TAHADHARI ya Tsunami: Kuanzia saa moja usiku Tsunami itafika Tanzania na mawimbi yatakuwa makubwa kuanzia muda huo. Taarifa zaidi itatolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wakati wowote kuanzia sasa, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agness Kijazi.
TSUNAMI INFORMATION2 _April11_2012
Earthquake_TSUNAMI INFORMATION _April11_2012
Taarifa zilizotolewa jioni hii, zinaeleza kwamba tahadhari kuu sasa imeondolewa baada ya kutokea kwa tetemeko la baharini pwani ya Indonesia na hivyo kupunguza nguvu ya Tsunami katika eneo la pwani ya Hindi, iliyosababisha kizaazaa katika eneo hilo.
Hata hivyo, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na vyombo vya kimataifa vinaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya bahari, ufuatiliaji unaofanyika kwa saa 24 na kutatolewa taarifa za mara kwa mara itakapobidi.
Ahsanteni sana kwa taarifa hiyo
Wabongo utashangaa wametangaziwa vizuri na mapema kabisa lkn utakuta wanaenda tena kushangaa Tsunami
TMA Tunawaomba waendelee kutujuza maana hali si shwali ukizingatia na mvua inayopiga mpaka mida hii ni balaa.
Wabongo tusibishane na kifo tuizingatie taarifa hiyo