na karatsasi linaloitwa degree without elimu.Na tusipoangalia watachukua chookaa yote iliyojaa mkoani Tanga.
Hii hatari